Mwaka mmoja wa habari za uongo barani Afrika

Picture of globe zoomed in on Africa with a c computer, mobile phone and a magnifying glass with an exclamation mark inside it.

Kuenea kwa taarifa zisizo sahihi barani Afrika kumelaumiwa katika kuchochea chuki , kuwachanganya wapiga kura na pia kusababisha kushuka kwa uchumi.

Utafiti mpya wa BBC kuhusu taarifa zisizo sahihi barani Afrika, umeangazia taarifa tano ambazo zilileta matokeo makubwa barani humo ndani ya miezi 12.

1. Rais wa Tanzania kuhamasisha ndoa za mitara ili kutokomeza ukahaba

Haki miliki ya picha Zambian Observer

Habari ni nini?

Makala inayodaiwa kwamba rais wa Tanzania John Magufuli aliwaambia wanaume kuoa mke zaidi ya mmoja ili kukomesha ukahaba ilienea sana.

Taarifa hiyo ilidai kwamba rais alitoa tamko hilo katika mkutano uliojumuisha wanaume 14,000 na kuwaambia kuwa kati ya watanzania milioni 70 ,milioni 40 ni wanawake na wanaume ni milioni 30 tu.

Makala hiyo iliyodai kuwa wanaume ni wachache kuliko wanawake kunaongeza kasi ya biashara ya ngono na ongezeko la wanandoa kutoka nje ya ndoa zao.

Taarifa hiyo ilisababisha matokeo gani?

Mara ya kwanza makala hiyo iliandikwa kwa lugha ya kiingereza katika tovuti ya 'Observer' nchini Zambia mwezi februari mwaka 2018 ingawa haikusomwa na wengi.

Lakini ilipoandikwa katika lugha ya kiswahili, ambayo ni lugha ya taifa nchini Tanzania katika mtandao wa nipasheonline.com .

Taarifa hiyo ilichapishwa pia katika mtandao maarufu ya JamiiForums na kusambaa katika mitando mingine nchini Kenya, Zambia, Afrika kusini na Ghana.

Je tunawezaje kutambua kuwa taarifa hizo sio sahihi?

Msemaji wa serikali alikanusha taarifa hiyo katika ukurasa wake wa Twitter na kusema kwamba rais hajawahi kutamka maneno kama hayo.

Taarifa hiyo ambayo haikuwa na ukweli ilidai, tatizo linatokana na wingi wa wanawake ukilinganisha na wanaume, kwa sababu idadi ya wanawake milioni 40 kwa wanaume milioni 30.

Huku takwimu ya hivi karibuni ya Umoja wa mataifa inakadiria idadi ya watanzania ni milioni 60, na haijagawa idadi ya wanaume na wanawake.

Haki miliki ya picha Twitter

Tovuti hiyo ambayo iliandika taarifa hiyo ilikuwa inafanana na gazeti maarufu la Nipashe nchini Tanzania .

Ingawa tovuti hiyo haikuwa na uhusiano wowote na gazeti la Nipashe ambalo tovuti yake halisi ni hii;

  • https://www.ippmedia.com/sw/nipashe

2. Mgombea urais wa Nigeria anaungwa mkono na vikundi vya haki za mashoga

Habari ni nini?

Kipindi ambacho Atiku Abubakar, alipochaguliwa kuwa mgombea urais katika uchaguzi wa Nigeria mwaka 2019, ukurasa wa bandia wa mtandao wa Twitter wenye jina la mpinzani uliandika ujumbe wa kuwashukuru jumuiya ya mashoga kwa kumuunga mkono.

Katika ujumbe huo, "Bwana Abubakar" ameandika kwamba jambo la kwanza ambalo atalifanya akichaguliwa kuwa rais ni kuondoa sheria ambazo zinawakandamiza wapenzi wa jinsia moja ambazo ziliwekwa na rais wa zamani wa Nigeria Goodluck Jonathan mwaka 2014.

Wapenzi wa jinsia moja wanahukumiwa kifungo cha miaka 14 gerezani huku ndoa za jinsia moja zikiwa zimekatazwa kabisa.

Taarifa hiyo ilisababisha matokeo gani?

Haki miliki ya picha The Nation

Mara baada ya ujumbe huo kuandikwa katika mtandao tarehe 14 Oktoba, blogu mbili nyingine ziliinukuu.

Siku 12 baadae, magazeti maarufu nchini Nigeria yalichapishwa taarifa hiyo hiyo.

Taarifa hiyo isiyo sahihi kuhusu mgombea urais anayehamasisha mapenzi ya jinsia moja ilitumika ili kumshusha kisiasa.

Kwa sababu viongozi wa dini wa kiislamu na kikristo ndio wenye ushawishi mkubwa nchini humo na waliungana kwa pamoja kupinga mapenzi ya jinsia moja.

Na ujumbe kama huo unaweza kuwapelekea viongozi hao kuwakataza waumini wao wasimpigie kura mgombea wa aina hiyo.

Tuna ueleo kiasi gani kuhusu taarifa zisizo sahihi?.

Ukurasa wa Twitter uliotumika kama chanzo cha taarifa kuhusu mgombea urais ulikuwa bandia na ukurasa wake rasmi ulikuwa na alama ya vyema yenye rangi ya bluu.

Huwezi kusikiliza tena
Je tunawezaje kujua kuwa taarifa hizo sio sahihi?

Na hakukuwa na barua rasmi kutoka kwa jumuiya hiyo ya wapenzi wa jinsia moja.

