Mauaji ya Khashoggi: Chama cha Republican na Democratic wataka uchunguzi wa mauaji hayo urudiwe

TRUMP na MBS Haki miliki ya picha ANDAR ALGALOUD / SAUDI KINGDOM COUNCIL / HANDOUT
Image caption Mwanamfalme Mohammed Bin Salman wa Saudi Arabia na Rais Trump wa Marekani

Rais Trump ametakiwa kuthibitisha kama mwanamfalme wa Saudi Mohammed bin Salman hajahusika kwa namna yeyote katika mauji ya Jamal Khashoggi.

Viongozi wa chama cha Republican na Democratic kutoka katika kamati ya masuala ya uhusiano wa kimataifa tayari wametuma barua wakitaka kesi hiyo ifanyiwe uchunguzi mwingine.

Awali rais Trump alitetea uhusiano uliopo kati ya Marekani na Saudi Arabia licha ya taifa hilo kulaumiwa kimataifa dhidi ya mauaji hayo.

Rais wa marekani Donald Trump ametetea uhusiano wa karibu uliopo kati ya Marekani na Saudi Arabia bila kujali lawama juu ya mauaji ya mwanahabari Jamal Khashoogi yanayoiandama Saud Arabia.

Trump amesisitiza kuwa huenda mwanamfalme Mohamed Bin Salman alijua kuhusu mauaji lakini uhusiano uliopo ni baina yake na Saud Arabia na hawezi kuupoteza.

Rais huyo wa nchi yenye nguvu zaidi duniani amewaambia waandishi wa habari kuwa asingependa kuharibu uchumi wa dunia kwa kuwa na mahausiano mabaya na Saud Arabia.

''Siwezi kuwambia nchi inayotumia pesa zake nyingi na imenisaidia kitu kimoja kikubwa sana, bei ya mafuta, sasa imetulia haipandi wala kushuka, hivyo siwezi kuharibu uchumi wa dunia kwa kuanza kuwa na uhusiano mbaya na Saud Arabia, siwezi kuharibu uchumi wa dunia na uchumi wa nchi yetu''.

Image caption Khashoggi alikuwa mkosoaji kinara wa sera za Saudia hasa zile za mwanamfalme bin Salman

Trump ameongeza pia, kuvunja uhusiano na Saud Arabia ni sawa na kuachia pesa nyingi ziende kwa mataifa mengine kama Urusi na China.

''Ni marekani kwanza kwangu mimi, hatuwezi kuachia mabilioni ya pesa yaende kwa Urusi na China, na watu wengine wazipate, ni kuhusu mimi , ni rahisi tuu, marekani kwanza, na tukivunja huu uhuasiano mtaona bei za mafuta zitakavyopanda, sasa hivi nimeziweka chini, na wamenisaidia kufanya hivyo , na ningependa bei ishuke zaidi.''

Kuhusu mwanamfalme bin Salman kuhusika na mauaji , trump amesema inawezekana Bin Salman alikua akijua kuhusu tukio hilo ama asiwe ana taarifa yoyote.

Uchunguzi wa shirika la kijasusi la nchi hiyo CIA ulioripotiwa na vyombo vya habari vya Marekani unaonesha kuwa uwezekano ni mkubwa kuwa bin Salman aliidhinisha mauaji ya Khashoggi.

Lakini Trump anasema uchunguzi huo haujakamilika kwa asilimia 100.

Khashoggi aliuawa ndani ya ofisi za ubalozi wa Saudia mjini Istanbul Uturuki alipoenda kuchukua nyaraka kuhusu talaka yake na aliyekuwa mkewe nchini Saudia.

Khashoggi alikuwa mkosoaji kinara wa sera za Saudia hasa zile za bin Salman na alikimbilia uhamishoni Marekani mwaka 2017 akihofia usalama wake.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption CIA imesema kuna uwezekano mkubwa kuwa mwanamfalme bin Salman alijua kuhusu mipango ya mauaji ya Khashoggi

Kwa upande wa Saud Arabia wamekuwa wakikanusha uhusika wa Bin Salman katika tukio hilo.

Awali walikanusha kabisa kutokea kwa mauaji hayo lakini baada ya kubanwa walikiri na kulaumu oeresheni haramu iliyofanywa na maaisa usalama wa nchi hiyo.

Kauli ya Trump inawapa nafuu viongozi wa Saudia ambao wamekuwa wakipitia wakati mgumu kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa kutokana na mauaji hayo.

Bado mwili wa mwanahabari huyo haujapatikana na inaaminika.

Hata hivyo, wakosoaji wa Trump wameshtushwa na kauli yake ya kuitetea Saudia.

Katika maelezo yake, Trump aliisifia Saudia kuwa mshirika imara katika kuibana Iran katika programu yake ya matumizi ya teknolojia ya nyuklia.

Maelezo hayo ya Marekani yamepingwa vikali na Waziri wa Mambo ya Nje ya Iran Javad Zarifambaye amesema ni ajabu kuona Trump anatumia jina la Iran katika utetezi wa tukio hilo, "Itakuwa Iran pia imesababisha moto wa nyika unaoendelea California. Maana sasa kwenye kila shida inayoikumba Marekani, Iran tunahusishwa."

Maelezo ya Trump yanasemaje?

"Dunia ni mahali hatari sana" Trump alisema hayo kabla Saudi Arabia haijaanza kushirikiana na Marekani dhidi ya Iran.

Mamlaka ya ufalme imepoteza mabilioni ya dola katika kupambana na ugaidi dhidi ya waislamu wenye itikadi kali, Huku Iran ikiwa imeuwa wamarekani wengi wasiokuwa na hatia katika mashariki ya kati.

Maelezo yake yamesisitiza kuwa Saudi imewekeza sana katika hilo na kama mikataba ikifutwa bila kuzingatia mchango wake basi watakaofaidika ni Urusi na China.

Pamoja na kwamba rais Trump alikiri kuwa mauaji ya Jamal Khashoggi yalikuwa ya kinyama, lakini alidai kuwa inawezekana hakuna ushaidi wote kuhusu mauaji yake.

Trump amesema kwamba atakutana na Mohammed bin Salman katika mkutano wa G20 wiki ijayo kama mwanamfalme huyo atahudhuria.

Mada zinazohusiana