Mwili wa mwandishi wa DW Isaac Gamba wawasili Tanzania kwa mazishi

Mwili wa mwandishi wa DW Isaac Gamba wawasili Tanzania kwa mazishi

Mwili wa mwandishi wa habari Isaac Gamba aliyekuwa akifanya kazi na Idhaa ya Kiswahili ya DW nchini Ujerumani umewasili Alfajiri ya hii leo ukitokea Ujerumani ambako mauti yalimkuta.

Mwili wa Gamba umepokelewa na wanahabari wenzake ambao walijitokeza toka mapema majira ya saa saba za usiku kumlaki mpendwa wao ambaye baadhi waliwahi kufanya naye kazi akiwemo mzee Ahmed Kipozi mwandishi wa habari mkongwe nchini Tanzania

Katika msafara ulio uliwasili na Mwili kutokea Ujerumani alikuwepo pia Mkuu wa Idhaa ya Kiswahilli ya DW Andrea Schmidt ambaye amesema pengo la Isack haliwezi kuzibika kwani alikuwa mchapa kazi, mbunifu mcheshi na asiyekata tamaa

‘’Nakumbuka wakati mmoja kabla ya kuja Tanzania alisema naenda nyumbani kula bata, akiwa na maana kwamba furahia maisha," amesema Bi Schmidt.

Video: Eagan Salla, BBC