Mtanzania akamatwa akiwa ameficha mihadarati njia ya kwenda haja kubwa uwanja wa JKIA Kenya

Msafiri Musa bado yuko chini ya uangalizi wa polisi JKIA Haki miliki ya picha @DCI_Kenya/Twitter
Image caption Msafiri Musa bado yuko chini ya uangalizi wa polisi JKIA

Raia wa Tanzania ni miongoni mwa raia wa nchi za nje ambao wanazuiliwa nchini Kenya baada ya kukamatwa akiwa ameficha mihadarati kwenye njia yake ya kwenda haja kubwa (rektamu).

Walikuwa safarini kuelekea China na India walipokamatwa Alhamisi usiku katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Jomo Kenyatta.

Mtanzania huyo ambaye ametambuliwa na idara ya uchunguzi wa jinai nchini Kenya kama Msafiri Musa alitoa tembe 47 za dawa za kulevya mara ya kwanza.

Aliwekwa chini ya uangalizi ambapo baadaye alitoa tembe nyingine 69.

Polisi hawajasema raia wa mataifa hayo mengine ni kina nani.

"Wachunguzi wa jinai wamewasilisha maombi katika mahakama ya JKIA kumzuilia zaidi ili kuwawezesha kukamilisha uchunguzi. Washukiwa bado wanaendelea kuangaliwa kwa makini," idara ya uchunguzi wa jinai Kenya imesema kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii