Lulu Jemimah: Mwanamke aliyejioa Uganda atimiza malengo kwa kupata ada ya Oxford

LULU JEMIMAH Haki miliki ya picha LULU JEMIMAH

Mwanamke aliyejioa nchini Uganda, Lulu Jemimmah, hatimaye amepata ada ya kusoma chuo maarufu cha Oxford kilichopo nchini Uingereza.

Bi Jemimma, 32, alikuwa anahitaji kiasi cha pauni 10,194 ili kumalizia mwaka wa pili na wa mwisho wa masomo yake ya uzamili. Baada ya kuchangiwa kwa kipindi cha mwezi mmoja, amefanikiwa kupata pauni 11,160 ambayo ni pauni 966 zaidi ya lengo.

Alifikia lengo siku ya Jumamosi na kuanzia jana amesitisha kupokea michango.

"Sihitaji taji tena mchango. Sikuwahi kufikiria kuwa ipo siku ningsema hivi, lakini sasa ninaacha kupokea mchango. Nina bahati sana. Nawashukuru sana kwa msaada wenu madhubuti," ameandika bi Jemmimah katika ukurasa wake wa mtandao wa Go Fund Me Page ambao alikuwa akiutumia kwa kampeni yake.

Mchango huo umetolewa na watu takriban 170, ambao waliguswa na kisa cha bi Jemmimah cha kujioa mwenyewe.

Ndoa mbili batili kufadhili elimu Uganda

Ukiacha mchango wa fedha, pia amepokea ufadhili wa tiketi za ndege kwa kipindi kilichobaki cha masomo yake baina ya Uingereza na Uganda.

"Siyo tu nimepata pesa ya ada, kwa sasa sina haja ya kuwa na hofu yeyote ya kuhamisha fedha katika benki, usafiri wa ndege na pesa ya kuombea viza," ameongeza bi Jemimmah.

Kwa nini alijioa

Haki miliki ya picha LULU JEMIMAH

Licha ya mafanikio ya kielemu kwa kujiunga na chuo maarufu duniani, anasema watu waliendelea kumuuliza swali moja ambalo kwa miaka kadhaa hakuwa analifurahia.

Swali lenyewe ni anapanga kuolewa lini, ili aanzishe familia na kupata watoto.

"Hawaamini kuwa kinachonifanya kuwa macho usiku sio hofu ya uwezekano wa kutopata bahati ya kutembea altarini kwenda kufunga ndoa."

"Nikiwa na miaka 16 baba yangu aliandika hotuba yake kwa ajili ya kuisoma siku ya harusi yangu. Kila nilipokuwa nasherehekea siku yangu ya kuzaliwa mama yangu alikuwa akiniombea, na kwa miaka ya karibuni maombi yake yalikuwa pamoja na kupata mume bora, ambaye atanifaa," amesema Bi Jemimah.

Kutokana na hali hiyo, Jemimah anasema aliamua kuchukua uamuzi wa kuwatuliza; "Nilipotimiza miaka 32 nikaamua kujioa. Naamini mimi nitajitunza na kujipa amani."

Harusi yake ilimgharimu kiasi cha dola 2 tu ambazo ni gharama yake ya usafiri. Aliazimisha gauni la harusi kwa rafiki, vito kutoka kwa dada yake na keki ya harusi iliokwa na kaka yake.

Waalikwa walitakiwa kujinunulia chakula na vinywaji kwa pesa zao wenyewe.

Kampeni ya ada

Haki miliki ya picha LULU JEMIMAH

Lengo la bi Jemimah ni kuionesha jamii yake kuwa inawezekana kufikia malengo kimaisha bila ya msaada wa mume.

Hata baada ya kujioa mwezi Agosti mwaka huu jijini Kampala Uganda, Bi Jemimah alikuwa anachangamoto moja ya kutafuta ada ya kumalizia masomo yake.

Alitumia ndoa yake hiyo, ambayo baadhi ya watu, wanaiona kama kituko kufanya kampeni mtandaoni ili kupata usaidizi wa kulipa ada hiyo.

Katika mwaka wake wa mwanzo wa masomo Bi Jemimah anasema alikumbana na changamoto nyingi za kifedha zilizomfanya aishi katika mazingira magumu.

Mambo ya kushangaza kuhusu tendo la ndoa duniani

Licha ya kuchangiwa na watu kadhaa, alishawahi kulala maktaba kutokana na kukosa pesa ya kodi ya chumba.

Anasema haikuwa dhamira yake kuomba msaada lakini hofu ya kufutwa chuo kutokana na kukosa fedha imemlazimu afanye hivyo.

"Nimepata bahati ya kuwa katika chuo bora chenye wanafunzi makini na walimu wenye weledi mkubwa...Nimefikia hapa kutokana na msaada wa marafiki na watu nisiowafahamu. Kwa mara nyingine tena naomba msaada wenu," aliandika mtandaoni kabla ya kuanza kuchangiwa.

Mada zinazohusiana