Wanaume waliopooza mwili wafanikiwa kutembea tena baada ya kupandikizwa kifaa maalum

Sebastian, Gertan and David have all benefited from the work of Dr Courtine
Maelezo ya picha,

Sebastian, Gertan na David wamenufaika na kazi ya Dkt. Courtine

Wanaume watatu waliopooza waliambiwa kuwa watatumia kiti cha magurudumu 'wheelchair' katika maisha yao yote lakini sasa wanaweza kutembea tena na shukrani zinawaendea madaktari kutoka Uswizi.

Kifaa maalum cha umeme kinazungushwa kwenye mgongo ili kusaidia kuonyesha ishara kutoka kwenye ubongo mpaka kwenye miguu.

Na kifaa hicho husaidia neva kutoathiri ukuaji wa uti wa mgongo.

Watafiti wanamatumaini kuwa jambo hili ambalo halikutegemewa litawawezesha baadhi ya watu waliopooza kufanikiwa kuwa huru tena kutembea.

Maelezo ya video,

Kifahamu kifaa kipya kinachowawezesha waliopooza kutembea

BBC ilipata nafasi ya kuhojiana na wagonjwa hao ambao wamefanyiwa jaribio hilo katika kliniki iliyotoa matokeo ambayo yalichapishwa katika jarida la 'Nature'.

Mgonjwa wa kwanza kutibiwa ni raia wa Uswiss David M'zee mwenye umri wa miaka 30 ambaye alikuwa anasumbuliwa na jeraha la mgongo kwa miaka saba baada ya kupata ajali.

'Kujaribu yasiyowezekana'

Daktari alimwambia David kuwa hataweza kutembea tena.

Lakini sasa anaweza kutembea hata zaidi ya nusu maili wakati kifaa hicho cha kupandikiza kikiwa kimewashwa.

David anawashukuru waliotengeneza kifaa hicho cha umeme wajulikanao kama École Polytechnique Fédérale de Lausanne (EPFL).

Kwa sababu sasa ana uwezo wa kutembea mwenyewe pia ingawa ni kwa muda mfupi lakini anaona mabadiliko katika maisha yake.

Maelezo ya picha,

David alimwambia daktari wake kuwa atatembea kabla ya binti yake hajaanza kutembea

"Kwangu mimi hii ina maana kubwa sana.Ninashangaa kwa kile ambacho tumefanikiwa kukifanya.Nafikiria kuwa inabid mtu ujaribu kile kisichowezekana na kukifanya kuwa kinawezekana.

Inaleta raha sana na nnajisikia vizuri kwa kweli" David alisema.

David amekuwa ni mtu mwenye furaha kubwa, ingawa baada ya kupata majeraha alikuwa mtu aliyepitia kipindi kigumu cha huzuni na kukata tamaa.

Alifanya majaribio yote ya kumuwezesha kurejea kuishi maisha yake kama awali lakini ilishindikana, ndio maana alikubali kufanyiwa jaribio hilo na Daktari Grégoire Courtine katika EPFL.

Dkt. Courtine anakumbuka jitihada ambazo David alikuwa nazo za kutaka kufanikiwa.

"Nilikuja na binti yangu, Charlotte,ambaye alikuwa na mwezi mmoja wakati huo.Na tulipokutana na David , David alimwangalia mtoto wangu machoni na kusema 'Nitatembea kabla yako'.

Wakati Charlotte alipoanza kutembea alikuwa na miezi 14, wakati ambao David alikuwa anatembea tayari katika ziwa Geneva.

Akamwambia kuwa "nimekushinda" ,Dr Courtine.

Daktari Courtine alishangazwa na kifaa hicho kinavyofanya kazi zaidi hata namna ambavyo David anavyoweza kutembea.

Kile ambacho hakikutegemewa ni kutengamaa kwa uti wa mgongo.

David alifanyiwa upasuaji na kuwekewa kifaa hicho na mmoja wa wataalamu wa upasuaji wa mishipa, Daktari Jocelyne Bloch kutoka hospitali ya chuo kikuu cha Lausanne.

Yeye pia alimwambia jinsi anavyoshangazwa na uponaji wa David.

David anaweza kutembea sasa mpaka kupanda ngazi nane wakati kifaa hicho kikiwa kimezimwa na hii ni mara ya kwanza kutokea katika jeraha kubwa la mgongo.

Ingawa inaonekana kuwa katika maisha ya uhalisia, Ni vigumu kwa David kutembea katika na kifaa hicho akiwa na kifaa hicho muda wote.

Kuna ishara zinazoonyesha kuwa hapo baadae kifaa hicho kinaweza kumfanya mtu asiwe huru na kutoweza kutumika muda wote.

Utaalamu huo pia ni ghali na hauna uhakika wa kutosha kutumika nje ya maabara kila siku, hivyo haukaribii kwenye tiba.

Hurejesha matumaini

Kwa mujibu wa daktari Mark Bacon, mkuu wa kitengo cha sayansi ya asasi ya watafiti wa mgongo, wanaeleza kwamba kupooza kunaweza kumfanya mtu kushindwa kutibika hata kwa kiwango kidogo.

"Chochote ambacho kiko kwa sasa ,ni jitihada ambazo mgonjwa alizochaguahakuna shaka katika hilo",Daktari Mark alisema.

David ni mgonjwa wa kwanza kati ya watatu ambao wamenufaika na jaribu hilo la kwanza la matibabu.

Wengine waliweza pia kutembea tena, kwa kiwango fulani.

Gertan Oskan mwenye umri wa miaka 35,ambaye ni mhandisi kutoka Netherlands,aligongwa na gari zaidi ya miaka saba iliyopita.

Daktari wake alimwambia kuwa katika siku yake ya kuzaliwa atakuwa amepooza kabisa kwa maisha yake yote lakini sasa anaanza kupata nafuu na kuanza kutembea.

Maelezo ya picha,

Wanaume watatu wamenufaika na machine hiyo mpaka sasa

Sebastian Tobler,mwenye umri wa miaka 48 kutoka nchini Ujerumani alikuwa anapenda kuendesha baiskeli na kutembelea maeneo ya pembezoni kabla hajapata ajali na baiskeli yake.

Lakini sasa hivi amerudia kuendesha baiskeli ambayo anatumia mkono zaidi na sehemu ya miguu yake.

Watafiti wanaamini kuwa mfumo huo utaweza kuwasaidia baadhi ya watu waliopoteza matumaini ya kutembea kuweza kutembea tena.

Kuna mpango wa kuanzishwa kwa majaribio makubwa zaidi barani ulaya na Marekani kwa miaka mitatu.

Kama jaribio hili litafanikiwa, watafiti wana matumaini kuwa mfumo huu utaweza kupatikana katika maeneo mengi.