Patrice Evra avunja rekodi kwa vituko

Patrice Evra akimbusu kuku mbichi Haki miliki ya picha Twitter
Image caption Patrice Evra akimbusu kuku mbichi

Kinachotakwa kusemwa ni kitu ambacho kipo wazi tu, lakini wakuu wanalazimu kusemwa...

Usilambe, usibusu au kula kuku mbichi...

Sawa…lakini sasa suala hilo liko nje ya muongozo, tunaweza kumuongelea Patrice Evra tu na ujumbe wake wa hivi karibuni katika ukurasa wa Instagram.

Mlinzi wa zamani wa Manchester United na West Ham ambaye anajulikana zaidi kwa kuweka picha zisizo za kawaida.

Hivyo hakuna kitu ambacho kinaweza kushtusha kutoka kwake - lakini kama hujaona bado tunashauri kuwa usiwe unakula au kunywa wakati unaangalia picha hizo.

Video hiyo inaonyesha Evra akiwa amejirikodi mwenyewe huku amemshika na kumpapasa kuku mbichi.

Na maelezo yake ya video hiyo yaliandikwa: "Ninajua kuwa ni kesho lakini ni kwa waliolengwa, #ninaupendamchezohuu,Tunapaswa kushukuru kila siku."

Hii ni mara tano bingwa wa mashindano ya magari ya Formula 1, Lewis Hamilton alifikiri kwamba mchezaji huyo wa zamani wa Ufaransa amefika kiwango kingine katika kupambanua vitu ambavyo havieleweki.

"Siwezi kudanganya, hii inashangaza,"Hamilton alieleza.

Na hakuwa peke yake aliyedhani kwamba vitendo hivyo alivyofanya raia wa Ufaransa havieleweki…hebu angalia?

Evra aliafuatiliza ujumbe wake wa awali wa video katika mtandao wa kijamii wa Instagram kwa kusema,

"Furahia maisha-acheni kujisononesha. Na watu wote ambao hawali nyama , huwa silalamiki chochote mnapokuwa mnakula majani yote kwenye bustani yangu!"

Aliendelea: "Yaacheni majani kwa ajili ya ng'ombe-wanahitaji kula pia!"

Naaaaaaaa hii inatosha kwa leo…

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii