Uchaguzi Marekani 2018: Je Trump anastahili kuwa na wasiwasi uchaguzi wa katikati ya muhula?

Donald Trump

Donald Trump hatakuwa kwenye karatasi za kura wakati raia Marekani watapiga kura Jumanne Novemba 6, lakini uchaguzi huu utabaini mustakabali wa urais wake.

Wapiga kura watakuwa wanawachagua maseneta 35, Magavana 36 wa majimbo na wabunge wote 435 katika bunge la wawakilishi, pamoja na maafisa wengine kadhaa wa serikali za majimbo.

Uchaguzi huu wa kati kati ya muhula ni muhimu iwapo wanachama wa chama cha Democratic watafanikiwa kulidhibiti bunge au seneti kutoka kwa wanachama wa Republican.

Hii ni kwa sababu wanaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa nguvu za anachoweza kufanya rais Trump katika miaka miwili ya mwisho wa muhula wake.

Wachambuzi wanatabiri kwamba udhibiti wa viti kadhaa bungeni unaweza kubadilika na vingi kwa sasa vinashikiliwa na wanachama wa Republican.

Wanachama wa Republican wapo katika nafasi nzuri kwenye ushindani katika Seneti, licha ya kwamba ni viti 9 tu vyao vinavyowaniwa, huku wanachama wa Democrats wakivitetea viti 24 na viti vya wabunge wawili wa kujitegemea wanopiga kura nao pia vinawaniwa.

Ni kura ya maoni kwa Trump

Uchaguzi wa nusu muhula au kati kati ya muhula kwa mara nyingi hutazamwa kama kura ya maoni kwa rais na mara nyingi huwa sio habari nzuri kwa chama kinachoidhibiti ikulu ya White House.

Kati ya uchaguzi 21 wa nusu muhula, uliowahi kuandaliwa tangu 1934, chama cha rais kimepata faida bungeni mara tatu na katika Seneti mara tano.

Viwango vya kumridhia rais ni kiashiria kizuri cha namna ambavyo matokeo huenda yakawa kwa chama chake na ki historia kwa Trump viwango vimekuwa vya chini, hugusia kiasi cha 40%.

Kwa kumithilisha, viwango kwa rais Obama vilikuwa 45% kabla ya uchaguzi wa nusu muhula 2010 ambapo wanachama wa Democrats walishuhudiwa hasara kubwa katika historia ya Marekani.

Huku Republicans wakiyadhibiti mabunge yote mawili, swali ni iwapo Democrats watashinda viti vya kutosha kudhibiti upya uongozi bungeni.

Matokeo kama hayo yatakuwa na athari kubwa na za mara moja kwa uwezo wa rais kuendeleza ajenda yake kisiasa na wanachama wa Democratic watasimamia utawala wake.

Je mambo yako vipi kwa sasa uhalisia?

Hivi ndivyo vipimo vinavyoweza kutudokezea.

1. Umaarufu wa rais

Uchaguzi wa nusu muhula huonekana kama kura ya moani kwa rais.

Wakati marais wanapoteza umaarufu, wapiga kura hutoa hasira zao kwa chama cha kiongozi huyo bungeni.

Iwapo kiongozi mkuu anavutia umati basi chama chake hupata faida, au angalau kinakwepa adhabu.

Kwa kutazama kura ya kutafuta maoni ya Gallup katika miaka 60 iliyopita, inadhihirisha hili.

Kila wakati kiongozi anapokabiliwa na sifa mbaya katika mwezi kabla ya kura ya nusu muhula - Ronald Reagan mnamo 1982, Bill Clinton mamo 1994, George Bush mnamo 2006 na Barack Obama mnamo 2010 na 2014 - humaanisha muanga umezimika kwa chama kiongozi huyo wapiga kura wanapokwenda debeni Novemba.

Mtazamo wa 2018:

Viwango vya kumridhia Donald Trump vimeimarika, licha ya panda shuka katika mwaka wake wa kwanza na nusu madarakani. Haikuwa rahisi kwake baada ya kuchaguliwa, kwa hivyo hakujakuwana mabadiliko makubwa.

Mwishoni mwa Agosti, rais alikuwa na umaarufu wa 40%. Baada ya kudidimia kati kati ya mwezi, mwishoni mwa Septemba viwango vilikwea hadi 42%.

Mkondo unaelekea vizuri kwa wanachama wa Republicans, lakini itabidi ukwee katika viwango ambavyo hakijawahi kufikia kuondokana na hatari iliopo katika uchaguzi huu wa nusu muhula.

2. Kura ya kutafuta maoni kabla ya uchaguzi

Hii inafanyika kwa kuwauliza watu je ni mgombea wa chama gani watamuunga mkono katika uchaguzi.

Kuna wagombea 435 katika bunge la wawakilishi katika kila uchaguzi wa nusu muhula, inamaanisha kuwa wagombea 870 kutoka vyama viwili vikuu pamoja na wagombea kadhaa wa kujitegemea walio na umaarufu na wanasiasa wa chama cha tatu.

Kila uchaguzi ni wa aina yake, kila eneo lina vivutio vyake, na kila wilaya ina utambulisho wake wa kieeno kama vile alama za vidole.

Kwa hivyo haitokuwa na maana kusema kwamba matokeo jumla ya uchaguzi wote utategemea kura ya maoni ya kuwauliza wapiga kura ni mgombea gani kati ya Democrat na Republican wanaempendelea.

Swali linalotumika katika uchaguzi wa muigo hatahivyo, limedhihirika kuwa kibashiria sahihi cha uwezekano wa matokeo ya uchaguzi wa nusu muhula kwa vyama viwili vikuu.

Mtazamo 2018:

Uongozi wa Democrat katik kura ya muigo imebadilika katika mwaka uliopita.

Mwishoni mwa msimu wa machipuko ilipungua na ikaonekana ni kama Republicans wameimarika tayari kwa kura ya Novemba. Kufikia Septemba kati hatahivyo, uongozi wa Democratic uliimarika mara dufu.

Mkondo umebailika kidogo - ambalo huenda ikaani ishara kuwa wapiga kura wanashinikizwa na uchaguzi ujao.

Haijulikani iwapo hilo litadumu. Lakini kwa namna hali ilivyo sasa, takwimu ni nzuri, lakini sio nzuri vile kwa Democrats.


3. Uchumi

Donald Trump na wanachama wenzake wa Republican wanashinikiza takwimu nzuri za kiuchumi kama kigezo kcha kwanini wanastahili kuendele kushikilia udhibiti kwa miaka miwili mingine Washington.

Kihistoria, hatahivyo, kukua kwa uchumi sio hakikisho la ufanisi wa chama cha rais.

Mnamo 1994, wakati chama tawala cha Democrats kiliposhinda bungeni Congress, uchumi ulipanuka kwa zaidi ya 4%, licha ya kwamba viwango vya ukosefu wa ajira vilikuwa juu kuliko kiwango cha sasa 5.8%.

Katika miaka mingine 2006 na 2014, uchumi haukuwa mbaya vile.

Uchumi unaozorota kwa upande mwingine huenda ikawa ni hukumu ya kifo kwa chama kilichopo madarakani kwenye matokeo ya uchaguzi wa nusu muhula.

Mtazamo 2018:

Kwa takwimu za sasa za robo ya mwaka zikiwa 4.2% na viwango vya ukosefu wa ajira vikiwa chini kwa 49 takiwmu za kiuchumi kwa sasa angalau- hazina shaka ni nzuri.

Trump ameushinikiza uchumi kwa kila namna na kwa hakika haitoathiri nafasi ya chama cha Republican Novemba. Lakini Je Trump atafanikiwa kuvunja mkonodo uliopoo kihistoria na kugeuza takiwmu hizo nzuri kwa manufaa ya utawala wake?

4. Kufadhili Kampeni

Pesa ndio kila kitu katika ulimwengu wa siasa.

Fedha zinazomiminika kwa wagombea, vyama vya kisiasa na makundi ya kujitegemea ni ishara ya nguvu katika uchaguzi kwa kutangaza biashara, mipango na jitihada za kutafuta kura.

hakuna anayependa kuirusha kaata yake kwa mshindwa, na iwapo tasiwra sio nzuri , matajiri na wanaharakati huenda wakasita kufungua mifuko kuziunga mkono kampeni za vyama.

Chama kilichopo madarakani kwa mara nyingi kina faida, na hilo lina ukweli katika uwezo wa kukusanya fedha.

Kutoa fedha kwa wanasiasa ambao tayari wana udhibiti ina maana hususan katika masuala ya maslahi ya kibiashara na kwa watu wanaotaka kuwana uwezo wa kushawishi sera za seriali.

Lakini kutoa fedha kwa wapinzani? Hilo linataka imani kubwa, azma na hisia ya kutaka kubadili utajiri wa kisiasa.

Kuna suala moja katika ufadhili wa kampeni ambalo linafuatilia kwa karibu katika uchaguzi kweny amiaka 25 iliyopita, kipindi ambacho jukumu la fedha katika kampeni za kisiasa liliongezeka.

Mtazamo 2018:

Wagombea wa Democratic katika bunge la wawakilishi wanaendelea kushinikiza faida yao ndogo kwa michango ya kibinafsi. Kufikia 4 Octoba, wamekusanya $430m dhidi ya $230m pekee kwa Republican.

Ari ya chama cha Democratic inageuka kuwa na manufaa kwa mifuko ya fedha - licha ya kwamba utamaduni wa kutoa huenda haumaanishi kwamba rasilmali za kifedha zinasambazwa kwa namna inayofaa.

Kuna habari nzuri kwa wahafidhina hatahivyo. Wagombea wa Republican wanaendelea vizuri katika kukusanya michango kutoka kamati za kisiasa na tofuati na Democrats - chama cha Republican chenyewe kina maelfu ya mamilioni ya dola kutumia katika vinyang'anyiro vikuu kote Marekani.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii