Wasanii nchini Tanzania watakiwa kufanya kazi zao kufuatana na maadili na desturi za taifa

Wasanii nchini Tanzania watakiwa kufanya kazi zao kufuatana na maadili na desturi za taifa

Wasanii nchini Tanzania wametakiwa kuishi na kufanya kazi zao kufuatana na maadili na desturi za taifa hilo.

Naibu waziri wa Sanaa utamaduni na michezo nchini Tanzania Juliana Shoza akilifunga tamasha la 37 la kimataifa la Sanaa la chuo cha Sanaa Bagamoyo, amesema kumekuwa na watu wengi wanao tumia mwavuli wa Sanaa kufanya mambo yao na ndio maana kumekuwa na mmomonyoko mkubwa wa maadili.

Picha: Eagan Salla