Mtanzania mwenye ulemavu wa ngozi aliyenusurika kuuawa baada ya mjomba wake kumuuza kwa wauaji kwa milioni mbili

Mtanzania mwenye ulemavu wa ngozi aliyenusurika kuuawa baada ya mjomba wake kumuuza kwa wauaji kwa milioni mbili

Katikati ya ziwa Victoria Barani Afrika, kuna kisiwa cha Ukerewe kaskazini magharibi mwa Tanzania sehemu ambayo ni kimbilio kwa Albino ambao kwa miaka kadhaa wamekua wakitengwa na kuuawa nchini humo.

Kisiwa hicho ni miongoni mwa maeneo machache katika kanda ya ziwa ambayo hajakumbwa na mauaji ama mashambulizi yoyote ya albino.

Kwa mujibu wa chama cha albino Tanzania kumekua na mashambulizi 180 ya albino na 75 kuuawa nchini Tanzania.

Christina alikimbilia Ukerewe baada ya kunusurika kuuawa kufuatia jaribio la kuuzwa kwa wauaji na mjomba yake.

Video: Eagan Salla, BBC