Mwandishi wa mapenzi Uchina afungwa jela miaka 10 kwa kitabu cha ngono ya jinsia moja

Person reading book Haki miliki ya picha iStock
Image caption Kitabu hicho kinadaiwa kuwa na "maudhui machafu".

Mwandishi mmoja wa vitabu nchini Uchina amefungwa miaka 10 jela kwa kuandika na kuuza kitabu chenye maudhui ya ngono ya wapenzi wa jinsia moja.

Mwandishi huyo mwanamke afahamikaye kwa jina la Liu, alihukumiwa kifungo hicho na na mahakama ya jimbo la Anhui mwezi uliopita kwa kuuza "maudhui machafu".

Jina la kitabu hicho ni "Occupation", lenye maana ya kazi kwa kiswahili na kimebeba maudhui ya "tabia ya ngono ya wapenzi wa jinsia noja wa kiume...pamoja na aina za kupotosha za ngono na kwenda kinyume na jamii."

Kwa mujibu wa shirika la habari la Beijing News, bi Liu - ambaye anafahamika zaidi mtandaoni kama kama Tian Yi - tayari amaeshakata rufaa dhidi ya adhabu hiyo.

Kutengeneza na kusambaza maudhui ya ngono ni kinyume cha sheria nchini Uchina.

Hukumu hiyo ilitolewa Oktoba 31, lakini habari hiyo imeripotiwa na vyombo vya habari hivi karibuni.

Trump amkingia kifua bin Salman mauaji ya Khashoggi

Polisi waliarifiwa juu ya uwepo wa kitabu hicho baada ya kupata umaarufu mtandaoni.

Bi Liu inasemekana ameshauza nakala zaidi ya 7,000 ya kitabu hicho na vyengine vya ngono na kujipatia yuan 150,000 ambayo ni sawa na $21,604.

Mapenzi ya jinsia moja ruksa India

Hata hivyo kifungo hicho kimezua mjadala mkali kwenye mitandao ya kijamii.

"Miaka 10 jela kwa kitabu tu? Hiyo ni miaka mingi sana," ameandika mtumiaji mmoja wa mtandao wa Weibo.

Mtumiaji mwengine wa mtandao huo akalinganisha uzito wa adhabu hiyo na kesi ya mtumishi wa serikali aliyefungwa miaka nane kwa kumnajisi binti wa miaka minne.

"Wale wanaokutwa na hatia ya ubakaji wanafungwa chini ya miaka 10. Mwandishi anafungwa miaka 10."

Mada zinazohusiana