Uraibu wa kingono: Tatizo lipo kweli na ni la aina gani?

Haki miliki ya picha Karen Charmaine Chanakira
Image caption Uraibu wa kingono upo

Ni mwaka sasa tangu mwandaaji maarufu wa filamu duniani Harvey Weinstein alifanya maamuzi ya kwenda kwenye kituo maalumu cha kupambana na uraibu wa kingono.

Hii ni baada ya mfululizo wa shutuma za kuwadhulumu watu kingono, shutuma ambazo zilisababisha kukua kwa kampeni ya #Metoo iliyolenga waathirika wa ubakaji kuweka wazi yaliowasibu.

Mwandishi wa BBC Sangita Myska amekutana na watu wanao sema kuwa wamesumbuliwa na uraibu wa kingono ili kufahamu zaidi kama tatizo hilo lipo kweli, na kama lipo ni la aina gani.

Kazi ya kwanza ya Neila huko Uingereza baada ya kutoka katikati ya bara la Asia miaka 15 iliyopita, ilikuwa ni kwenye kampuni ya fedha ambayo ilikuwa imezungukwa na wanaume wababe kama asemavyo yeye kwamba walikuwa wanajipatia pauni milioni moja kama hela ya ziada.

Alikuwa ni mmoja kati ya wanawake wawili tu katika timu nzima, na wafanyakazi wenzao wakiume walikua wakiwachokoza kwa kucheza video za ngono kwenye televisheni kubwa ambazo zilitakiwa kuonyesha taarifa za masoko.

"Sikupenda lakini ilikuwa ndio mwanzo wa ajira kwangu iliyo nifungulia njia katika jiji. Ilinilipa vizuri na ilikua kazi ya kisasa na sikutaka kupoteza fursa hiyo," anasema.

"Nilijua wanaume wa ofisini walikua wakitaka niwajibu, walitaka kunishitua. Hivyo nilianza kwenda nyumbani na kuangalia video za ngono mwenyewe, hivyo ofisini sikushtuka tena. Kwa haraka nilibobea japo nilizaliwa katika familia yenye maadili makali ambapo ngono si jambo la kujadiliwa," anasema.

Kila siku alikuwa akifikiria atafikaje nyumbani kwa haraka ili achague filamu ya ngono na midoli yake ya ngono ili aaanze kujichua.

Haki miliki ya picha Karen Charmaine Chanakira
Image caption Hali hii huanza kidogo kidogo na baadhi ni kutokana na kutazama picha za ngono

Neila alimwelezea mwandishi wa BBC namna alivyokuwa anajiskia.

"Ilianza kidogo kidogo, hisia zinapanda sanaa. Na unaendelea kuangalia na kila mara unahamia kwenye vifaa vyako. Kila famamu zako zime sisimuka, unatazama kitu kinacho kufurahisha.Akili yako ipo mahali kwingine kabisa. Unajua haiwezi kuacha mpaka ubonyeze kitufe cha kusimamisha video. Unajua unasimamia mwenyewe raha yote unayoipata na inakufanya unafika kileleni namna ambayo binadamu hawezi kuku fikisha- na hasa mwanaume.

"Hali ya kujichua na kufika kileleni itakuchukua muda wa dakika tano mpaka kumi, lakini unarudi nyuma kwasababu hutaki kabisa kuiacha hiyo hali, ambayo ni kama umelewa,"

Akitumia njia hiyo alikuwa akitazama video za ngono kwa masaa mawili mpaka matatu kwa siku saba za wiki.

Tabia yake ilibadilika, anasema, asipo angalia picha za ngono, alipata kiu. Alikua akitumia masaa na masaa akijiambia kuwa anachokifanya si kosa alijiambia "Kila kitu kipo salama,huwezi pata magonjwa ya zinaa, huna haja ya kujipodoa. Kila kitu ni kwa maamuzi yako na unapata matokeo ya uhakika".

Lakini ili kuendelea kupata matokeo ya uhakika aina ya picha za ngono alizokuwa akiangalia zilimpeleka upande mbaya zaidi.

"Kwa kawaida unanza kuangalia picha za ngono za Vanilla, yaani mwanaume kwa mwanamke au mwanamke kwa mwanamke, hizi za kawaida. Lakini baada ya muda zinakuwa hazikupi midadi tena. Mwili wako unazizoea. Nisawa sawa na madawa ya kulevya unahitaji kuongeza dozi. Ili kuongeza unatazama zile picha za ngono za kibabe zaidi.

"Unaanza kuangalia zile za kufanya mapenzi kinyume na maumbile, baada ya muda ile inakuwa kawaida hivyo unaanza kutafuta nyingine ngumu kama vile zile picha za ngono za mtungo mfano wanaume wengi wanawake wawili.

Haki miliki ya picha Karen Charmaine Chanakira
Image caption Uraibu wa kingono ni matendo ya ngono yasiyo ya kawaida.

Hii ilianza kumkosesha raha Neila, ambaye alianza kuona ana kosa raha kadiri anavyo endelea.

