Je 'miji ya kikoloni' Afrika inaweza kusitisha uhamiaji Ulaya?

wahamiaji wa Afrika Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waafrika wengi huwa wanahatarisha maisha yao kwa kuvuka bahari ya Mediterania

Mapendekezo ambayo yanatatanisha yaliyotolewa na waziri wa Ujerumani kwamba mataifa ya kigeni yanaweza kumiliki ardhi barani Afrika ili kuzuia uhamiaji, umepingwa na Umoja wa Afrika(AU).

Umoja wa ulaya au taasisi kama ya benki ya dunia wanapaswa kujiimarisha kwa kujenga miji barani Afrika ili kuweza kusaidia upatikanaji wa ajira na kuliendeleza bara.

Waziri wa Ujerumani katika nchi za Afrika, Gunter Nooke,aliiambia BBC kwamba alipendekeza hayo kutokana na ongezeko kubwa la uhamiaji kutoka Afrika mpaka ulaya.

"Kama mataifa ya Afrika yataweza kuruhusu ardhi yao itumike kwa taasisi kubwa za kigeni ili kuwezesha bara hilo kuendelea kwa miaka 50", Nooke alisema.

Ni wazo ambalo linatatanisha , limekosolewa na kukataliwa kwa kudaiwa kuwa ni ukoloni.

Lakini wengine kama Carol Musyoka, mhadhiri wa chuo kikuu kimoja kikubwa nchini Kenya anaunga mkono wazo hilo.

BBC ilimuhoji bi.Musyoka na kuelezea kuwa wazo hilo linavutia na yuko tayari kuliunga mkono kama litalenga kuhakikisha kuwa waafrika wananufaika.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mji wa Lagos unatarajiwa kuwa na watu milioni 30 ifikapo mwaka 2050 na itawawia vigumu watu kupata ajira

Mchumi kutoka Marekani ambaye ni mshindi wa Nobel Prize, Paul Romer alitoa wazo hilo muongo mmoja uliopita.

Mwaka 2009, Nchi zinazoendelea zinapaswa kufikiria kutoa sehemu ya eneo lake kwa mataifa ya kigeni ambayo yataweza kujenga miji ya mikataba kwa ajili ya kukuza uchumi .

Aliongeza kudai kuwa miji hiyo itaendeshwa na sheria tofauti na nchi husika.

'Hong Kong ya Marekani ya kati'

Mwaka 2008 , wakati huo rais wa Madagascar Marc Ravalomanan alieleza namna ambavyo anavutiwa kutumia mpango huo katika visiwa vya bahari ya India,

Alisema miji kama hiyo miwili itajengwa eneo ambalo wananchi na wahamiaji kutoka mataifa ya jirani wanaweza kuishi.

Upande wa upizani ulimshutumu bwana Ravalomanana na kuandaa maandamano ambayo yaliua wazo hilo na kusababisha kuondolewa madarakani mwaka 2009.

Hondura aliyekuwa rais wa Porfirio Lobo Sosa , yeye pia aliliunga mkono wazo hilo , kwa kusema mwaka 2011 miji hiyo maalum ya mkataba inaweza kuboresha mamia ya maisha ya watu kwa kutoa ajira zenye ushindani, huduma nzuri za afya na elimu na mfumo mzuri wa kisheria na usalama.

Gazeti moja kutoka Honduran La Prensa liliandika kuwa ni wakati sasa wa kuweka mipango ya kuifanya nchi yao ifanane kama Hong Kong ya Marekani ya kati.

Bwana Sosa alishindwa kutekeleza, baada ya kukosolewa vikali na wapinzani wake.

Barani ulaya , uhamiaji ni hatari katika masuala ya kisiasa nchini Marekani na wahonduran wengi ni wahamiaji katika mpaka wa Marekani.

Serikali ya sasa ya wahonduran wana matumaini ya kubuni kitu kinachoitwa ukanda maalum wa uchumi ili kukuza maendeleo.

Ingawa bado hawajaainisha mipango yao ni ipi, inasemekana kuwa mpango huo wa kukuza uchumi unaweza kuwa chini ya sheria za kigeni na kuwavutia wawekezaji wa kigeni.

