Ndani ya Hospitali ya kwanza ya Tembo India
Huwezi kusikiliza tena

Hospitali maalum na ya kwanza ya kuwatibu Tembo nchini India

India imefungua hospitali maalum inayonuiwa kuwatibu Tembo waliookolewa kutoka vizuzini na wengine waliojeruhiwa katika ajali.

Hospitali hiyo ina vifaa vya hali ya juu kama vile mashine za X- Ray.

Tembo au Ndovu nchini India ambao kwa sasa wamesalia takriban 25,000 misituni, ni viumbe vilivyo katika hatari ya kupotea.