Baadhi ya watu wameanza kunywa mikojo yao wakiamini kuwa ni tiba

mkojo Haki miliki ya picha ISTOCK

Mtu kufikia hatua ya kunywa mkojo wake mwenyewe ni jambo ambalo anaweza kulifanya kama amekwama mlimani au jangwani na hana chakula chochote.

Lakini siku hizi baadhi ya watu wameanza kunywa mikojo yao wakiwa majumbani kwao tu.

Kwa mfano Kayleigh Oakley mwenye umri wa miaka 33, ambaye ni mwalimu wa yoga kutoka Newington, anadai kwamba anakunywa mkojo wake mwenyewe kwa sababu umemsaidia kupona baadhi ya maradhi ambayo yalikuwa yanamsumbua kwa muda mrefu.

Kayleigh aliwaambia waandishi wa habari kwamba alianza kunywa mkojo wake mwenyewe miaka miwili iliyopita.

"Nilisikia kwamba mkojo unaweza kusaidia kuweka upya mfumo wa kinga, kumfanya mtu kuwa na afya njema na ngozi iwe na muonekano mzuri", alisema mwalimu huyo wa yoga.

Na kwa sasa hanywi tu jagi lililojaa mkojo wake kila siku, lakini pia huwa anajipakaza usoni kwa madai kuwa anatunza ngozi yake.

Kinachoshangaza zaidi, sio Kayleigh peke yake ambaye anasifia matumizi yake ya mkojo kwa siku za hivi karibuni.

Wiki iliyopita Leah Sampson, mwanamke mwenye miaka 46 kutoka Alberta, Canada aliliambia gazeti la The Sun kuwa kunywa mkojo wake mwenyewe kumemsaidia kupunguza nusu ya uzito wa mwili wake.

Leah alisema kwamba alikuwa na uzito wa kilo 120 na alipata msongo wa mawazo wa namna anaweza kuupunguza na hivyo hali hiyo ilimpelekea kuwaza kama mkojo utamsaidia.

"Rafiki yangu alinitumia video ya YouTube ikionesha namna ambavyo mkojo ni tiba.

Siku moja nlisimama na kukojoa katika mikono yangu na kuunywa", Leah alisema..

Kwa sasa hanywi tu huo mkojo bali anautumia kusukutua mdogo asubuhi wakati akipiga mswaki na kunyunizia katika macho yake.

Pamoja na kwmba watu wengi wameamini kuwa ni tiba akini ikumbukwe kuwa wataalam wa afya hawashauri watu kutumia njia hii.

Lakini jambo hilo halikumzuia Faith Canter mwenye umri wa miaka 39 ambaye alibainisha kwamba alianza kunywa mkojo wake ili umsaidie kutibu majeraha aliyopata baada ya kuumwa na mdudu.

Faith alianza kunywa mkojo wake baada ya kupata mzio wa kuumwa na mbu na kusababisha jicho lake kuvimba .

Mara ya kwanza nlijisikia sikupenda kuutumia lakini nilipona ndani ya siku tatu tu.

"Niliendelea kunywa mkojo wangu kila siku asubuhi tangu siku hiyo na sijawahi kudhulika tena, Faith aliongeza.

Kuna video ambayo ilisambaa sana katika mtandao wa Facebook mwezi juni ikimuonesha mwanamke mmoja ambaye alikuwa anakunywa mkojo wa mbwa wake.

Haki miliki ya picha ISTOCK

Katika video hiyo ilionesha jinsi alivyokuwa anatembea na mbwa wake, kisha walisimama kukinga mkojo wa mbwa huyo kwenye kikombe. Na kamera hiyo ilionyesha namna mwanamke huyo alivyokuwa anakunywa.

Baada ya kumaliza kunywa mkojo wa mbwa wake, mwanamke huyo alidai kwamba alikuwa na huzuni na ngozi yake ilikuwa haivutii.

Kwa sasa, licha ya kuwa watu wengi kuona kuwa chumvi nyingi iliyopo kwenye mkojo ni dawa lakini bado madaktari wanasema sio vizuri kiafya.

Sababu ya kwanza ya msingi ni kwamba mkojo ni bidhaa taka, hii inamaanisha kwamba ni uchafu unaotokana na chakula na mchanganyiko wa maji ambao tayari umeshafanya kazi mwilini na kinachotoka ni uchafu.

"Watu wengi wana amini kuwa mkojo ni salama, kama mtu hana matatizo yeyote ya kiafya.

Ambapo ukikaa ndani ya mwili wa binadamu unaweza kusababisha aina ya bakteria na bakteria hao wanaweza kumfanya mtu asijisikie vizuri na kupelekea kupata madhara makubwa" Dr Zubair Ahmed aliiambia BBC.

Ukiachia mbali madhara ambayo mtu anaweza kuyapata Dr Ahmed aliongeza kusema kuwa hakuna ushaidi wa kitibabu ambao unaonyesha kwamba mkojo una faida kiafya kwa namna yeyote ile.

"Mkojo ni moja ya njia ambayo inasaidia mwili kutoa sumu mwilini", alieleza.

"Hakuna ushaidi wowote unaoeleza faida za mkojo kiafya.

Wakati ukinywa hata kiwango kidogo cha mkojo unaweza kuhatarisha afya yako, hakuna ushaidi wa kitaaluma unaoshauri watu wanywe mkojo kwa manufaa ya afya yao".

Na Dkt. Andrew Thornber alionya hatari ya kurudisha uchafu katika mfumo wa mwili kwa kunywa mkojo.

"Kazi kubwa ya mkojo ni kusaidia figo kufanya kazi baada ya kuchuja damu na kuuondoa kimiminika chochote na chumvi pamoja na madini", aliongeza.

Mkojo kwa mwanadamu ambaye ana afya njema umetengenezwa na maji kwa asilimia 95 lakini uchafu mwingine ni asilimia tano ambao unakuwa mwingi kupitiliza katika mwili na unaweza kusababisha madhara makubwa.

Wakati huohuo , Dr Thornberaliongeza kuwa unywaji wa mkojo unaweza kusababisha matatizo katika figo.

"Baadhi ya watu wanadhani kwamba mtu akinywa mkojo utamfanya apate vitamin kwa haraka ingawa kuna kuna njia nyingine nyingi ambazo zinaweza kumsaidia mtu kuwa na afya nzuri".

Sio tu madaktari ndio wameonya juu ya matumizi hayo ya mkojo lakini hata wataalam wengine wa afya wamepinga unywaji wa mkojo.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii