Uganda inakuwa nchi ya kwanza kukinga kabla ya maambukizi

Ebola vaccine Uganda

Chanzo cha picha, Wales News Service

Maelezo ya picha,

Chanjo hiyo itatolewa kwa wasaidizi wa masuala ya afya

Uganda itakuwa nchi ya kwanza ulimwenguni kutoa chanjo ya ugonjwa wa Ebola kukiwa hakuna mlipuko wa ugonjwa huo.

Wizara ya afya ikiwemo shirika la afya ulimwenguni WHO limeunga mkono hatua hiyo kutokana na sababu ya tishio la kusambaa kwa ugonjwa huo kutoka nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Tishio la kusambaa kwa ugonjwa huo hadi nchi zinazopakana na nchi hiyo ya DRC linazidi kuongezeka hasa upande wa Mashariki ulipo mji wa Beni

Hii ni kutokana na ukosefu wa usalama na hivyo kukwamisha jitihada za kupambana na ugonjwa huo kama ilivyotukia siku za karibuni ulipozuka na kusababisha vifo vya watu 179.

Na kwa naana hiyo Mikoa iliyo jirani na mpaka wa nchi za Burundi, Rwanda na Uganda iko hatarini.

Kutokana na hali hiyo Uganda ndipo ilipoamua kuchukua hatua za makusudi na za awali kukabiliana na ugonjwa huo wa Ebola.

Chanjo hiyo itagawiwa kama kinga ya kuzuia kwa mtu binafsi wakiwemo wafanyakazi wa afya walioko mstari wa mbele vitani, timu za ufuatiliaji na za mazishi.

Mwakilishi kutoka serikali ya Uganda kwa shirika la afya ulimwenguni WHO , Dr. Yonas Woldemariam, ameiambia BBC kwamba kiwango cha zaidi ya chanjo 2000 vimekwisha patikana .

Timu zinazo shughulika na chanjo zimepelekwa upande wa magharibi wa nchi ya Uganda karibu na mpaka baina yake na nchi ya D.R Congo, ili kuanza kazi katika wilaya tano zilizoko hatarini zaidi ..

Ebola vaccine Uganda

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Mipakani ndiko kutakakopewa kipaumbele zaidi

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia chanjo hiyo ilikuwa ikitolewa maalumu kwa watu wote waliowahi kuwa karibu na wagonjwa walio thibitika kuathiriwa na ugonjwa wa Ebola.

Uganda imeendelea kuchukua hatua zingine kama vile uchunguzi wa watu wanaovuka kutoka katika maeneo yenye mkusanyiko mkubwa wa watu karibu na mpaka baina yake na nchi ya DRC tangu mwezi wa August mwaka huu.

Nchi hiyo ya DRC, ina sifa ya kujibu haraka dharura za kiafya.Mnamo mwaka 2000, ilipata maambukizi ya Ebola yaliyo sababisha vifo vya watu zaidi ya mia mbili. Na tangu wakati huo, iliimarisha ufuatiliaji wake na timu za kukabiliana na dharura kwa kutambua mapema viashiria vya kuzuka kwa virusi.