Uholanzi: Mwanaume mmoja wa miaka 69 anataka kupunguza miaka 20 ya umri wake kisheria

Emile Ratelband anadai kuwa yeye ni mungu mdogo Haki miliki ya picha AFP/GETTY IMAGE
Image caption Emile Ratelband anadai kuwa yeye ni mungu mdogo

Mkufuzi mahiri kutoka Uholanzi anataka kubadilisha umri wake kisheria na kuongeza matarajio yake ya mahusiano ya kimapenzi.

Emile Ratelband mwenye umri wa miaka 69, anataka kubadilisha siku yake ya kuzaliwa kutoka mwezi Machi 1949 mpaka kuwa Machi 1969, akilinganisha na mabadiliko ya kubadilisha jinsia.

"Tunaishi katika wakati ambao unaweza kubadili jina lako na kubadili jinsia yako.

Kwa nini siwezi kuwa na maamuzi ya umri wangu?" Ratelband alisema.

Mahakama moja mashariki mwa mji wa Arnhem inatarajia kusikiliza kesi hiyo nadini ya wiki nne zijazo.

Hata hivyo mamlaka ilitilia shaka kesi hiyo wakiamini kuwa hakuna sheria ambayo inamruhusu mtu kubadili siku yake ya kuzaliwa ,Vyombo vya habari vya nchi hiyo viliripoti.

Jaji mmoja ametaka kujua ni nini ambacho kitatokea baada ya bwana Ratelband kutaka kupunguza miaka yake 20.

"Wazazi ambao watakuwa wanakuangalia watakuwa ni kina nani?Huyo mtoto mdogo alikuwa nani?" Jaji aliuliza.

Kwa nini Mwanaume huyo anataka kubadili umri wake

Ratelband amedai kuwa huwa anahisi kutengwa kwa sababu ya umri wake.

Na hali hiyo huwa inamkosesha fursa za kupata ajira na kufanikiwa kupata wenza katika tovuti ya Tinder.

"Nikiwa nna umri wa miaka 69, ni kama nimefungwa. Kama nikiwa na miaka 49 basi nnaweza kununua nyumba mpya na magari ya aina tofauti tofauti.

Ninaweza pia kupata kazi nyingi zaidi", Ratelband alibainisha.

Haki miliki ya picha Getty Images

Aliongeza kwa kudai kuwa akiwa kwenye mtandao wa Tinder ambao unasema umri wake ni 69,huwa hapati majibu.

Hivyo akiwa na umri wa miaka 49 na kwa muonekano wake ulivyo basi anaweza kuwa katika nafasi nzuri ya kifahari.

Ratelband amesema kwamba kwa mujibu wa daktari wake, mwili wake ni wa mtu mwenye umri wa miaka 45 na kujielezea mwenyewe kuwa yeye ni mungu mdogo.

Aliandika kwenye ukurasa wa Facebook mwaka jana na kuelezea namna ambavyo aliamua kuchukua uamuzi huo.

Alidai kwamba alifanya uamuzi huo siku moja alipokuwa anajiangalia katika kioo na sio kwa sababu alikuwa na hofu ya kuwa mzee lakini anataka kuishi muda mrefu awezavyo.

Ratelband alisema kuwa atatangaza tena mafao yake kama atabadili siku yake ya kuzaliwa.

Ratelband anafanya kazi katika vyombo vya habari na mhamasishaji ambaye pia ni mkufuzi wa vipindi.

Huwa anasoma sauti ya muigizaji Vladimir Trunkov katika lugha ya Kiholanzi katika filamu ya Pixar film Cars 2.

Mada zinazohusiana