Uchaguzi Brazil: Jair Bolsonaro ashinda uchaguzi wa urais wa nchi hiyo

l Jair Bolsonaro

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Rais Mteule wa Brazil Jair Bolsonaro

Mgombea wa urais wa mrengo wa kulia nchini Brazil Jair Bolsonaro ameshinda uchaguzi wa Urais wa nchi hiyo kwa asilimia 55 katika duru ya pili dhidi ya mgombea mweza Fernando Haddad wa mrengo wa kushoto na chama cha wafanyakazi.

Mkuu huyo wa jeshi wa zamani kampeni zake zilijikita kuimarisha ulinzi.

Mgombea wa urais wa mrengo wa kulia Nchini Brazil ameshinda kwa kishindo uchaguzi wa urais.

Amepata asilimia 55 dhidi ya 45 za mpinzani wake mkuu Fernando Haddad kutoka chama cha mrengo wa kushoto cha wafanyakazi.

Bolsonaro alipigia kampeni juu ya ahadi ya kumaliza rushwa na kupunguza kasi ya Uhalifu.

Alisisita juu ya kubadili sheria za umiliki wa Bunduki na ubebaji wake.

Wakati wa kipindi cha Kampeni kila upande wa mgombea walisema kuwa kila upande ukishinda unaweza kuingamiza Brazil.

Ukaribu wa Bolsonaro na baadhi ya wanajeshi, mgombea mweza alidai kuwa akishinda basi ni hatari kwa demokrasia ya Brazil.

Katika hotuba yake baada ya kutangazwa mshindi alisema kuwa atalinda katiba na demokrasia ya Brazil.

''hii sio ahadi kwa chama ama neno kwa mtu yoyote, bali ni ahadi mbele ya mungu'' anasema Bolsonaro.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Wafuasi wa Bolsonaro

Sera ya uchumu ya rais huyu Mteule ni kupunguza serikali kuingilia uchumi.

Alitoa maoni pia juu ya Brazil kujitoa katika makubaliono ya Paris ya mwaka 2015 ya mabadiliko ya tabia nchi.

Bolsonaro amesema kuwa atasafisha wanasiasa wala rushwa wote, alitoa ahadi hiyo katika moja ya kampeni zake , jambo ambalo linazungumzwa na wananchi Wengi waliochoshwa na visa vya Rushwa kutoka kwa wanasiasa wakongwe ambao wamewahi hadi kufungwa kwa ajili ya Rushwa.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Mgombea mweza Fernando Haddad alipata asilimia 45

Mgombea mwenza kutoka chama cha wafanyakazi Fernando Haddad amejitahidi kujiweka mbali na sakata za rushwa ambazo zimekua zikiandama chama chake kwa muda mrefu.

Haddad amelijiunga na chama hicho takribani mwezi mmoja kabla ya duru ya kwanza ya uchaguzi baada ya aliyekuwa mgombea na rais wa zamani Lula Da silva kusimishwa kugombea.

Lula anatumikia kifungo cha miezi 12 kutokana na Rushwa.

Bolsonaro ataapishwa tarehe moja mwezi wa kwanza mwaka 2019 na kuchukua nafasi ya Rais Michel Temer ambaye anaondoka madarakani akiwa na uungwaji mkono wa chini wa asilimia 2.