Watumiaji wa bidhaa hizi tano wanasikia kwa mara ya kwanza zina madhara kwa sayari

Diver

Chanzo cha picha, PA

Maelezo ya picha,

Watafiti wanaamini bidhaa za kujikinga na miale ya jua zinaharibu miamba ya matumbawe.

Nchi ya Palau iliyoko magharibi mwa bahari ya Pacific imekuwa ya kwanza kupiga marufuku bidhaa za kujikinga na miale ya jua ili kulinda miamba yake ya matumbawe.

Hata hivyo huenda watumiaji wa bidhaa hiyo wanasikia kwa mara ya kwanza kwamba ina madhara kwa mazingira.

Watafiti wanaamini kemikali 10 zinazotumiwa kutengeneza mafuta ya kujiking na miale ya jua zina sumu ambayo inahatarisha viumbe hai wa majini.

Hizi hapa ni bidhaa zingine tano ambazo hukua na ufahamu zinaathiri mazingira kwa njia moja au nyingine

Dawa za kupanga uzazi

Chanzo cha picha, Getty Images

Wakati vidonge vya uzazi wa mpango vinaweza kusababisha watu wachache wanaoishi katika sayari ya dunia - kupunguza utegemezi uchumi kwenye rasilimali za asili - utafiti wa Kiswidi wa 2016 umebaini ushahidi wa madhara isiyo ya kawaida.

Katika utafiti wake,Lina Nikoleris wa chuo Kikuu cha Lund aligundua kuwa homoni ya ethinyl-estradiol (EE2) - ambayo ni mfano homoni ya oestrogen inayotumiwa kutengeza dawa hiyo zinabadilish mfumo wa jeni ya baadhi ya samaki.

Utafiti huo pia ulibaini kuwa homoni ya EE2 ilifanya samaki kula chakula hasa mabaki yake yanapotupwa baharini.

"Tafiti zilizopita zilionyesha kuwa samaki pia walipata shida kuendeleza kizazi chao," anasema bi Nikoleris.

"Hii inaweza kuangamiza kizazi kizima cha samaki ,hali ambayo itakuwa na madhara kwa mazingira."

Parachichi

Chanzo cha picha, Reuters

Mbali na kuwa tunda hili limetokea kupendwa na watu, inasadikiwa kuwa ina madhara kwa mazingira it is also bad for the environment.

Wanaharakati wa shirika la Water Footprint Network wanaopigania utumizi mzuri wa maji, wanasema inachukua takriban lita 272 kukuza mti mmoja wa tunda la parachchi - kuna hofu huenda upanzi wake ukaathiri mazingira ya eneo linalotumiwa kukuza mmea huo.

Mwaka 2011, uchunguzi uliyofanywa na mamlaka ya maji nchi Chile ulibaini kuwa wamiliki wa mashamba ya aina 65 ya parachichi wakipindisha kiharamu mkondo wa maji ya mito katika mashamba yaolikuwa

Hali hiyo ililaumiwa kwa kusababisha ukame, uliyosababisha wanavijiji kuchagua kati ya kunywa maji au kufulia.

Mananasi

Chanzo cha picha, Getty Images

Costa Rica, ni moja ya wakuzaji wakubwa wa mananasi.

Taifa hilo limekata maelfu ya hekari ya misitu ili kupanda mananasi.

Wahifadhi wa mazingira wanasema ukataji huo mbaya wa misitu utakua na athari kwa mazingira nchini humo

Pia wanasema uzalishaji mkubwa wa mazao aina moja tu - huhitaji kiasi kikubwa cha dawa za wadudu, ambazo zinaweza kuwa na madhara kwa mazingira.

Shampoo

Chanzo cha picha, PA

Mafuta ya nazi ni moja kati ya mafuta mazuri duniani- Lakini utumizi wake mkubwa umechangia uharibifu wa misitu.

Katika ripoti yake ya mwaka 2018 kundi la wahifadhi wa mazingira linalo julikana kama WWF lilionya kuwa uharibifu wa misitu ya kitropiki na kukuza minazi au mitende ambayo inasadikiwa kutoa "kiasi kikubwa cha hewa chafu ya kaboni, huchochea mabadiliko ya hali ya hewa, na kuharibu makazi ya viumbe hai kadhaa ardhini".

Huenda unaufahamu kuwa mafuta ya nazi hutumiwa kutengeneza bidha kadhaa zinazotumiwa na watu kama chokoleti, siagi, mkate na biskuti biscuits, ni watu wachache wanajua mafuta hayo hutmiwa sana kutengeza nyingi bidhaa za nyumbani.

Katika shampoo, kwa mfano mafuta ya nazi hutumiwa kutengeneza bidhaa inayo saidi a nywele kutoharibiwa na kemikali

Mafuta ya nazi pia hupatikana katika bidhaa za urembo kama wile lipstiki. Pia hupatikana katika sabuni ya kufuliana dawa ya mswaki.

Manukato

Chanzo cha picha, Getty Images

Viwango vya juu vya uharibifu wa hewa vimeendelea kuangaziwa lakini una habari manukato huenda ni sehemu ya tatizo hilo?

Katika ripoti yake ya mwaka 2016 taasisi ya madaktari ya Royal, ilionya kuwa sio uchafuzi wa hewa nje ambao watu walihitaji kuwa na wasiwasi nao bali pia hali duni ya hewa katika nyumba zetu, zinazosababishwa na bidhaa za kila siku kama vile manukato ya kufanya nyumba inukie vizuri.

Mara nyingi manukato hayo imetengenezwa na kemikali inayofahamika kama limonene, ambayo hutumiwa kuleta harufu ya citrus - na pia kwa chakula.

Tatizo sio utumizi wa kemikali hiyo lakini inapochanganyika na hewa safi ya mazingira inaweza kuwa na madhara