3. Wanahabari mashuhuri nchini Kenya walieneza sifa za uongo

Taarifa ilikuwa inahusu nini?

Mtangazaji wa habari za biashara katika shirika la utangazaji la CNN, Richard Quest alidaiwa kuwa nchini Kenya katika mji mkuu wa Nairobi mwezi oktoba kwa ajili ya kupiga picha za kipindi chake cha luninga.

Mtangazaji wa zamani Julie Gichuru aliandika katika mtandao wa twitter tarehe 25 oktoba akijadili namna ambavyo Quest alifurahia kufika Kenya.

Na kuandika jinsi Kenya ilivyo ya ajabu.

"Hakuna kitu kinachoweza kuzipita huduma zinazotolewa Kenya.

Hapa nimezungukwa na twiga wakati napata kifungua kinywa.Katika nchi ambayo benki ya dunia imeichagua kuwekeza barani Afrika, kitu gani kingine nakihitaji?Kenya inastaajabisha!"

Haki miliki ya picha Twitter

Taarifa hiyo ilisababisha matokeo gani?

Julie ambaye anafuatiliwa na watu zaidi ya milioni katika ukurasa wake Twitter na watu 600,000 kwenye Instagram, ndani ya dakika chache ujumbe huo uliwafikia maelfu ya watu na waliiamini taarifa hiyo kuwa ya kweli.

Je tunawezaje kutambua kuwa taarifa hizo sio sahihi?

Mwandishi huyo wa CNN alipoona ujumbe huo aliwasiliana haraka na Julie na kubaini kuwa sio yeye aliyeandika ujumbe ule.

Julie akajibu ujumbe ule na kufuta ukurasa wake.

4.Wasomali kuzikwa katika kaburi la kina kifupi Ethiopia

Taarifa ikiuwa inahusu nini?

Mwezi Julai, televisheni moja ya satelaiti nchini Ethiopia (ESAT) ilirusha video inayoonesha miili ya ya watu wenye asili ya Somalia wakizikwa katika kaburi la kina kifupi na watu wa kabila la Oromo Ethiopia.

Ilidai kuwa kanda hiyo ilirekodiwa katika eneo la Oromia Ethiopia, ambako kumeshuhudiwa ghasia kubwa kati ya makundi hayo mawili mwaka huu.

Taarifa hiyo ilikuwa na athari gani?

Haki miliki ya picha YouTube
Image caption Video hiyo ilionyesha miili ikisukumwa ndani ya kaburi la kina kifupi

Idhaa ya BBC Afaan Oromo iliripoti kwamba video hiyo iliyosambaa pakubwa katika mitandao ya kijamii Ethiopia ilisababisha mashambulio makali kwa watu wa kabila la Oromo wanaoishi katika nchi jirani ya Djibouti na Somalia.

Wakimbizi wa Oromo katika nchi jirani ya Djibouti waliiambia BBC kwamba walipigwa na maduka yao kuporwa mara baada ya video ile kusambaa.

Je tunawezaje kujuaje kuwa taarifa hio sio sahihi?

Video hiyo ambayo haikuthibitishwa, ilisambazwa Cameroon kiasi ya 3000 km magharibi mwa Ethiopia, mnamo Juni, wakati iliposemekana kuhusiana na mzozo wa sasa kati ya raia wa sehemu inayozungumza kiingereza wanaotaka kujitenga, na serikali.

Kanda iliyoonyeshwa kwenye TV ya ESAT pasi kuthibitishwa kumbe ilionekana pia kufanyiwa ukarabati, kwa kutumiwa sauti ya wanaoonekana kuwa ni vijana wa kabila la Oromo waliopiga kelele juu ya sauti halisi ya video hiyo.

Baada ya kugunduliwa kwamba video hiyo ni ghushi, ESAT iliiondoa kutoka kwenye majukwa yake yote na kuomba radhi rasmi katika mtandao wake wa Youtube.

Hakuna pendekezo lolote kwamba ESAT TV iliikarabati video hiyo au kuitangaza wakati ikitambua kuwa ni ya uongo.

Sahihisho Novemba 23: Taarifa hii imesahihishwa kuweka wazi kuwa ESAT TV haikuhusika kwa kuikarabati video, au kwamba ilitangaza kwa kujua video ya uongo.

5. Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma 'ajiuzulu'

Taarifa ilihusu nini?

Mwezi februari tarehe 12,mwandishi mmoja wa Afrika kusini SABC aliripoti kuwa rais Jacob Zuma alikubali amejiuzulu.

Taarifa hiyo ambayo ilikuwa imewanukuu viongozi kutoka ngazi za juu wa chama cha ANC, ambao walikuwa wanajadili kuhusu hatima ya kiongozi huyo.

Mwandishi mwingine wa Afrika kusini aliliweka tangazo hilo katika ukurasa wake wa twitter.

Zuma alikuwa anakabiliwa na shutuma nyingi za ufisadi na alikuwa anashinikizwa na chama chake kujiuzulu.

Hivyo taifa lilikuwa linasubiri taarifa kuhusu uwezekano wake wa kujiuzulu.

Je tunawezaje kutambua kuwa taarifa hizo sio sahihi?

Msemaji wake Zuma alikanusha taarifa hiyo na kudai kuwa ilikuwa sio taarifa sahihi.

Lakini siku tatu baadae, Zuma alijiuzulu kiukweli.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii