Utawala wa Trump kurejesha vikwazo vyote dhidi ya Iran

Rais Trump alianza kurejesha vikwazo dhidi ya Iran tangu mwezi Mei

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Rais Trump alianza kurejesha vikwazo dhidi ya Iran tangu mwezi Mei

Utawala wa Trump umerejesha vikwazo vyote vya Marekani vilivyokuwa vimeondolewa chini ya mkataba wa nuklia uliyofikiwa mwaka 2015.

Ikulu ya Marekani imesema "hivi ni vikwazo vigumu kuwahi kuwekwa na utawala huu" dhidi ya Tehran. Inalenga Iran na mataifa yanayofanya biashara na Iran

Hata hivyo, mataifa manane yamepewa muda mfupi kuendelea kuingiza mafuta kutoka Iran.

Mataifa ya bara ulaya yanayounga mkono mkataba huo wa nuklia yamesema yatalinda kapuni za ulaya zinzaofanya biashara ''halali"na Iran.

Rais DonaldTrump alijiondoa kutoka kwa mkataba wa wa nuklia wa Iran mwezi Mei, na kutaja makubaliano hayo ya kupunguza shughuli za kinyukila za Iran uliofakiwa mwaka 2015 kama mbaya zaidi kuwahi kuafikiwa.

Siku ya Ijumaa Trump aliandika katika mtando wake wa Twitter akisema "Vikwazo vinakuja,"

Marekani imekuwa ikiregesha pole pole vikwazo dhidi ya Iran, lakini hatua hii ya sasa ni muhimu kwa sababu inalenga sekta kuu ya uchumi wa Iran.

Makubaliano ya awali yaliifanya Iran kupunguza shughuli zake tata za nuklia ili vikwazo dhidi yake vilegezwe.

Barack Obama, rais wa Marekani wakati huo, alihoji makubaliano hayo yalilenga kuzuia Iran kusitisha uundaji wa silaha za nuklia.

Uingereza, Ufaransa, Ujerumani Urusi na Uchina pia ziliunga mkono mkataba huo wa nyuklia wa Iran na kuendelea kuudumisha.

Kwa nini Marekani ikajiondoa?

Rais Donald Trump alitangaza kujitoa katika mkataba wa kimataifa wa nyuklia wa Iran mwezi Mei na kuuita mpango uliooza na kero kwa raia wote wa Marekani.

Alisema mpango huo unaifaidi tu na kuiongeza nguvu Iran.

Hatua gani zitachukulia?

Vikwazo hivyo Marekani dhidi ya Iran vitaanza kutekelezwa tena kuanzia Jumatatu Novemba 5, na vitakuwa na athari kwa sekta ya kawi na ile ya uchukuzi wa majini nchini Iran bila kusahau bishara ya mafuta, na biashara kati ya taasisi za kifedha za kigeni na benki kuu ya Iran.usafiri wa meli, fedha na nishati.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Sekta ya mafuta ya Iran inakabiliwa na vikwazo vipya

Iran imejibu vipi hatua hiii mpya ya Marekani?

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Iran,Bahram Qasemi amekiambia kituo cha kitaifa cha runinga ya nchi hiyo kwamba ''tuna habari kuhusiana na vikwazo hivyo lakini tuna uwezo wa kukabiliana na masuala ya kiuchumi ya taifa letu''

Alisema kuwa''hakuna uwezekano''wa Marekani ''kufikia malengo yake ya kisiasa kupitia vikwazo kama hivyo''

Vikwazo hivyo ni vipi?

Bwana Trump alitia saini agizo kuu ambalo lilirudisha vikwazo dhidi ya taifa hilo siku ya Jumanne. Vikwazo hivyo vinalenga:

Ununuzi wa noti za Marekani unaofanywa na Iran.

Biashara ya dhahabu na vyuma vingine

Graphite, aluminium, chuma, mkaa na programu zinazotumiwa katika sekta ya viwanda

Ubadilishanaji wa fedha unaohusishwa na sarafu ya Iran

Vitendo vinavyohusishwa na ulipaji madeni ya Iran