Mtoto wa miaka 13 aliyepinga umiliki wa bunduki auawa kwa kupigwa risasi Marekani kwa msimamo wake

Bi Sandra Parks Haki miliki ya picha WDJT
Image caption Bi Sparks aliyeuawa huko Milwaukee

''Tuko katika hali ya machafuko. Katika mji ninakoishi, husikia visa na kujionea mifano mingi ya visa kama hivi kila siku. Watoto wadogo ndio waathiriwa wa visa vya kufyatuliwa risasi kiholela…''

Miaka miwili iliyopita, mwanafunzi msichana wa umri wa miaka 11 Sandra Parks, aliandika maneno haya katika shindano la uandishi wa insha kwa kuandika kuhusu mauaji katika mji wake.

Siku ya Jumatatu usiku, msichana wa miaka 13, alipigwa risasi iliyopigwa kuelekea nyumbani mwao.

Familia hiyo iliyokuwa na wasiwasi na ikapiga simu nambari za dharura za 911, lakini Sandra alifariki kabla hajapokea matibabu.

Mamake msichana huyo, Bernice Parks, ameiambia polisi kwamba alilala mapema huku watoto wake wengine wakiendelea kutazama televisheni. Aliamshwa na mlio wa risasi dakika chache kabla ya saa mbili usiku na kumpata mtoto wake akivuja damu sakafuni.

''Mama nimepigwa risasi, wapigie polisi, Bi Parks aliambia kituo cha Televisheni cha WITI .'Nilimuangalia. Lakini hakulia, wala kupiga kelele. Alikuwa mtulivu… hakustahili kuiaga dunia katika hali hiyo.''

Meya wa mji wa Milwaukee ulioko Marekani, Tom Barrett ameelezea tukio hilo kama la ''uendawazamu'' akizungumza na wanahabari.

Barett amesema kisa hicho kilisababishwa na mtu aliyeamua kupiga risasi kuelekea katika nyumba hiyo.

Sasa msichana huyo amefariki katika kipindi cha kusherehekea wiki ya shukrani katika chumba chake.

Bw Barett anadhani kwamba mpigaji risasi hiyo alitaka 'kutimiza lengo, kwa kudhihirisha hasira ili kumshtua mtu, alisema hilo siku ya Jumanne: Kile tunachofahamu ni msichana huyo alifariki usiku wa kuamkia jana katika chumba chake cha malazi.

Haki miliki ya picha MILWAUKEE COUNTY JAIL
Image caption Washukiwa waliotekeleza mauaji ya mtoto huyo Isaac D. Barnes na Untrell Oden

Jarida la Milwaukee limeripoti kuwa mshukiwa mmoja, Isaac D. Barnes amefunguliwa mashtaka ya mauaji na wa pili Untrell Oden, anadaiwa kukabiliwa na mashtaka mawili ya kusaidia kuficha risasi.

Mpenzi wa zamani wa Bw Barnes anadaiwa kuwadokezea polisi kuhusu uwezekano wake kuhusika katika mauaji hayo.

Anasema mpenzi wake huyo alifika kwenye gari lake akiwa amevalia barakoa na bunduki kubwa yenye mifuo.

Anadai kwamba alimwambia 'una bahati, watoto wako wamo kwenye gari, nilikuwa nimepanga kukuangamiza'.

Polisi walimpata Bw Barnes katika nyumba iliyo karibu akijificha kwenye kabati.

Mji huo wa Milwaukee umeripotiwa kuwa visa vya mauaji vimepungua tangu mwaka 2014 na 2015 ambapo visa vya mauaji vilikuwa juu zaidi lakini tangu hapo mji huo umeorodheshwa kuwa hatari zaidi nchini Marekani, kulingana na takwimu za FBI.

'Sandra alikuwa kila kitu ambacho hakipatikani duniani'

Sandra alikuwa mwanafunzi katika shule ya Keefe Avenue.

Aliandika insha yenye mada ya "Our Truth" (Ukweli Wetu) iliyoshinda kwa kuwa nambari tatu katika mashindano ya shule za umma yanayoandaliwa kila mwaka ya Martin Luther King Jr.

Alizungumza katika radio ya Wisconsin mwezi Januari mwaka 2017, akisema anatamani ''kukomesha visa vyote vibaya vinavyoendelea.''

Parks alisema kile unachokisikia ni kwamba mtu ameuawa au amepigwa risasi. Watu hawajali kuhusu baba, mtoto au mjukuu aliuliwa'' .

Bi Parks aliambia jarida hilo la Milwaukee kwamba mtoto wake '' alikuwa kila kitu ambacho hakipo duniani.''

''Mtoto wangu alikuwa mtu mtaratibu. Mtoto wangu hakupenda vita,'' alisema. 'Kila mtu alimfahamu alimfurahisha.

Kulingana na shule hiyo ya umma Milwaukee imesema Sandra ni mwanafunzi wao wa saba kuuawa mwaka 2018.

Katika maombolezo yake yaliofanyika siku ya Jumanne, alikiri kwamba msiba huo ni mzito sana.

''Kwa ufahamu wangu kuna watoto wengi wamefariki hivi majuzi na siwezi kusema mtoto wangu alikuwa bora kuliko wengine, alisema Bi Parks

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii