Nedim Yasar: Jambazi sugu auawa baada ya kustaafu na kuandika kitabu Denmark

Nedim Yasar, a former gang member who was fatally shot a day before the launch of his memoir on leaving a life of crime, 3 February 2017 Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Nedim Yasar alibadili na kuwa mshauri bada ya kuacha maisha ya ujambazi

Aliyekuwa wakati mmoja kiongozi wa kundi la wahalifu ambaye aliandika kitabu kuhusu jinsi aliishi maisha yake, ameuawa kwa kupigwa risasi siku moja kabla ya kutolewa kitabu chake.

Nedim Yasar, 31, alipigwa rasasi wakati akitoka kuzindua kitabu hicho siku ya Jumatatu kwenye mji mkuu wa Copenhagen.

Yasar alipelekwa hospitalini lakini akafariki kutokana na majeraha. Kitabu chake kilichapishwa siku ya Jumanne.

Awali alikuwa amesema kulikuwa na njama ya kumuua mwaka uliopita.

Katika kisa hicho cha siku ya Jumatatu mtu ambaye alikuwa amevaa vazi leusi alimfyatulia Yasar takriban risasi mbili kwa mujibu wa polisi wa Copenhagen.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Eneo la mkasa mjini Copenhagen

Yasar, ambaye alizaliwa nchini Uturuki na kuwasili Denmark akiwa na umri wa miaka minne, alikuwa kiongozi wa genge la wahalifu la mjini Copenhagen, Los Guerreros, kundi sugu lenye uhusiano na biashara za dawa za kulevya kwa mujibu wa polisi.

Alihama genge hilo mwaka 2012 na kujiunga na mpango wa kubadili tabia baada ya kugundua kuwa angekuwa baba kulingana na shirika la habari la Ritzau.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kitabu cha Yasar kilitolewa Jumanne

Kisha akawa mshauri wa vijana na kujitengenezea jina kwa kuandaa kipindi kwenye kituo cha radio cha Radio24syv.

Kufuatia kufichuka taarifa za kuuliwa kwa Yasar, Radio hiyo ilichapisha picha ya ofisi yake ikiwa na bendera ya Denmark nusu mlingoti.

Kitabu cha Yasar, Roots: Kujitoa maisha ya ujambazi, kimeandikwa na Marie-Louise Toksvig na kinaelezea safari ya Yasar anapojitoa kutoka maisha ya uhalifu.

Waziri wa sheria nchini Denmark, Søren Pape Poulsen, alitaja kifo cha Yasar siku Jumanne kama husuni na kitu kisicho na maana yoyote.

Mada zinazohusiana