Umoja wa Ulaya washutumu ukiukaji wa haki za binaadamu Tanzania

Mkuu wa ujumbe wa umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Balozi Roeland van de Geer, akiwa na Rais wa Tanzania, John Magufuli Haki miliki ya picha IKULU TZ
Image caption Mjumbe wa Umoja wa Ulaya Tanzania, Balozi Roeland van de Geer, aliitwa kurudi nyumbani Brussles mwishoni mwa Juma.

Umoja wa Ulaya unasema umemuita mjumbe wake nchini Tanzania kwa mashauriano pamoja na kutathmini upya uhusiano wake na nchi hiyo kutokana na kuongezeka kwa ukiukaji wa haki za binaadamu Tanzania.

Taarifa ziliibuka mwishoni mwa juma nchini Tanzania kwamba mjumbe wa Umoja wa Ulaya nchini humo, Balozi Roeland van de Geer, ameitwa kurudi nyumbani Brussles Ubelgiji.

Gumzo kubwa limekuwepo kuhusu operesheni ya kuwasaka na kuwachukulia hatua wapenzi wa jinsia moja iliyo idhinishwa na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda inayoanza rasmi leo Jumatatu tarehe 5 Oktoba.

Njia ya jadi ya kufunga uzazi wa wasichana Kenya

Serikali ya Tanzania 'yamruka' Makonda

Abdul Nondo ashinda kesi ya 'kujiteka'

Makundi ya kutetea haki za binaadamu yameikosoa operesheni hiyo kwa kukiuka haki za kimataifa za binaadamu.

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binaadamu Amnesty International lilieleza kwamba kampeni hiyo itashinikiza chuki miongoni mwa umma.

'Serikali ina jukumu la kumlinda kila mtu nchini Tanzania na kuwahakikishia haki zao za binaadamu bila ya ubaguzi', amesema Joan Nyanyuki, Mkurugenzi wa Amnesty International Afrika mashariki, Upembe wa Afrika na eneo la maziwa makuu.

Katika taarifa rasmi Umoja huo umeeleza, "Umoja wa Ulaya unajutia kupungua kwa haki za binaadamu na mkondo wa sheria Tanzania na itafanya ukaguzi m'pana wa uhusiano wake na Tanzania."

Makonda aliunda kamati maalum ya watu 17 inayohakikisha kuwa watu wanaofanya biashara chafu za ngono wanachukuliwa hatua za kisheria.

Serikali ya Tanzania hatahivyo, imesema itaendelea kuheshimu mikataba yote ya kimataifa ambayo imeisaini na kuiridhia.

Imejitenga na kampeni hiyo ya kuwakamata na kushtaki mashoga inayoongozwa na Bwana Makonda.

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya nje ya Tanzania iliyotolewa Jumapili, Novemba 4 inadai kampeni hiyo ni mawazo binafsi ya Makonda na si msimamo rasmi wa serikali.

"Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea na itaendelea kuheshimu na kulinda haki hizo kama zilivyo katika Katiba," imesema taarifa hiyo.

Kufuatia tangazo hilo Marekani imeonya raia wake wanaoishi Tanzania wajihadhari kwa kuondoa au kuficha "picha na lugha ambayo huenda zikakiuka sheria za Tanzania kuhusu mapenzi ya jinsia moja na kuonyesha wazi picha za ngono".

Trump anafaa kuwa na hofu uchaguzi Marekani?

Je unaijua faida ya parachichi?

Mapenzi ya jinsia moja ni haramu katika baadhi ya nchi Afrika ikiwemo Tanzania.

Mwaka jana, naibu waziri wa elimu nchini alitetea tishio la kuchapisha orodha ya majina ya wapenzi wa jinsia moja, ambao wengi hulazimika kuishi kwa kujificha Tanzania.

Nchi ambayo kauli kali dhidi ya wapenzi wa jinsia moja zinaonekana kuongezeka, huku zile za makundi ya kutetea haki za watu wa jamii hiyo zikionekana kudidimia, angalau tangu rais Magufuli aingie madarakani mnamo 2015.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii