WWF: Ulaji nyama kwa binadamu ndio chanzo kikuu cha kupungua kwa wanyama pori

Man eating chicken

Ulaji wa nyama kwa wingi umesababisha idadi kubwa ya wanyama pori duniani kupungua katika miaka ya hivi karibuni, watafiti kutoka shirika la kuhifadhi wanyama pori WWF waeleza.

Ripoti iliyotolewa hivi karibuni inasema takribani asilimia 60 ya wanyama wametoweka kati ya mwaka 1970 na 2014.

"Dunia inapoteza viumbe hai hawa kwa wingi wakati wanyama hao wanapouliwa ,"imeeleza ripoti hiyo.

Ripoti hiyo imewataka watunga sera kuja na mikakati mipya ya maendeleo endelevu.

Ripoti hii ambayo inatolewa kila baada ya miaka miwili ikiwa na lengo la kuangalia maisha ya wanyama pori.

Toleo la mwaka 2018 linaleza kuwa robo ya eneo ya dunia liko huru na shughuli za binadamu na sehemu hiyo itaathirika mara kumi ifikapo mwaka 2050.

Mabadiliko hayo yanatokana na ongezeko la utengenezwaji wa chakula na ongezeko la mahitaji ya nishati, ardhi na maji.

Ingawa upoteaji wa misitu umechelewesha upandaji miti katika baadhi ya maeneo katika miongo ya hivi karibuni, upotevu huo umeongezeka zaidi katika misitu ya kitropiki ambayo iinajumuisha viumbe na mimea mbalimbali.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

African elephant habitat has halved since the 1970s

Inadaiwa kuwa Amerika ya Kusini na Kati wanaathirika zaidi na kutoweka kwa viumbe hao kwa asilimia 89 ukilinganisha na mwaka 1970.

Viumbe wa majini nao wako katika hatari kubwa zaidi , ripoti hiyo imeeleza.

Ongezeko la plastiki limeathiri sehemu kubwa ya bahari duniani ikiwa ni pamoja na sehemu ya bahari ya Pasifiki.

Viumbe hai wa majini katika maziwa, mito na mikondo mingine ya maji wamepungua asilimia 83 tangu mwaka 1970, kwa mujibu wa ripoti.

WWF imeitaka dunia kuwa na makubaliano ambayo yanafanana na makubaliano ya Paris 2015 katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kupunguza gesi ukaa.

Viongozi au watoa maamuzi katika ngazi zote wanapaswa kufanya maamuzi sahihi kisiasa na kiuchumi ili kufikia malengo ya kutunza utu na mazingira ya dunia kwa namna nzuri.

Hata hivyo utafiti huo umekosolewa na moja ya mhifadhi mmoja ambaye aliiambia BBC kuwa mwaka 2016, Amerika kusini na kati walipoteza idadi ya wanyama wenye uti wa mgongo kwa asilimia 89 ukilinganisha na mwaka 1970.