"Tunaamini kuwa haya maeneo yatakayowekwa kwa ajili ya kukuza uchumi itaweza kutekelezeka na watu wataona matokeo yake chanya katika upande wa kutoa ajira na wanasiasa kutoka miji yote watahitaji mpango huo", waziri wa uchumi Arnaldo Castillo aliiambia BBC.

' Wazo ambalo halina msingi '

Uzito mkubwa upo kwa wanaopinga wazo hilo, mamia ya watu masikini wanaoishi Honduran wanaamini kwamba mpango wa kuanzisha eneo maalum katika kuwekeza kiuchumi itaweza kuifanya jamii kuishi katika kanuni tofauti na maeneo mengine ya nchi.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Maelfu ya watu wamekuwa wakiikimbia nchi yao kwa nia ya kutafuta maisha mazuri Marekani.

Romer aliongea kwenye mdahalo wa TED mwaka 2011 uliokuwa ukijadili namna ambavyo wageni wanaweza kuiongoza miji kisasa na kutoa huduma bora na kuwafanya watu waache kuhama katika nchi zao kwa sababu za kiuchumi.

Wazo kama hilo limefanya kazi katika mji wa Hong Kong .Walihoji namna ambavyo eneo la China lilivyoweza kukuza uchumi wake wakati ilipokuwa chini ya utawala wa Uingereza mwaka 1841 mpaka 1997.Nooke anaona kuwa miji iliyojikita kibiashara inaweza kutoa elimu kwa vijana wa Afrika.

Wazo lenyewe ni kuwa miji hii huru inaweza kuleta maendeleo na mafanikio.

Hatahivyo , wengine walitoa angalizo kuwa mpango huo unaweza usifanye kazi.

"Kutengeneza miji maalum ya uchumi ni wazo ambalo haliingii akilini", Ken Opalo kutoka chuo kikuu cha Georgetown cha nchini Marekani.

Miji kama hiyo utaongeza uhamiaji ndani ya nchi na hautaweza kunufaisha au kutatua tatizo ka mataifa ya Afrika.

Hata kama miji hiyo haijaendelea au inakabiliana na rushwa, itakuwa vyema kama jitihada zitafanywa na taasisi za nchini mwao, Opalo aliongeza kuwa njia nzuri ambayo itasaidia bara hillo ni kuwekeza katika kiwango kidogo na cha kati cha biashara ili kuweza kutoa ajira.

Mkurugenzi wa mawasiliano wa Umoja wa Afrika ,Leslie Richer amelikataa wazo hilo la wageni kuongoza miji na kusema kuwa haliwezi kutekelezeka na hilo ni jibu la kivivu katika kukabiliana na uhamiaji .

Wazo hilo linamaanisha kuwa Afrika inapaswa kuwaachia wadhifa taasisi za kigeni.

'Ukoloni wa hiari'

Mpango wa Umoja wa Afrika wa Agenda ya 2063 umepinga wazo hilo.

"Afrika yenyewe inaweza ikaleta miujiza katika bara lake, Kwa kuimarisha ukuaji wa uchumi katika bara hilo kwa kuwa na umoja na siasa na uchumi imara", Umoja wa afrika upo kwa ajili ya kujenga maendeleo ya Afrika Raila Odinga,

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Hong Kong ni miongoni mwa miji ghali zaidi duniani

Lakini Nooke alieleza kuwa wazo hilo la wageni kuongoza miji , ikimaanisha kuwa hiyo itakuwa njia ambayo itawezesha migogoro kuzuiliwa baina ya Umoja wa Ulaya na serikali za Afrika.

Bi.Musyoka ni miongoni mwa waafrika wenye matumaini kuwa miji itaweza kujengwa na kukubalika kwa ukoloni wa hiari kwa sababu serkali nyingi za Afrika kutoa maisha bora kwa raia wake.

Mawazo yake yanazika jitihada za waasisi wa bara la Afrika kutaka kuwa huru, lakini kwa upande wa vijana wa Afrika kuhatarisha maisha yao ili kufika ulaya kwa sababu ya umasikini, uchumi na uongozi mbovu.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii