Mmiliki wa klabu ya Leicester City ahusika kwenye ajali ya helikopta

Leicester City football ground

Chanzo cha picha, Liam Hopkin / @hopkin_liam

Maelezo ya picha,

Walioshuhudia walisema waliiona ndege hiyo ikiondoka uwanjani kabla ya kupoteza mwelekeo huku wengine wakisema kuwa waliona moto mkubwa wakati ilianguka.,

Helikopita ya mmilki wa klabu ya Leicester City imeanguka eneo la kuegesha magari nje ya uwanja wa klabu hiyo ilipokuwa ikiondoka uwanjani baada ya mechi ya Ligi ya Premier.

Vichai Srivaddhanaprabha alikuwa ndani ya helikopita hiyo siku ya Jumamosi kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa familia yake.

Mtu mmoja ayeshuhudia alisema aliona mchezaji wa Leicester Kasper Schmeichel akikimbia nje ya uwanja kwenda eneo la ajali.

Haijulikani ni watu wangapi walikuwa ndani ya helikopta hiyo.

Chanzo cha picha, Pete White

Maelezo ya picha,

Wakati helikopta ilikuwa ikipaa kutoka uwanjani

Maelezo ya picha,

Walioshuhudia walisema waliiona ndege hiyo ikiondoka uwanjani kabla ya kupoteza mwelekeo

Leicester ilikuwa imetoka sare ya bao 1-1 dhidi ya West Ham kwenye uwanja wa King Power huku mechi ikikamilika saa moja kabla ya helikopta hiyo kupaa kutoka uwanjani.

Walioshuhudia walisema waliiona ndege hiyo ikiondoka uwanjani kabla ya kupoteza mwelekeo huku wengine wakisema kuwa waliona moto mkubwa wakati ilianguka.

Klabu inasema inawasaidia polisi na huduma za dharura na itatoa taarifa zaidi hivi karibuni.

Chini ya umiliki wa Bw Srivaddhanaprabha, Leicester City ilishida Ligi ya Premier mwaka 2016.

Vichai Srivaddhanaprabha ni nani?

Chanzo cha picha, Leicester City Football Club

Maelezo ya picha,

Vichai Srivaddhanaprabha

  • Baba wa watoto wanne
  • Billionea na mwanzilishi wa kampuni ya King Power International
  • Anachukua nafasi ya tano kama mtu tajiri zaidi nchini Thailand
  • Aliinunua Leicester City mwaka 2010 kwa pauni milioni 39
  • Chini ya umiliki wake klabu ilishinda Ligi ya Premier mwaka 2016 na kufika robo fainali ya Champions League mwaka mmoja baadaye