Mwanafunzi aliyejilipia karo kwa kumtengenezea Lil Wayne mkufu

Joy BC making the necklace in the workshop

Chanzo cha picha, Joy BC

Maelezo ya picha,

Joy BC akitengeneza mkufu

Mwanafunzi wa sanaa ambaye alitengeneza mkufu wa dhahabu kwa mwanamuziki Lil Wayne amesema mauzo yake yalimsaidia kulipa karo yake ya chuo kikuu.

Joy Bonfield-Colombara, 29, kutoka kusini mashariki mwa London, alisema alikuwa na wakati mgumu kulipa karo ya pauni 9,500 kwa mwaka kwenye chuo cha sanaa cha Royal College of Art.

Lakini wakati akitathmini kuacha masomo, alipata ujumbe wa barua pepa kutoka kwa rafiki wa rapa huyo raia wa Marekani, ambaye alikuwa anataka kumnunulia mkufu huo kama zawadi ya siku ya kuzaliwa.

Mkufu huo wa dhahabu una uso wa Lil Wayne.

Albamu ya hivi majuzi ya Lil Wayne ya Tha Carter V, inayowashirikisha wanamuziki Snoop Dogg, Nicki Minaj, Travis Scott na Kendrick Lamar, ilishika namba tano katika jadwali la muziki nchini Uingereza mwezi huu.

Chanzo cha picha, Joy BC

Maelezo ya picha,

Joy BC aliserma rafiki wa Lil Wayen alimuambia aliupemda sana

Bi Bonfield-Colombara, ambaye pia anafahamika kama Joy BC, alishangaa sana wakati alijulishwa kiwango cha pesa ambacho angelipwa alichosema ni maelfu kadhaa wa pauni.

Alisema alikuwa na muda wa wiki mbili hadi tatu kumaliza kazi hiyo kabla ya siku ya kuzaliwa ya miaka 36 ya Lil Wayne.

"Nilimpigia mpenzi wangu simu na kumuambia nimeshangazwa sana," alisema.

"Nilichonga kila kitu kwa mikono yangu, hunichukua muda mrefu sana. Mkufu mmoja nilimtengenezea mtu ulinichukua miezi 9.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Lil Wayne, akiwa amevaa mkufu huo mapema mwezi huu huko New Orleans

"Mpenzi wangu aliniambia nisitengeneze sawa na wa Ronaldo," alisema. Akimaanisa sanamu ya Ronaldo iliyokosolewa sana kwenye mitandao ya kijamii.

Bi Bonfield-Colombara, ambaye aliwai kusomea Glasgow School of Art, alisema amekuwa akituma maombi ya msaada kwa masomo yake.

"Mama yangu alichukua mkopo wa benki na mimi nikapata mkono wa serikali, kwa mahitaji yangu nilitegemea karo yangu."

"Nilihitajika kutafuta karibu pauni 10,000. Nilitumia mtandao wa GoFundMe nikafanikiwa kuchangisha pauni 1,500, Kisha nikapata barua pepe hii."

"Licha ya pesa nilizopata kwa mkufu huu haziwezi kulipa karo yangu yote, zinalipa sehemu kubwa."