Mchezaji wa raga mpenzi wa jinsia moja Kenneth Macharia apewa hifadhi ya muda Uingereza

Kenneth Macharia, member of Bristol Bisons RFC Haki miliki ya picha Phillip Rogerson
Image caption Kenneth Macharia

Mcheza raga mpenzi wa jinsia moja amepewa hifadhi ya muda licha ya awali kuripotiwa kuwa angesafirishwa kutoka Uingereza.

Mchezaji huyo wa timu ya Bristol Bisons Keneth Macharia alisema ikiwa ombi lake ya kuomba hifadhi litakataliwa na arudishwe Kenya anaweza kunyanyaswa.

Mbunge wake James Heappey alithibitisha kuwa hatua ya kurudishwa Kenya imefutwa lakini akasema Bw Macharia bado ana kazi kubwa ya kufanya na wakili wake.

Ofisi ya mambo ya ndani ilisema haitazungumzia mambo ya kibinafsi.

"Kwa kweli hizi ni habari njema na hawezi kuwekwa kwenye ndege hivi karibuni," mbunge wa Conservative

"Wakili wa Ken anastahili kuelewa hasa ni kitu gani kilisababisha kufutwa uamuzi."

Vitendo vya mapenzi ya jinsia moja ni haramu nchini Kenya na adhabu yake ni kifungo cha miaka 14 jela.

Bw Macharia amekuwa akizuiliwa kwenye kituo cha uhamiaji cha Colbrook, karibu na uwanja wa Heathrow.

Zaidi ya watu 68,000 wameweka sahihi shinikizo kuzuia asifukuzwe na kutaka apewe hifadhi.

Mada zinazohusiana