Bobi Wine: Nyota wa muziki wa pop na mbunge afanya tamasha la kwanza tangu akamatwe

Bobi Wine appears on stage on the outskirts of Kampala Haki miliki ya picha AFP
Image caption Bobi Wine

Nyota wa muziki wa pop na mbunge wa upinzani nchini Uganda Bobi Wine amefanya tamasha lake kwanza tangu ashtakiwe na kufungwa kwa mshtaka ya uhaini.

Kulikuwa na idadi kubwa ya polisi kwenye tamasha hilo, ambalo liliruhusiwa tu kufanyika kwa sababu halikuwa la kisiasa.

Bobi Wine anadaiwa kuteswa na kupigwa akiwa kuzuizi mwezi Agosti, madai yanayokanwa na mamlaka.

Umaarufu wake miongoni mwa vijana nchini Uganda unaonekana kuwa changamoto kubwa kwa rais wa miaka mingi Yoweri Museveni.

Baadhi ya maelfu ya watu waliohudhuria tamasha walivaa nguo nyekundu, rangi inayohusishwa na vuguvugu la Bobi Wine la People Power.

"Ninashukuru polisi wa Uganda kwa kutupa ulinzi na kutotuzuia kama vile wamekuwa wakifanya awali," Bobi Wine aliuambia umati kwa mujibu wa AFP.

"Sisi ni watu wenye amani na tunataka kusikilizwa."

Mbunge huyo mwenye miaka 36 ambaye jina lake kamili ni Robert Kyagulanyi, aliwania na kushinda kama mgombea huru kwenye uchaguzi mdogo huko Kyadondo East kati kati mwa Uganda

Mwezi Agosti yeye pamoja na wanasiasa wengine 30 wa upinzani walishtakiwa kwa uhaini baada ya msafara wa rais kutupiwa mawe baada ya mkutano wa kampeni.

Aliondoka nchini Uganda kwenda kupata matibabu nchini Marekani kufuatia majeraha aliyoyapata akiwa kizuizini lakini akarudi nyumbani mwezi Septemba.

Idadi kubwa ya watu nchini Uganda wako chini ya miaka 35 na Wine amekuwa kama mfano wa vijana wenye ghadhabu ya ukosefu wa ajira na siasa zilizokwama.

Bobi Wine alizaliwa miaka minne kabla ya Bw Museveni kuwa rais mwaka 1986 na amekuwa akitoa wito kwa Museveni astaafu kutokana kwa siasa za mwaka 2021.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Tamasha hilo lilifuatiliwa kwa karibu na polisi
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Maelfu walihudhuria tamasha katika vitongoji vya mji wa Kampala
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Bobi Wine amelkuwa mfano kuigwa na vijana wa Uganda

Mada zinazohusiana