Mahakama Malawi yasitisha ujenzi wa sanamu la Gandhi baada ya wakosoaji kumuita mbaguzi

Mahatma Gandhi pictured on board the SS ‘Rajputana’ in 1931

Chanzo cha picha, Daily Herald Archive/Getty Images

Maelezo ya picha,

Mahatma Gandhi mnamo 1931

Presentational white space

Mahakama moja nchini Malawi imesitisha ujenzi wa sanamu la Mahatma Gandhi baada ya wakosoaji kumshutumu kwa kutumia maneno ya kibaguzi.

" Sisi wenyewe ni watu wesui , na kauli hizo zimechangia chuki dhidi na kutompenda Gandhi," Kundi linalojiita Gandhi Must Fall limesema katika kesi iliowasilisha kotini.

Jaji Michael Tembo ametoa agizo la kuzuiwa ujenzi huo kwa muda.

Ujenzi wa sanamu hilo ni sehemu ya makubaliano ya ujenzi wa jengo na India wenye thamani ya $10m.

Kwa mujibu wa makubaliano hayo, ukumbi wa mikutano uliopewa jina la Gandhi unajengwa Blantyre, mji mkuu kibiashara nchini Malawi.

makamu wa rais nchini India Venkaiah Naidu alitarajiwa kuitembelea nchi hiyo kuidhinisha rasmi jengo na sanamu hilo, vyombo vya habari nchini humo vinaripoti.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Wanafunzi katika chuo kikuu Cape Town walishinikiza kuondolewa kwa sanamu la mfanyabiashara wa kikoloni wa Uingereza Cecil Rhodes

Mahakam kuu imesema shughuli ya ujenzi wa sanamu hilo usitishwe mpaka kesi itakaposikilizwa tena - au mpaka agizo jipya la mahakama litolewe.

Je ni kweli Gandhi alikuwa mbaguzi?

Mahatma Gandhi ametambulishwa kwa namna tofuati kama mwandamanaji kupinga utawala wa ukoloni, kiongozi wa kidini, mkosoaji mwenye itikadi kali ambaye alitumikia hikima badala ya ghasia kupigania masuala tofuati, mwanasiasa mjanja na kadhalika.

lakini je kiongozi huyo mkuu India alikuwa na ubaguzi?

Wahariri wa kitabu kilichogubikwa kwa mzozo kuhusu maisha ya Gandhi na kazi yake nchini Afrika kusini wanaamini hivyo kwa hakika.

Wasomi nchini Afrika kusini Ashwin Desai na Goolam Vahed walikaa miaka 7 wakitathmini maisha magumu ya mwanamume aliyeishi nchini mwao kwa zaidi ya miongo miwili 1893 hadi 1914 na aliyepigania haki za Wahindi huko.

Katika Kitabu cha South African Gandhi: Stretcher-Bearer of Empire, Desai na Vahed wameandika kuwa wakati alipokuwa akiishi Afrika, Gandhi aliendelea kupigania Wahindi "Kando na waafrika na watu wa rangi au maarufu Afrikaans licha ya kwamba kundi hilo lilinyimwa pia haki za kisiasa kwa misngi ya rangi na wangeweza kulalamika kuwa raia wa Jumuiya ya madola".

Wameandika kwamba mipango ya kisiasa ya Gandhi - kupigania kuondoshwa kwa sheria zisizo za haki au uhuru wa kuzunguka au biashara - ulichonga utambulisho wa aina yake kwa wahindi , "uliotegemea yeye kuyashughulikia masuala ya wahindi katika namna ambayo inawatenganisha wahindi na waafrika, huku tabia zake zikiambatana na zile za wazungu katika miaka ya awali".

Gandhi, wahariri hao wameandika, hakuwa na imani na yaliowafika waathirika, na aliamini uongozi wa taifa unastahili kuendelea kudhibtiwa na wazungu, na aliwaita Waafrika, Kaffir, neno alilolitumia kwa sehemu kubwa ya kukaa kwake nchi humo.

Chanzo cha picha, HULTON ARCHIVE

Tatizo lipo wapi na Gandhi?

Gandhi anatazamwa kama shujaa wa uhuru nchini India, lakini barani Afrika, alikoishi kwa zaidi ya miaka 20 anaonekana kuwa tatizo.

zaidi ya raia 3,000 wa Malawi wamesaini nyaraka kupinga ujenzi wa sanamu hilo, wakilalamika kwamba hakufanya jambo lolote la kuifaidi nchi hiyo.

Miaka miwili iliyopita, wahadhiri katika chuo kikuu Ghana pia walitaka sanamu la Gandhi katika makao ya chuo hicho liondolewe, wakieleza kuwa kiongozi huoy ambaye hakutumia ghasia alikuwana ''utambulisho wa ubaguzi''.

Mji huo umenukuu maandishi yake, ambapo amewaeleza Waafrika kuwa "watwana au wazawa wa Afrika" na "kaffir" (tusi lenye ubaguzi dhidi ya Waafrika weusi).

Mnamo 2015, sanamu la Gandhi nchini Afrika kusini liliharibiwana mwanamume aliyelipaka rangi nyeupe.

Gandhi sio kiongozi wa kihistoria ambaye masanamu yake yamezusha malalamiko.

Chanzo cha picha, AFP

Waandamanaji hao walisema sanamu hilo lina "ishara nzito ya uongozi, "na linamtukuza mtu aliyewanyanyasa watu weusi na kuwaibia ardhi wazawa wa eneo hilo".