Awer Mabil: Kuanzia kuishi nyumba ya udongo kambi ya wakimbizi hadi kufunga mabao Australia

Awer Mabil Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Awer Mabil aliifungia Australia bao lake la kwanza iliposhinda Kuwait 4-0

Safari ya Awer Mabil ilianzia kwenye nyumba ya matope akiwa mkimbizi na leo hii anatikisa nyavu akiwa mchezaji mpira wa kimataifa.

Mcheza kandanda huyo mwenye miaka 23 alikulia kwenye kambi ya wakimbizi nchini Kenya na mazingira duni yalikuwa ni matatizo ya kila siku kwa familia yake.

Baada ya kuhamia nchini Australia kama sehemu ya programu ya kibinadamu, alikumbwa na ubaguzi wa rangi wakati akijaribu kucheza kandanda.

Lakini ameyapitia mengi na hata kulifungia bao taifa lililompa hifadhi la Australia wakati ikiichakaza Kuwait kwa mabao 4-0 mwezi Oktoba.

Mabil alizaliwa kwenye kambi ya wakimbizi ya Kakuma baada ya wazazi wake kukimbia vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan.

Njaa na mazingira mabaya vilikuwa changamoto mbili za kila siku familia yake ilikumbana nazo.

"Tulijenga nyumba moja ya udongo," anaiambia BBC. "Ambayo ni kama nyumba ya chumba kimoja cha kulala katika nchi za magharibi.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mabil mwaka 2012 na Adelaide United

"Lakini unajua hii si nyumba yako. Tulikuwa wanne - mimi, mama yangu, kaka yangu na dada yangu. Tulipata chakula kutoka Umoja wa Mataifa kila mwezi.

Kila mtu angepata kilo moja ya mchele, kwa hivyo sisi wanne tungepata kilo nne na kilo tatu za maharagwe. Ilikuwa changamoto kwa sababu lazima tungepima.

"Tulikuwa tunapata chakula kimoja kwa siku. Hakukuwa na kitu kama kifunguakinywa na chakula cha mchana."

Masaa mawili ya kutembea kwenda kutazama mpira

Mabil, ambaye ni winga alianza kuicheza kandanda kwenye kambi ya wakimbizi kuanzia akiwa na umri wa miaka mitano akiwa na marafiri zake.

"Nilipenda kucheza kandanda. Ilikuwa njia tu ya kuniweka nje ya matatatizo," anasema. Nilivutiwa sana na klabu ya Manchester United lakini kulikuwa na TV moja, umbali wa saa mbili hivi ukitembea na ulihitajika kulipa dola moja kutazama."

Maisha yake yalibadilika wakati yeye na familia yake waliwasili nchini Austalia.

"Nikasema sasa fursa yangu ndiyo hii - ikiwa nitajitahidi, kila kita kitafanyika na ninawe kufuata ndoto zangu." mambo yalianzia hapo.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mabil (katikati) asherehekea kushinda FFA Cup na Adelaide United mwaka 2014

Ubaguzi wa rangi

Mabadiliko katika maisha ya Mabil hayakuwa yote mema. Kwa mara ya kwanza alikumbwa na ubaguzi - lakini anasema haioni Australia kama nchi ya kibaguzi."

"Nimekabiliana nayo sana," anasema na kuongeza, "Wakati mmoja wakati nikiwa na miaka 16 nilifika nyumbani na mmoja wa majirani zangu akanishambulia."

Kitu cha kwanza nilifanya kilikuwa ni kufunga mlango na kuwaficha ndugu zangu. Nikuwa nazungumza na watu hao huku mlango ukiwa umefungwa. Nilisema; Nenda. Waliendelea kusema: Rudi nchini mwenu."

Licha ya hilo, anasema anajivunia kuiwakilisha nchi hiyo.

"Ninaiwakilisha Australia kwa sababu imenipa mimi na familia nafasi maishani kuwa na fursa ya pili," amesema.

"Siwezi kusema Australia ni nchi ya ubaguzi. Kuna watu walio wabaguzi lakinia ni nchi ya watu wote.

Ni sehemu yangu kwa sababu nimeishi nusu ya maisha yangu huko. Ninaiita nyumbani kwa hivyo ninajaribu kuiwalisha Australia."

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mabil akishangilia bao huko Esbjerg mwaka 2017

Mwaka 2015 aliahamia FC Midtjylland huko Denmark.

Miaka mitatu baadaye bado yuko huko, kama mchezaji wa kimaiafa wa Australia na tarehe 16 Oktoba alifunga bao la kwanza dakika ya 88.

"Majibu yamekuwa mazuri," anasema Mabil ambaye hata alipata ujumbe wa pongezi kutoka kwa mtu aliyekuwa akimunzi, mchezaji wa zamani wa Manchester United, Juventus na West Ham Patrice Evra.

Mabila sasa ana wakfu wake - Barefoot to Boots - na mara kwa mara yeye husafiri kwenda Kakuma.

Mada zinazohusiana