Watayarishaji wa kipindi cha Sabrina washtakiwa na hekalu la shetani

Mwanzilishi wa hekalu la shetani Lucien Greaves Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mwazilishi wa Hekalu la shetani Lucien Greaves anasea kuwa ishara ya kundi hilo inatumika vibaya.

Kundi la wanaharakati wa hekalu la shetani linawashtaki watengenezaji wa kipindi cha msururu cha runinga -The Chilling Adventures of Sabrina kwa gharama ya $50 million (£38m) kutokana na sanamu.

Netflix na Warner Bros wanadaiwa kunakili sanamu ya kundi hilo Baphomet katika kipindi hicho.

Kampuni zote mbili zimekataa kuzungumzia swala hilo.

Hekalu la shetani haliamini nguvu zisizo za kawaida za shetani , lakini linataka kuendelea kuwashawishi wafuasi zaidi kujiunga nalo.

Kesi hiyo iliowasilishwa mjini New York inadai kwamba sanamu inayofanana inaonekana katika vipindi vinne vya kipindi hicho.

Lucien Greaves , mwanzilishi wa hekalu la shetani, alichapisha ujumbe wa twitter akifananisha sanamu yao na ile inayoonyeshwa katika kipindi hicho.

Kipindi cha The Chilling Adventures of Sabrina ni kipindi chenye watu wasio na nguvu za kawaida katika Netflix kufuatia Sabrina Spellman, kijana ambaye alifariki na ambaye anashiriki uchawi.

Kinatokana na kitabu cha ucheshi kwa jina hilo hilo ambacho kilishawishi kipindi hicho cha Sabrina the Teenage Witch, kilichoanza 1996-2003.

Waigizaji katika kipindi hicho wanaoabudu 'mungu mweusi' ama shetani anayekula wenzake na kuabudu kwa lazima na hekalu la shetani wanadai kwamba wanachama wake wanashirikishwa na 'uovu huo wa upinzani'.

Bwana Greaves alithibitisha kuwa kundi hilo huenda likachukua hatua za kisheria dhidi ya kampuni zinazotayarisha kipindi hicho kwa kunakili sanamu yao ili kukuza uigizaji wa kipindi chao cha kishetani.

Hekalu hilo la shetani lilitengeneza sanamu ya mbuzi kwa jina Baphomet ikiwa ni miongoni mwa kampeni zake kutengeza sanamu ya amri kumi za mungu katika mji wa Oklahoma kwa lengo la kuwa na uhuru wa kidini.

Bwana Greaves aliambia chombo cha habari cha Marekani CNBC kwamba Baphomet amekuja kutuwakilisha sisi kama watu na kwamba sanamu hiyo ya Sabrina inalidharau kundi lao.

Je hekalu la shetani ni lipi?

Likianzishwa mwaka 20102 , kundi hilo linafanya kazi kuhakikisha utengano wa kanisa na taifa na linamchukulia shetani kama ishara ya upinzani na mamlaka.

Huku likiwa na majumba 15 ya mikutano nchini Marekani , uanachama wa kundi hilo uliimarika kabla ya uchaguzi wa rais Donald Trump mwaka 2016.

Katika hotuba yake , bwana Greaves anasema kuwa hekalu hilo lilivutia uanachama wa takriban watu 100,000 huku maelfu wakituma maombi ya usiku kucha baada ya uchaguzi huo.

Baphomet ni nani?

Ni sanamu ya, Baphomet ni kiumbe mwenye kichwa kinachofanana na cha mbuzi lakini ameongezwa maungo ya ajabu.

Ni kiumbe huntha mwenye mabawa, na kwenye sanamu hiyo inayotumiwa kwa sasa huoneshwa akiwa na watoto wawili wanaotabasamu.

Sanamu inayotumiwa kwa sasa ina urefu wa karibu futi 9, na iligharimu $100,000 (£64,000) kuitengeneza.

Sanamu hii imekuwa ikitumiwa kuwapiga vita wale walio na imani za Kikristo na imani nyingine zenye kumcha Mungu mmoja. Ni sanamu hii ambayo imekuwa ikitumiwa kuendesha vita dhidi ya kuwekwa kwa sanamu za Kikristo na dini nyingine katika majengo maarufu, bustani na maeneo ya umma nchini Marekani.

Agosti 17, sanamu hiyo ya kiumbe anayefahamika kama Baphomet ilipelekwa katika jimbo la Arkansas anakotoka rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton.

Wanaotumia sanamu hiyo ni watu wa kundi linalofahamika kama Satanic Temple (Hekalu la Shetani) ambalo ni kundi la 'kidini' na kisiasa ambalo hupinga kuingizwa kwa dini katika masuala ya serikali.

Kundi hilo liliandaa maandamano ya watu 150 waliyojumuisha waabudu shetani, watu wasioamini Mungu yupo na Wakristo pia.

Maandamano hayo yalifanyika nje ya jengo lililo makao makuu ya jimbo la Arkansas katika mji wa Little Rock.

Walikuwa wamekerwa na hatua ya kuweka sanamu ya Mnara wa Amri Kumi za Mungu katika uwanja wa makao makuu hayo.

Satanic Temple walisema sanamu hiyo inakiuka Sheria ya Kwanza ya Marekebisho ya Katiba nchini Marekani ambayo huzungumzia uhuru na haki za kidini.

"Ikiwa utakubalia kuwepo kwa sanamu ya dini moja basi kunafaa kuwa na uhuru kwa wengine kuweka sanamu za kidini, na ukizuia basi kusiwe na sanamu yoyote ile," mwanzilishi mwenza wa tawi la Satanic Temple katika jimb la Arkansas Ivy Forrester alinukuliwa na wanahabari siku hiyo ya maandamano.

Haki miliki ya picha Matt Anderson
Image caption Sanamu ya Baphomet inayotumiwa na Satanic Temple

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii