Maisha yako yanaweza kupungua kwa miaka minne ukiwa na uzani wa juu au chini zaidi

Feet on scales

Chanzo cha picha, Getty Images

Kuwa na uzani wa juu au wa chini zaidi inaweza kuchangia maisha yako kuwa mafupi kwa miaka minne kwa mujibu wa jarida la Lancet.

Ripoti moja ambayo ni kubwa zaidi ya aina yake iliwahusisha karibu watu milioni 2 ambao walisajiliwa na madaktari nchini Uingereza.

Watafiti waligundua kuwa kuanzia umri wa miaka 40, watu walio na kiwango chenye afya ya kile kinafahamika kama BMI wako kwenye hatari ya juu ya kufa kutokana na magonjwa.

Lakini watu walio na BMI isiyo ya afya nzuri wako kwenye hatari kubwa ya kuwa na maisha mafupi.

BMI hupatikana na kugawa uzani wa mtu na kimo chake. Mtu mwenye afya huwa na BMI kati ya 18.5 na 25.

Madaktari wengi wanasema kuwa ndiyo njia nzuri zaidi ya kufahamu ikiwa mtu ana uzani wa juu na kuwa pia ndiyo njia ya kupima.

Utafiti huo uliochapishwa kwenye jarida la Lancet ulionyesha kuwa miaka ya kuishi wanaume na wanawake walio na uzani wa juu ilipungua kwa miaka 4.2 na 3.5 mtawalia.

Tofauti ya uzani kwa wanaume na wanawake ni miaka 4.3 na 4.5. Lakini baadhi ya wataalamu wamehoji ikiwa BMI ni njia mwafaka ya kupima afya ya mtu.

Hata hivyo Dr Karatina Kos, mhadhiri mkuu wa masuala ya kisukari chuo cha Exeter anaaminia hivyo.

Kwa watu wengine BMI ni kipimo kizuri, aliiambia BBC.