Wasiwasi wa mizimu unavyozua mjadala kuhusu uchomaji wa maiti Zimbabwe

maiti Haki miliki ya picha Getty Images

Uchomaji wa maiti umeleta mjadala mkubwa nchini Zimbabwe, na kutaka mila na desturi pamoja na imani za kidini kuzingatiwa.

"Kwa kuwa tumeumbwa kwa mavumbi na mavumbini tutarejea'', mstari huu kutoka kwenye Biblia unaleta uzito kidogo kwa waumini wengi wa kikristo nchini Zimbabwe ambao wanapinga utaratibu wa kuchoma maiti.

Wanafikiri kwamba ni bora kuzika kawaida na wanahisi kwamba mwili utarejelea kwenye mavumbi kiasilia tu badala ya kuuharakisha kuurudisha mavumbini kwa kuuchoma.

Uchomaji wa maiti huwa unatumia joto linalokadiriwa kufika nyuzi joto 500 mpaka nyuzi joto 800.

Huwa inategemea na maamuzi ya familia yenyewe kuamua watayafanyia nini majivu ambayo wameyapata baada ya kuuchoma.

Mjadala huo unaendelea kuchukua vichwa vya habari katika mji wa Bulawayo,ambao ni wapili kwa ukubwa nchini Zimbabwe na kwao ni lazima kwa maiti kuchomwa kwa wale ambao wanakufa wakiwa na miaka 25 kushuka chini.

Mapendekezo hayo yalikuja zaidi ya mwaka mmoja tangu halmashauri iliposema kwamba watoto wenye umri wa miaka 10 na walio chini ya hapo inabidi wachomwe ili kusaidia kuondoa changamoto inayowakabili watu wa mipango miji.

Ongezeko la watu katika maeneo ya miji nchini Zimbabwe unasababisha maeneo ya kuzika kukosekana.

Madiwani wameweka mipaka katika jambo hilo na wanahisi kwamba kuchoma maiti ndio suluhisho.

Eneo moja kati ya maeneo sita ya makaburi yameripotiwa kuwa na nafasi ya kuwa na makaburi 200.

Na katika mji mkuu pia wanakabiliwa na tatizo hilohilo.

Haki miliki ya picha Getty Images

Kuna watu wanaopinga kile ambacho kimeandikwa kwenye biblia kuhusu kuchoma maiti lakini upinzani mkubwa kuhusu kuchoma maiti unaonekana kuanza kutoka kwenye ibada za mazishi ya jadi.

Kunyunyiza pombe kunahitajika kwenye makaburi

Wanaharakati wa mila na desturi wanasema kwamba kuchoma maiti hakuwasilishi tamaduni ya dini za Afrika.

Watu waliokufa ni muongozo na wanauzito mkubwa katika walio hai.

Hivyo wanahitajika kuheshimiwa na heshima yao inapatikana kwa kujengewa kaburi ambalo litaangaliwa vizuri.

Kuna utamaduni ambao huwa unafanyika katika makaburi ambapo wanajumuisha kunyunyizia pombe ili kuwaomba radhi mababu.

Katika majivu ambayo sio ardhi ya mwanadamu itakuwa ngumu kufanya matambiko ya namna hiyo.

Roho za waliokufa na wanaoishi huwa zinawasiliana na huwa ni vigumu kutenganisha.

Kuchoma mwili wa binadamu kunasitisha uhusiano huo na kunaleta huzuni zaidi.Na wengi wanaona kuwa huo ni utamaduni wa kigeni.

Marehemu Gordon Chavunduka, aliyekuwa mkuu wa chuo kikuu cha Zimbabwe alisema miaka 20 iliyopita na maneno hayo bado yanakumbukwa na baadhi ya watu:

Falsafa ya waliokufa katika utamaduni wa jamii ya washona barani Afrika inasema kwamba inachukua mwaka kwa roho ya marehemu kuuacha mwili wake na kujumuika na mababu wa kale.

"Kama mwili umechomwa , basi roho yake itakuwa kama imefungwa. Ingawa itabaki kuwa hai. Na utaratibu wa mazishi ya kimila ukienda tofauti wanafamilia au jamii husika wataadhibiwa."

Majeneza ya kushangaza nchini Ghana

Hii pia inaeleza namna ambavyo mamlaka wamefikiria kwa umakini katika kushauri kuwa wale waliokufa katika umri mdogo ndio watakaochomwa kwa sababu hawana kumbukumbu za muda mrefu ambazo zitahitaji mila za jadi kutumika.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Nchini Ghana, hali kuhusu maiti huwa tofauti

Diwani aliwaondoa watu wazima kuanzia miaka 25 ambao wana uwezekano mkubwa wa kuwa na watoto ambao waliwaacha na wanaendelea kuwaangalia kiroho.

'Uoga wa wachawi'

Bado kwenye upande wa utamaduni , kuna wale ambao wanakubali maiti kuchomwa wakiwa na sababu kadhaa.

Eneo moja la makazi mjini Harare, kulikaririwa kuwa ni njia nzuri ya kumuokoa mtu na wachawi na mizimu, ambao baadhi uamini kuwa labda hawakufa na walichukuliwa na wachawi.

Wanamazingira wamesema kuwa kuchoma maiti ni afadhali kwa sababu sanduku la kuwekea maiti yanadaiwa kupuliziwa kemikali hatari ambayo inaweza kuathiri mfumo wa maji.

Lakini mwisho wa siku , kama kitu chochote kitaweza kusisitiza watu watoke kwenye utaratibu wa kuzika na waje kwenye kuchoma maiti nchini Zimbabwe, gharama ni kitu ambacho kinazingatiwa.

Watu wengi huwa wanahangaika kupata kipato cha kuishi kutokana na hali ya uchumi na huku wanahanaika kupata fedha ya kfanya mazishi.

Inagharimu dola 63 kuchoma maiti wakati kuzika ni dola 1000.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii