Mimba za utotoni Kenya: Serikali yaanzisha uchunguzi

Amina Mohamed akihutubia mkutano wa UN. Haki miliki ya picha AFP

Mjadala umeibuka nchini Kenya kuhusiana na suala la wasichana wadogo wa shule ya msingi kupachikwa mimba.

Mjadala huo ulitokana na kauli iliyotolewa na waziri wa elimu Amina Mohamed, kwamba "Idadi kubwa ya watahiniwa wamejifungua" katika siku tatu za mtihani wa kitaifa wa wanafunzi wa shule ya msingi (KCPE) ambao unafanywa na watoto- waliyo na umri kati ya miaka 13 na 14.

Waziri alisema: "Hali hii ikiendelea kujirudia kila mara mwaka mzima, nchi huenda ikatumbukia katika majanga."

Kitengo cha BBC cha Reality Check kimechunguza baadhi ya data zilizopo kuhusiana na mimba za utotoni ili kubaini ikiwa hali hiyo inaendelea kuongezeka nchini Kenya.

Kitengo hicho kiligundua ujumbe mmoja uliyosambazwa katika mitandao ya kijamii ukidai kuwa wasichana wa shule wamekuwa wakiwanyonyesha watoto wao wakati wa mtihani.

Madai ya uwongo

Ujumbe huo umesambazwa kupitia ukurasa wa makundi kadhaa yaliyo na akaunti ya Facebook. Baadhi ya kurasa hizo zinafuatiliwa na watu zaidi ya 150,000.

Kila ujumbe uliyosambazwa ulitumia picha aina moja - katika kile kinachoonyesha wanawake wadogo wakiwa wamevalia sare za shule za rangi ya samawati na kila mmoja wao amebe mtoto.

Hakuna chochote kinachoonyesha chimbuko la ujumbe huo au taarifa zilizochapishwa.

Hata hivyo utumizi wa picha moja katika kila ujumbe uliyosambazwa uliwachanganya na kuwakasirisha watumiaji wa mitandao ya kijamii.

Lakini matokeo ya hali hii ni yapi- na Je ina athari gani kwa maadili ya kijamii?"

Kuna baadhi ya watu wanatilia shaka ikiwa ujumbe huo ni wa kweli.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Takwimu za serikali zinaashiria viwango vya mimba za utotoni vimepungua

Picha ya awali katika ujumbe huo ilionekana katika taarifa ya mtandao wa shirika la habari la CNN na haikuwa ya kinamama na watoto wakiwa shuleni nchini Kenya.

CNN imethibitisha kuwa picha hiyo ilipigwa nchini Tanzania na ilikuwa ya wanawake wadogo wakiwapeleka watoto wao katka kituo cha mlezi ya mchana.

Picha hiyo hatahivyo imeunganishwa na taarifa gushi zinazodai hali ya mimba za utotoni katika shule za Kenya.

Baadhi ya taarifa zilizochapishwa ziidai kuwa wanafunzi 19 kati ya 30 walikuwa wakinyonyesha watoto wao. Wengine wakiashiria kuwa ni wanafunzi 21 kati ya 30.

Kitengo cha BBC cha Reality Check pia kiligundua kuwa majina ya shule zilizokuwa zikitajwa katika baadhi ya ujumbe huokama vile shule ya upili ya Chabera na Nyanza hazikuwepo.

Ukweli kuhusu mimba za utotoni Kenya

Mjadala wa hivi karibuni kuhusiana na hali halisi ya mimba za utoto nchini Kenya ''uligubikwa na taarifa ghushi kama hii iliyoangaziwa na kitengo cha BBC Reality Check.

Lakini kuna hofu kubwa kuhusiana na suala hili katika jamii za mijini na vijijini.

"Mimba za u totoni sio jambo geni nchini Kenya ," asema Elizabeth Muiruri, kutoka shirika la Save the Children.

"Hata hivyo taarifa za hivi karibuni katika vyombo vya habari kuhusiana na wasichana wadogo wa shule kujifungua wakati wa mtihani ni za kutia hofu."

BBC imefanya mahojiano na waalimu wa shule na maafisa wa afya katika jimbo Kisumu Magharibi mwa Kenya na maeneo yaliyo karibu.

Walio hojiwa walisema kumekuwa na ongezeka la idadi ya mimba za utotoni hali ambayo inajumuisha wasichana wa miaka 15.

Walisema hali hiyo inachangiwa na umasikini na ukosefu wa elimu ya uzazi na usawa wa kijinsia.

Kati ya Julai mwaka 2016 na Juni 2017, wizara ya afya ilirekodi karibu visa 350,000 vya mimba miongoni mwa wasichana wa miaka kati ya 15 na 19.

Idadi hiyo ni ya wanawake wajawazito wanaoenda kliniki kutafuta ya uzazi kabla na baada ya kujifungua.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa ukilinganisha na mwaka 2014 hali ya mimba za utotoni katika maeneo ya tofauti nchini Kenya imepungua.

Haki miliki ya picha AFP

Upungufu huo umetokana na kuimarishwa kwa elimu ya uzazi shuleni.

ambayo imechangia wanafunzi kuwa na ufahamu wa mbini za mpango wa uzazi, asema Fredrick Okwayo mmoja wawashauri wa shirika la UNFPA.

Hata hivyo idadi ya wasichana wanaoshirikishwa katika elimu hiyo bado ni dogo.

Hali inawafanya baadhi ya wathirika wa mimba za utotoni kupoteza nafasi ya kujiendeleza maishani.

Vipi hali ya Kenya iukilinganisha na mataifa mengine?

Kwa mujibu wa ripoti ya Benki ya Dunia nchi kama Nigeria na Tanzania, zimekuwa na viwango vya juu vya mimba za utotoni.

Lakini idadi hiyo imeendelea kupungua katika kipindi cha miaka 30.

Afrika Kusini imetajwa kuwa na idadi ya chini ya mimba za aina hiyo.

Licha ya ukosefu wa ushahidi wa unaoashiria kuongezeka kwa visa vya mimba za utotoni nchini Kenya ukilinganisha na mataifa mengine barani Afrika, serikali imekuwa mbioni kukabiliana na tatizo hilo.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii