Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 14.11.2018: Dembele, Mata, Herrera, Sanchez, Barella, Cottrell

Ousmane Dembele, 21. Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ousmane Dembele, 21 awindwa na Liverpool

Timu ya Liverpool iko tayari kuvunja rekodi ya klabu yao kwa kutoa Pauni milioni 85 mwezi Januari kwa Barcelona ili kupata saini ya mshambuliaji wa ufaransa Ousmane Dembele, 21. (Sun)

Viungo wa kati wa Manchester United Juan Mata, 30 na Ander Herrera, 29, wote wako tayari kujadili kuhusu kusaini mkataba mpya katika klabu hiyo.Mkataba wa wachezaji hao unatarajia kumalizika mwishoni mwa msimu huu. (Sky Sports)

Image caption Alexis Sanchez, 29

Mchezaji wa mashetani wekundu Alexis Sanchez, 29, ambaye hafurahii kukosa namba anaweza kutafuta namna ya kuondoka mwezi Januari. (Evening Standard)

Haki miliki ya picha Getty Images

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho yuko tayari kuwauza beki wa Eric Bailly, 24 pamoja na mchezaji wa kimataifa wa Argentina Marcos Rojo, 28, ili kuweza kumleta mlinzi wa kati mpya mwezi Januari. (Telegraph - subscription required)

Tottenham inajiandaa kupeleka kiasi cha pauni milioni 35 kwa Cagliari , ili kupata saini ya kinda Nicolo Barella mwenye umri wa miaka 21 anayecheza nafasi ya kiungo wa kati. (Sun)

Image caption Nick Powell, 24

RB Leipzig wako tayari kumsajili kiungo wa klabu ya Wigan Nick Powell, 24 ambaye mkataba wake unamalizika mwezi Januari. (TeamTalk)

Borussia Dortmund na Marseille ,wote wanavutiwa na kiungo wa kati wa Arsenal mwenye umri wa miaka 17 Ben Cottrell. (Sun)

Crystal Palace na Fulham wamevutiwa na kumsajili kwa mkopo mchezaji wa kimataifa wa Uturuki Ozan Tufan, 23 anayeichezea Fenerbahce. (Aksam - in Turkish)

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii