Brexit: Baraza la mawaziri Uingereza laidhinisha rasimu ya makubaliano ya kujitoa katika EU

Theresa May Haki miliki ya picha PA

Baraza la Mawaziri nchini Uingereza hatimaye limeidhinisha rasimu ya mswada wa makubaliano juu ya nchi hiyo kujiondoa katika Umoja wa Ulaya maarufu kama Brexit.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya majadiliano makali yaliyoduymu kwa takriban saa tano,

Bi May amesema kwamba atawasilisha taarifa hiyo leo katika bunge la nchi hiyo, ambapo ataelezea uamuzi wa serikali.

Amekuwa mbioni kutetea mapendekezo ya mkataba baina ya Uingereza na muungano wa ulaya unaohusu masharti ya jinsi Uingereza itakavyoweza kujiondoa katika muungano huo.

Wafuasi wenye msimamo mkali wanaounga mkono Uingereza kujitoa kwenye muungano huo wanadai kuwa mkataba huo ni sawa na kusalimu amri.

Wamekuwa wakitoa wito wa kura kupigwa tena ili kuamua kama Uingereze ijitoe au kusalia kwenye muungano huo.

May pia amesisitiza bungeni kuwa Uingereza itajitoa kwenye muungano wa Ulaya.

Haki miliki ya picha Getty Images

"tuko katika hatua ya mgawanyiko" lakini mchakato wa Brexit,unaendelea na utatoa nafasi ya makubaliano hayo kukamilishwa.

Mpatanishi mkuu wa Umoja wa Ulaya kuhusu masuala ya Brexit Michel Barnier amesema mswada huo wa makubaliano umewasilisha hatua ya maamuzi katika majadiliano, lakini bado kuna kazi ya kufanya.

Lakini Jacob Rees-Mogg mmoja wa viongozi wakuu wanaotaka Uingereza kujiondo kwenye muungano wa EU ameutaja mswada huo kama "mkataba uliyooza".

Mhariri wa BBC wa siasa za Uingereza Laura Kuenssberg amesema ni wazi kuwa baraza la mawaziri ''halikuzungumza kwa kauli moja'' huku mawaziri tisa wakiupinga mkataba huo wazi wazi .

Katika taarifa aliyoitoa nje ya ofisi yake ya Downing Street, Bi May aliafiki kuwa mswada huo uliidhinishwa baada ya "majadiliano ya muda mrefu na maafisa wa EU."

Amesema kuwa ''naamini kuwa mvutano huu ni kwa maslahi ya Uingereza yote", akiongeza kuwa : "Ukiondoa pingapiza utaona wazi suala muhimu lililopo mbele yetu.''

"Mkataba huu unalenga kufanikisha uamuzi uliyofikiwa katika kura ya maoni, ambayo unarudisha usimamizi wa fedha zetu, sheria na mipaka, kukomesha uhuru wa utangamano, kulinda ajira, usalama na umoja wetu; au tuondoke bila makubaliano ama tusiondoke kabisa."

Yaliyomo kwenye rasimu hiyo ya makubaliano ya Uingereza kujitoa katika EU yamechapishwa pamoja na muongozo unaelezea kwa kina uhusiano wa Unchi hiyo na muungano wa ulaya utakavyokua siku zijazo.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Wajumbe wa Uingereza na Umoja wa Ulaya katika mazungumzo ya BREXIT

Ni mambo gani yaliyoangaziwa katika makubaliano hayo?

  • Makubaliano ya kujiondoa yanaangazia masuala ya ''talaka kati ya Uingereza na EU''
  • Inajumuisha kujitolea kwa Uingereza kulinda haki ya raia wa mataifa wanachama wa EU pamoja naraia wa Uingereza wanaoishi EU kuendelea kuendelea kuishi, kufanya kazi na kusoma bila hofu.
  • Kuna muda wa miezi 21 ya mpito utakaotolewa baada ya Uingereza kujitoa EU mwezi Machi mwaka 2019 na unajumuisha makubaliano ya kifedha kutoka Uingereza .
  • Suala lenye utata mkubwa katika mashauriano ya Brexit ni "uwajibikaji", linalo lenga kuhakikisha hakuna vikwazo vipya vya mpaka vinawekwa katika mpaka wa Uingereza na Ireland ikiwa taifa hilo halitakubaliana na makubaliano ya kibiashara kati ya Uingereza na Muungano wa Ulaya.
  • Pande zote mbili zimekubaliana kuwajibikia makubaliano mengine mbadala.

Mambo 3 makuu kuhusu yaliotokea na yanayotarajiwa:

  • Jambo kuu na muhimu - Theresa May amepata makubaliano ya Uingereza kujitoa katika EU yanayoeleza ni lini na vipi watajitoa.
  • Baraza la mawaziri bado limegawanyika kuhusu yaliomo ndani. Inategema unauliza upande upi , 10 walipinga au 10 walielezea wasiwasi lakin hawakuwa na namna ili kuidhinisha rasimu hiyo.
  • Mwisho - Iwapo Theresa May atapata ufanisi katika siku chache zijazo na katika mkutano wa EU Novemba 25 ametupa kionjo cha alichonacho. Mpango wake, hakuna mpango au hakuna Brexit.

Ni nini kita kachofuata?

Theresa May itakabiliwa na maswali magumu bungeni atakapokutana na wabunge siku ya Alhamisi

Huku hayo yakijiri EU imesem "hatua ya mgawanyiko" imefikiwa katika majadiliano.

Hatua hiyo ilihitajika kufikiwa kabla ya kuitisha kikao maalum cha kukubaliana mpango wa kujitoa ikiwezekana mwezi ujao.

Baada ya hapo serikali itakabiliwa na kura nyingine bungeni ambapo wabunge wataombwa kuidhinisha mpango huo.

Uingereza inatarajiwa kujitoa katika muungano wa EU Machi 29 mwaka 2019 - ikiwa makubaliano ya kujiondoa yatatiwa saini ili kutoa fursa ya kuanza rasmi kwa awamu ya mpito

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii