Tunafahamu kipi hadi sasa kuhusu mauaji ya watu 11 Marekani

A Swat officer and police officers arrive at the scene of a suspected religiously-motivated attack on a synagogue in Pittsburgh, Pennsylvania, 27 October 2018

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Polisi wakiwa nje ya sinagogi

Mwanamume anayeshukiwa kuwaua watu 11 kwenye sinagogi huko Pittsburgh, Marekani, amefunguliwa mashtaka ya mauaji katika kile kinaaminiwa kuwa shambulizi baya zaidi linalohusu chuki dhidi ya wayahudi kwenye historia ya Marekani.

Robert Bowers, 46, analaumiwa kufyatua risasi kwenye sinagogi ya Tree of Life wakati wa ibada ya Sabato.

Anakabiliwa na mashataka 29 yakiwemo ya matumizi ya bunduki kuua.

Rais Donald Trump amelaani shambulizi hilo na kulitaja kuwa kitendo kiovu cha mauaji.

Watu sita wakiwemo polisi wanne walijeruhiwa kwenye shambulizi hilo la siku ya Jumamosi.

Chanzo cha picha, AFP/Getty Images

Maelezo ya picha,

Mshukiwa wa mauaji Robert Bowers

Mshambuliaji naye alijeruhiwa wakati wa ufyatuaji huo.

Rais Trump alisema atazuru huko Pittsburgh hivi karibuni. Aliamrisha bendera zote nchini Marekani kupeperushwa nusu mlingoti hadi Oktoba 31.

Kipi kilitokea?

Jumamosi asubuhi waumini walikusanyika kwenye sinagogi kwa shughuli ya kuwapa watoto majina wakati wa Sabato.

Squirrel Hill ni kati ya maeneo yaliyo na watu wengi wa jamii ya wayahudi huko Pennsylvania na huu ulikuwa ni wakati wa shughuli nyingi zaidi kwenye sinagogi hiyo.

Polisi wanasema walipata simu mwendo ya saa 9.54 asubuhi na kutuma maafisa baada ya dakika moja.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kikosi cha SWAT kilitumwa eneo hilo

Kulingana na ripoti mwanamume mzungu aliingia jengo la sinagogi wakati wa ibada ya asubuhi akiwa amejihami kwa jumla ya bunduki nne.

Mtu huyo alikuwa tayari ameuwa watu 11 na alipokuwa akiondoka sinagogi baada ya dakika 20, akakumbana na kikosi cha polisi cha Swat na kufyatuliana risasi.

Mshambuliaji kisha akarudi ndani ya jengo kujaribu kujificha kutoka kwa polisi.

Alijisalimisha baada ya ufyatuaji wa risasi na sasa anatibiwa hospitalini kwa majeraha kadhaa ya risasi.

Chanzo cha picha, Google

Maelezo ya picha,

Sinagogi ya Tree of Life huko Pittsburgh