Suala la kudhalilika ndio kitu abacho huleta hofu kubwa kwa kila mtu anayeamini kuwa yeye ni mraibu wa kingono. Aibu huwafanya waendelee kujificha na huwaendesha zaidi kuendelea na hali yao. Picha za ngono ni mchanganyiko wa mihemko na aibu," Neila anasema

Picha za ngono zimebadilisha namna anavyo tazama wanaume. Alipokuwa akijaribu kutafuta mwanaume wa kudumu tabia zao zilikuwa haziendani na alivyotaka.

"Nitaangalia kupitia mashati yao kama wana six pack" anasema. Urefu wa uume wa wanaume wa uingereza haukua unatosha kwangu. Lakini najua si njia nzuri ya kuchagua mwenza wa maisha."

Alikuwa namahusiano mengi yaliyo shindikana, lakini ukweli ni kwamba video za ngono alizokuwa anaangalia zilizokuwa zimebeba maudhui ya unyanyasaji dhidi ya wanawake ili kupata mihemko ndizo zilikuwa zikimpa hofu.

"Ilibidi nijiulize mwisho wake ni nini sasa, je nitaendelea kutazama video za ngono ili kujiridhisha na kukidhi hamu yangu.

Neila ameondoka mjini humo na sasa ni mtoa ushauri nasaha. Akiwa katika miaka 40 ameamua kuwa mtoa ushauri kwa wagonjwa wengine ambao wanaamini kuwa wameathirika na uraibu wa kingono.

Na kituo anacho tumia kuelimisha watu ndio kituo pekee kinachohudumia watu wa aina kama hiyo huko uingereza. Kupata huduma hiyo unalipia ma elfu ya pound kwa muda wa saa moja kwasababu kituo cha taifa cha kushughulika na Uraibu hakitambui kama uraibu wa kingono ni tatizo. Lakini inakadiriwa kuwa mamia kama sio ma elfu ya watu wanahitaji kupata matibabu ya hali hiyo kila mwaka huko uingereza, wengi wao ni wanaume.

Je uraibu wa kingono upo?

  • Shirika la afya duniani WHO hivi karibuni liliongeza tabia za kingono zisizo za kawaida katika orodha yake ya matatizo ya siyo ya kawaida.
  • Shirika la afya la uingereza halitambui kama uraibu wa kingono ni ugonjwa - na haijaweka takwimu maalumu.
  • Ukurasa wa mtandao shirika la afya uingereza umeandika uraibu unahusishwa na Kamali, madawa ya kulevya, pombe, na dawa za usingizi na kuongeza kuwa kuwa na uraibu wa kitu maanayake ukikosa hicho kitu unakuwa na dalili zote za kutokuwa sawa.
  • Kliniki zisizo za kiserikali uingereza zina taarifu kuwa maelfu ya watu kama sio mamia ya watu wanawafwata kila mwaka kuomba msaada wa kutibu hali hiyo.

Sababu ya tatizo hili ni kwamba wanawake wanaona aibu zaidi na inawapa ugumu katika kukiri tatizo na kuomba msaada. Lakini pamoja na maelezo yote. Paul ni mmoja wa wale waathirika zaidi na anahitaji msaada kuachana na uraibu wa kingono, moja ni kwa sababu ni mwanaume na pia hufika kileleni kwa kufanya ngono na si kuangalia picha za ngono.

Haki miliki ya picha Karen Charmaine Chanakira
Image caption Mawazo ya kujihukumu baada ya kumaliza ngono hubaki kichwani

Akiwa na takribani miaka 50 mreefu na aliyevalia vyema shati jeupe na koti. Paul anamwambia mwandishi wa BBC kuwa uraibu wake ulianza miaka 30 iliyopita akiwa chuo kikuu. Alikuwa na mahusiano mazuri na msichana wake lakini siku moja mahusiano yale yalikuwa hayatoshi kwake.

"Nilimpenda, kweli nilimpenda lakini sijui kwa sababu gani nilienda kumfwata kahaba," anasema. Nilikuwa nina haja sana ya kufanya ngono ya kipekee na tofauti na nilijua hiki ni kitu ambacho sitakiwi kukifanya. Sikuwahi kumsaliti lakini kwa kahaba niliona ni kitu tofauti."

Ndani ya wiki kadhaa tabia hii ilibadilika kabisa.

"Nilikuwa na mahusiano na wasichana sita kwa wakati mmoja na nilikuwa nakutana na makahaba wawili au watatu kwa wiki. Ilikua ni kama kuagiza chakula kwa sababu nina njaa. Nahitaji kitu, naagiza kinakuja kisha nasahau."

Anasema alijua kunakitu hakiko sawa. Na muda alipoanza kufikiria kumshirikisha mtu au kuto kufanya hivyo au hata kupata msaada, akapata kazi yake ya kwanza huko London - na akajikuta yupo kwenye mazingira ambayo tabia kama hii yake inakubalika sana.

"Huwezi amini, kusafiri nchi mbali mbali duniani, kujiingizia pesa nyingi sana kuhudhuria mara kwamara kwenye makasino na Bar Londonunajikuta mpaka unaingia kufanya ngono na watu unao fanya nao kazi, Paul anakumbuka. Sasa kwa kipindi hiki nafikiria labda nina tatizo? Au labda ni mwanaume tu wa kawaida?"

Haki miliki ya picha Karen Charmaine Chanakira
Image caption Je Uraibu wa kingono kweli upo?

Hata kwa kipindi hicho, mawazo ya kujihukumu yalibaki kichwani kwa Paul.

Atakwenda na wafanya kazi wenzie kwenye bar zenye wadada ambao huwachezea wanaume na kuwa kalia wakiwa watupu na kila mmoja atatumia Euro 1000 kwa usiku mmoja kwa siku za jumanne labda na kwenda tena siku za alhamisi. Lakini Paul pekeake alijikuta anarudi tena pale siku za jumamosi.

Kama Neila, Paul anasema alianza kutafuta kitu kingine kisicho kawaida ili kumpa raha ambapo baada ya kuwa mwanaume anaye fanya mapenzi na wanawake kwa miaka zaidi ya kumi akaanza kushiriki ngono na wanaume wenzie.

"Nikahama kabisa kutoka kwa wanawake mpaka kwa wanaume.Kwa hiyo sikuzote nilianza kutoka na wanaume. Naweza sema nina kiasi cha ushoga ndani yangu. Ni kutafuta muhemko wa hali ya juu tu. Na kipindi chote hicho nilikuwa na wasichana wazuri sana.

Subiri kwa mwaka mmoja kabla ya ujauzito mwingine

Kama alivyo sema Neila, Paul anasema tabia yake ilikuwa haizuiliki, kama hafanyi ngono alikuwa anapata kiu ya ngono. Na malengo yake yalikuwa si kufka kileleni bali ilikuwa ni tabia tu ambazo zilikuwa zinampa raha.

"Raha yangu ilikuwa ni kuwaza kile kitu ninakwenda kukifanya, kitu ambacho nilikuwa sitaki kitokee ni ku fika kileleni kwa sababu hapo shughuli yote inakuwa imeisha."

Haki miliki ya picha Karen Charmaine Chanakira
Image caption Ilimchukua Paul muda mrefu kuanza kutazama picha za ngono, baada ya kuzijua akiwa na miaka 12.

Ilimchukua Paul muda mrefu kuanza kutazama picha za ngono, baada ya kuzijua akiwa na miaka 12.

"Niliwahi kutana na majarida nikiwa bado kwa wazazi, niliyakuta yamefichwa wazazi wangu wakiwa hawapo. Hivyo ndio nilivyo anza kujua ngono. Lakini kuwa muwazi sikuwahi kupata ashki." Hayo yalibadilika baada ya kupata mtandao wenye kasi. Kwa kipindi hicho mawazo yake yalihama kutoka makahaba mpaka kwenye picha za ngono ambazo aliangalia kwa masaa na masaa.

Paul amepokea msaada kwa muda mrefu kutoka katika kituo cha Laurel, na sasa anaamini anaendelea vizuri na anapona. Haja lala na makahaba kwa miaka sasa na hajaangalia picha za ngono kwa miezi kadhaa, anasema.

Malengo yake ni kutulia kuanza upya na mwanamke mmoja tu.

"Ni ugonjwa wa upweke,Unafika mahali unatambua kwamba una muda mchache wa kushi duniani. Sijawahi kufanya ngono na kusikia raha na mtu ambaye nina mpenda na nina mjali. Ni kitu ambacho nimekikosa kwa miaka 30."

Mwezi wa sita, shirika la afya duniani lilitambua rasmi kwamba tabia za ajabu za kingono ni ni ugonjwa wa kimataifa. Washauri wa afya wanasema japo kuwa hakuna utafiti wa kutosha kuthibitisha rasmi kuwa ufanyaji ngono kupita kiasi ni uraibu, ni muhimu kwa serikali kutoa huduma ya ushauri nasaha kupitia mashirika yake.

Mwandishi wa BBC anasema kwa utafiti mdogo alio ufanya uraibu wa kingono ni tatizo na watu wanahitaji kusaidiwa.

Hata hivyo baadhi huofia kwamba kwenda kwenye huduma za kupata msaada wa kupambana na uraibu yaani rehab inatoa ishara kwamba unatafuta kisingizio cha kukwepa kukubali tabia zako.

Na katika kundi lililo hojiwa na BBC wanatambua kuwa kuna tofauti ya kufanya ngono kwa makubaliano na kuto kuwepo kwa makubaliano. Na wote hakuna aliyefanya uhalifu ila kwa kawaida watu hawa huanza kwa kujiumiza wenyewe kisha wapenzi wao. Wakati maharamia wa kingono wao huwajeruhi watu wanao watumikisha kingono.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii