Kunusurika kifo baada ya ajali ya ndege: Je hilo ni tukio lisilokua la kawaida?

Chanzo cha picha, EPA/Handout
Ndege iliyoanguka katika jimbo la Durango nchini Mexico iliripotiwa kupoteza injini zote mbili
Taarifa ya kunusurika kifo kwa abiria wote 103 waliyokuwa ndani ya ndege iliyoanguka katika jimbo la Durango nchini Mexico siku ya Jumanne imetajwa kuwa miujiza.
Hii inatokana na picha za kuogofya zilizokuwa zikionyesha jinsi mabaki ya ndege hiyo uilivyokuwa ikiteketea katika eneo la tukio.
Karibu kila mmoja aliyekuwa ndani ya ndege hiyo alijeruhiwa lakini wote walinusurika kifo.
Je hilo ni tukio lisilokua la kawaida? Cha kushangaza ni kuwa huenda, hilo si jambo geni kama unavyodhania.
Kuna uwezekano gani wa kuponea ajali ya ndege?
Ukweli ni kwamba hakuna jibu la moja kwa moja kwa sawali hili- Sawa na jinsi hatuwezi kuuliza kuna nafasi gani ya kuponea ajali ya gari.
Hii ni kwa sababu inategemea mazingira yaliyochangia ajali yenyewe.
Lakini baada ya Bodi ya kitaifa ya usafiri salama nchini Marekani kufanya uchunguzi wa kitaifa wa ajali za ndege kuanzia mwaka 1983-1999, ilibaini kuwa zaidi ya 95% ya waliyo kuwa ndani ya ndege hizowaliponea kifo ikiwa i pamoja na 55% ya watu waliojeruhiwa vibaya zaidi.
Nafasi ya kunusurika kifo hutegemea kuwepo kwa moto wakati wa ajali, umbali wa ndege angani na sehemu ilipo ndege yenyewe.
Kwa mujibu wa utafiti wa mwaka 1996,Baraza la Ulaya linaloshughulikia usalama wa usafiri wa angani linakadiria kuwa 90% ya ajali za ndege hutokana na hitilafu za kiufundi.

Chanzo cha picha, Getty Images
Mwaka 2009, abiria 150 walinusurika kuzama baada ya ndege yao kuangua ndani ya mto Hudson mjini New York
Miongo miwili baada ya tafiti hizo mbili kufanywa , usalama wa safari za ndege umeimarishwa huku ajali zinazosababisha vifo zikipungua kwa kiwango cha haja.
Usafiri wa ndege ni salama kuliko usafiri mwingine wowote lakini hofu ya kupata ajali bado ni mtihani mkubwa kwa wasafiri kote duniani.
Hii ni kwa sababu tunaona taarifa za kuogopesha za ajali ya ndege au sinsi zinavyoigizwa Hollywood.
Nini hubainisha kama mtu anaweza kunusurika ajali ya ndege?
Tom Farrier, Mkurugenzai wa zamani wa chama cha Usafiri wa angani, ameelezea katika tovuti yake ya Quora kwamba kuna mazingira matatu ambayo inaweza kuwanusuru watu kutokana na ajali ya ndege.
- Hali ya hewa watakayokumbana nayo watu waliyomo ndani ya ndege wakati wa ajali( je wanaweza kuihimili?)
- Vitu vinavyowazunguka abiria baada ya kupata ajali -kwa mfano ndege kutolipuka na kushika moto
- Kama mazingira baada ya ajali ni hatarishi kwa abiria aau waokoaji
Katika ajali ya ndege ya Mexico, iliyoanguka muda mfupi baada ya kupaa, watu wengi walinusurika kwa sababu walifanikiwa kutoka ndani ya mabaki ya ndege kabla iwake moto.

Chanzo cha picha, Getty Images
Mwanamume aliyekatwa mguu baada ya kunusurika ajali ya ndege
Alipoulizwa iwap[o ni ajali gani mbaya zaidi kati ya ndege kuanguka ardhini na majini, mtaalamu wa masuala ya ndege Adrian Gjertsen, anasema hali zote mbili hutegemea uwepo wa karibu wa huduma za uokozi.
"Kwa mfano wakati wa ajali ya mto Hudson, huduma ya uokozi ilikuwa karibu.
Aliambia BBC kuwa ''Ukijipata kati kati ya bahari changamoto kubwa itakua jinsi ya kufika salam nchi kavu.''
Unaweza vipi kuimarisha nafasi ya kunusurika ajali ya ndege?
Zingatia ushauri wa usalama wako ukiwa safarini.
Hakikisha unafunga mkanda wa usalama, usivalie nguo zinazo eneza moto haraka na pia ni vyema kunakili mpangilio wa viti endapo taa zitazimika.
Watu pia wanajadili ikiwa ni salama kuakaa chini ndege ikihusika katika ajali.
Baadhi ya tafiti zinaashiria kuwa ni salama zaidi abiria kukaa badala ya kutembea ndani ya ndege.
Bwana Gjertsen anasema sio rahisi hivyo, na kwamba yote inategemea ndege imekumbwa na hali gani wakati wa ajali.
"Moja ya tatizi kubwa ni kua baadhi ya abiria hung'ang'ania kushuka na mizigo yao hali ambayo inalemaza juhudi za uokozi na usalama wa watu wengine pia