Tumbili aua mtoto nchini India, je unajua ni mnyama hatari

Aua mtoto wa miezi mitatu India Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Tumbili asababisha maafa India

Mtoto wa kiume mwenye umri wa miezi mitatu amefariki dunia baada ya kuporwa kutoka mikononi mwa mama yake na kung'twa na tumbili kaskazini mwa India.

Mama wa mtoto huyo alikuwa akimnyonyesha wakiwa nyumbani kwao katika mji wa Agra wakati tumbili huyo alipoingia nyumbani mwao na kumshika, imeeleza familia ya mtoto huyo.

Tumbili huyo alimg'ata vibaya mtoto huyo akiwa juu ya paa la nyumba ya jirani baada ya wenyeji kumfukuzia mnyama huyo.

Mtoto huyo wa kiume alifia hospitalini kutoakana najeraha alilolipata, wenyeji wanasema kuwa matukio ya tumbili kushambulia watu katika eneo ni ya mara kwa mara.

  1. Hii ndio picha bora ya mwaka 2018
  2. Dereva aliyeruhusu nyani kuendesha basi afutwa kazi India
  3. Nyani azima umeme kwa karibu masaa 6 nchini Zambia

Mjomba wa marehemu , Dhirendra Kumar, ameiambia BBC kuwa familia ya mtoto imehuzunishwa sana kutokana na tukio hilo.

Tumbili wako wengi sana eneo hili .Tunaishi kwa mashaka.tumesha uarifu uongozi wa mahali hapa mara nyingi tu ili watusaidie lakini hakuna lolote lililofanyika mpaka sasa.Mama wa mtoto amevunjika moyo hata kusema hawezi mpaka sasa, "alisema.

Bibi wa mtoto huyo , Pushpa Devi,ametamka kwamba familia yake kamwe haitaweza kusahau tukio hilo na machungu yake kutokana na kumpoteza mtoto wao.

Haki miliki ya picha YOGESH KUMAR SINGH
Image caption Bibi wa marehemu , Pushpa Devi amesema kwamba watu wa eneo lake wanaishi kwa mashaka makubwa kwa kuwahofia tumbili

"Nimepoteza mjukuu wangu. saa machache kabla ya tumbili kushambulia mtoto wetu, nilikuwa nimempakata mikononi mwangu. Mtoto huyo hakupaswa kufa . Watu watajadili tukio hili kwa muda sana na baadaye watasahau tu.Lakini tunapaswa kuukubali ukweli kuwa mtoto wetu amekwenda .

Ajay Kaushal, afisa aliyehusika na kituo cha polisi cha karibu, ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba mtoto alikuwa amejeruhiwa vibaya.Tumbili aliking'ata kichwa cha mtoto huyo na alimdondosha wakati watu walipokuwa wakimfukuza kwa fimbo na wengine kumrushia mawe.

Hili ni tukio la hivi karibuni katika mfululizo wa mashambulizi ya tumbili dhidi ya binaadamu katika eneo hili la Agra,eneo ambalo ni la kihistoria kutokana na kuweko kwa jumba maarufu ulimwenguni la Taj Mahal. Mnamo mwezi Mya, watalii wawili walishambuliwa katika jumba la Taj Mahal.

Miezi miwili kabla, kulitukia tukio la namna hii ambapo mtoto mdogo alishambuliwa na tumbili na anaendelea kupata matibabu hospitali.

Haki miliki ya picha YOGESH KUMAR SINGH
Image caption Tumbili hawa wanaonekana kiila kona ya mitaa ya Agra

Tumbili hawa wanahaha kila mahali kutokana na njaa, hivyo wanakisaka kila mahali, lakini wana tabia ya kupokonya na hata kushambulia vile vile.

Mr Singh alisema tumbili hao wamezidi kuwa wasumbufu na nguvu zaidi kutokana na kuondolewa kwa makazi yao ya asili,ambayo yameharibiwa kutokana na shughuli za kuupanua mji huo.

Baadhi ya mashirika yamekuwa yakitoa wito kuwa tumbili hao kuharibiwa na kutengwa na sheria ya ulinzi wa wanyamapori.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii