Nyota wa Afrika wamkumbuka mmiliki wa Leicester City Vichai Srivaddhanaprabha

Riyad Mahrez (left) with the late Leicester City owner Vichai Srivaddhanaprabha and the Premier League trophy

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Riyad Mahrez (kushoto) ni mmoja ya walitoa heshima zao kwa Vichai Srivaddhanaprabha

Wachezaji wa Kiafrika waliiowahi kuichezea Leicester City wametoa heshima zao na kuelezea hisia zao kufuatia taarifa za kufariki kwa mmiliki wa lklabu hiyo Vichai Srivaddhanaprabha katika ajali ya ndege Jumamosi.

Bilionea huyo wa Thailand nimojawapo ya watu watano waliofariki wakati helikopta ilipoanguka muda mfupi baada ya kuondoka kutoka uwanja wa King Power stadium.

Leicester City ina kundi kubwa la wachezaji kutoka Afrika katika ligi kuu ya England ambao wamekuwa wakitoa heshima zao na rambarambi katika mitandao ya kijamii.

"Mungu aipokee roho yako. Pumzika salama bosi," Mshambuliaji wa Nigeria Kelechi Iheanacho ameandika kwenye Twitter.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Wilfred Ndidi: "Ulikuwa mkarimu sana na mwenye kusaidia watu. Asante kwa yote ulioifanyia klabu..''

Mwenzake Wilfred Ndidi amesema: "Ulikuwa mkarimu sana na mwenye kusaidia watu. Asante kwa yote ulioifanyia klabu, kwa kuihimiza timu daima na kuja kunitazama nilipocheza katika kombe la dunia. Pumzika salama bosi."

Kauli ya Ndidi inajiri muda mfupi baada ya kuifungia Leicester bao 1-1 dhidi ya Westham katika mechi ambayo Srivaddhanaprabha aliitazama Jumamosi.

Winga wa Algeria Rachid Ghezzal aliandika katika ukurasa wake wa Instagram: "Pumzika kwa amani Bosi. Maombi yangu yazifikie familia kwa ajali hii. Ninawaombea nguvu na uvumilivu jamii nzima ya Leicester katika wakati huu mgumu. Asante bosi."

Mlinzi wa Tunisia, Yohan Benalouane ni mwingine aliyeguswa kwa taarifa hizi: "Mpendwa Bwana mwenyekiti. Ni vigumu mno kupata maneno sahihi, kutokana na kwamba nimehuzunishwa sana. Wewe ndiye baba wa klabu yetu, familia yetu, umetusaidia sote kuzifikia ndoto zetu."

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Daniel Amartey aliyepata jeraha kubwa katika mechi ya Jumamosi, alitoa pole zake akiwa kitandani hospitalini

Mchezaji wa kiungo cha kati wa Mali Fousseni Diabate alituma rambi rambi zako "Asante kwa kunipa fursa ya kuwa katika kiwango kikubwa zaidi. Asante kwa tabasamu na ukarimu wako. Asante kwa kuniamini. Asante na kwaheri"

Beki wa Ghana Daniel Amartey, aliyepata jeraha kubwa katika mechi ya Jumamosi, alitoa pole zake akiwa kitandani hospitalini.

"Asanteni nyote kwa maneno yenu ya kunipa moyo lakini nimehuzunika sana kutoka kwenye operesheni na kusikia habari kuhusu mwenyekiti wetu aliye na umuhimu mkubwa kwa klabu yetu na kwa wachezaji wetu wote. Maombi yangu yaiendee familia yako Boss," Amartey aliandika katika ukurasa wake wa Instagram.

Mshambuliaji wa Algeria Riyad Mahrez, aliyejiunga hivi karibuni na Manchester City baada ya kipindi chenye ufanisi cha miaka minne na Leicester City, ikijumuisha ushindi wataji la ligi kuu England mnamo 2016 pia alitoa heshima zake.

"Mojawapo ya watu wazuri niliowahi kukutana nao. Sitowahi kukusahahu kamwe. Pumzika kwa amani Vichai."

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Ahmed Musa mchezaji wa kiungo cha mbele wa Nigeria

Kwa upande wake Mchezaji wa kiung cha mbele wa Nigeria Ahmed Musa, aliyeondoka kwenye klabu hiyo hivi karibuni kujiunga na timu ya Saudi Arabia Al-Nassr, ametuma ujumbe wa moyoni kufuatia ajali hiyo.

"Mtu aliye na umuhimu maalum, hatosahauliwa, wakati wenye furaha sitawahi kuusahau. Kumbukumbu nzuri daima zitakuwepo, kamwe sitokusahau," alisema.

"Kifo kamwe hakiwezi kumuondoa mtu mzuri, kutoka mioyo ya watu aliowapa matumaini. Kumbukumbu itasalia na itaendelea kuwepo katika vizazi vijavyo. Alikuwa mtu mzuri na baba kwa wengi. Roho yake na ipumzike pema penye wema."

Srivaddhanapraba, aliyeinunua klabu hiyo mnamo 2010, alitumia helikopta mara kwa mara kwenda kutazama mechi za Leicester katika uwanja huo wa King Power Stadium na uwanja wa mazoezi wa timu hiyo.

Klabu hiyo imaktiaza mechi zake za kati kati ya wiki kwa timu ya kwanza na ya vijana katika kutoa heshima kwake.