Chelsea Clinton: 'Hakuna aliyemwambia baba abadili jina lake'

Chelsea Clinton Haki miliki ya picha Chelsea Clinton
Image caption Chelsea Clinton ameandika vitabu viwili vya watoto

Chelsea Clinton amesema kwamba matarajio ya umma kwa mama yake yalikuwa tofauti sana ukilinganisha na matarajio waliokuwa nayo kwa baba yake.

Mtoto wa rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton na aliyekuwa mgombea wa urais Hillary Clinton, alizungumza na BBC mara baada ya kutajwa katika wanawake 100 wa BBC.

"Matarajio ya watu kutoka nje ya familia yetu yalikuwa tofauti sana kwa mama yangu ukilinganisha na baba yangu, kwa mfano hakuna mtu aliyemtaka baba abadilishe jina."

Bi.Clinton alisema kwamba baba yake amekuwa akimuunga mkono mama yake katika kazi, lakini aliongeza pia kuwa haitakuwa sahihi kusema kwamba mafanikio yake yalitolewa angaliwa kwa jicho sawa na jinsi mafanikio ya baba yake yalivyotathminiwa.

"Ninakumbuka nilipokuwa Arkansas mwaka 1980, kulikuwa na msukumo mkubwa kwa mama yangu kubadilisha jina lake kutoka Hillary Rodham na kuwa Hillary Rodham Clinton,

kitu ambacho alikubali kukifanya kwa sababu aliona ni kama kinaleta malumbano yasiyo na maana na alikuwa anataka kusonga mbele kwa kuweka kipaumbele kwa kile alichohisi kuwa anakitaka", Chelsea Clinton alieza.

Bi.Clinton ambaye ni mkuu wa asasi isiyokuwa ya kiserikali ya Clinton Foundation, alidai kwamba hana mpango wa kuwania wadhifa wowote labda kwa siku za mbeleni.

"Huwa ni labda kila siku, lakini inapaswa kuwa labda kwa kila mtu", Chelsea alisema

"Ikiwa sio sasa, basi haitatokea tena, kwa sababu nna matumaini kuwa kila mtu ambaye anajali mafanikio ya nchi yake kwa siku zijazo atajihisi

namna hiyo labda kugombea uongozi wa shule au uraisi au kugombea nafasi yeyote ile".

Aliongeza kuwa ana matumaini kwamba watu wengi wanadhani atagombea nafasi ya uongozi kwa sababu yatakuwa maamuzi sahihi kwake na kwao.

Bi Clinton ameandika vitabu viwili vya picha kwa ajili ya watoto, vinavyoitwa , ambavyo vyote vimeangazia mwanamke ambaye anatumia sauti yake kufanya maamuzi ili kuleta mabadiliko na kuweka historia.

Mwanamke mmoja katika kitabu chake anayeitwa Caroline Herschel, ambaye ni mtaalamu aliyegundua vumbi lililokuwa karibu na jua katika karne ya 18 lakini hakupata umaarufu kama kaka yake aliyegundua sayari ya Uranus.

" Kwa muda mrefu tumekuwa tukitofautisha uwasilishaji wa historia , anayefundisha historia ataelewa umuhimu wa utofauti wa historia hiyo.

Nadhani kuna umuhimu mkubwa , haswa kwa sasa, tunaweza kuwafanya wanawake wengi wang'are kutokana na ujuzi wao ambao umeusaidia ulimwengu na kuongeza ujuzi katika sayansi katika mambo mengi yanayoendelea kufanyika.

Wanawake 100 wa BBC(BBC 100 Women) imeandika kuhusu wanawake watano na Caroline Herschel,ambaye mafanikio yake yalimezwa na kazi za ndugu zake wa kiume.

Wanawake 100 wa BBC maana yake nini?

Wanawake 100 wa BBC ni majina 100 ya wanawake wenye ushawishi duniani kote kila mwaka na huwa inaandika kuhusu kazi au taarifa zao.

Imekuwa ni mwaka muhimu sana kwa haki za wanawake duniani,

Hivyo mwaka 2018 wanawake 100 wa BBC inatoa taswira ya wanawake wamechochea maendeleo kwa kutumia nguvu zao zote na kutaka kubadili dunia inayowazunguka.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii