Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 24.11.18: Kante, Hazard, De Bruyne, Lennon, McCarthy, Weigl, De Jong

N'Golo Kante, Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption N'Golo Kante

Mchezaji wa Chelsea N'Golo Kante, mwenye umri wa miaka 27, atalipa kodi zaidi nchini Uingereza kuliko kampuni kubwa ya kimataifa ya Amazon, baada ya kusaini mkataba mpya wa pauni milioni 15. (Sun)

Meneja wa Chelsea Maurizio Sarri ana matumaini kuwa mshambuliaji wake Eden Hazard atafuata nyayo za N'Golo Kante kusaini mkataba mpya wa kusalia Stamford Bridge. (Standard)

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho anasema wachezaji kisasa ikiwa ni pamoja na wachezaji wake Luke Shaw , Anthony Martial, Jesse Lingard na Marcus Rashford wanakosa ukomavu na wanahasira . (Mirror)

Chelsea na Juventus wanamfuatilia kwa ukaribu kinda Yunus Akgun,raia wa Uturuki anaipiga na Galatasaray. (ESPN)

Meneja wa Arsenal Unai Emery amekubali timu yake inahitaji kuimarika zaidi kama wanataka kupigania nafasi nne za juu za ligi kuu.(Mail)Pep Guardiola

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola amesema hakuna namna kwa mabingwa watetezi waligi kuingia sokoni mwezi januari kusajili nyota wapya(Express)

Mlinzi wa klabu ya West Ham Pablo Zabaleta anaweza kupata mkataba mpya katika klabu yake baada ya kuonyesha soka la kuvutia msimu(Mirror)

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Pep Guardiola

Pep Guardiola atasubiri mpaka kipindi cha majira ya kiangazi kuangalia uwezekano wa kumsajili kiungo wa Ajax Frenkie de Jong, 21. (Telegraph)

Arsenal wanamuangalia kiungo wa Borussia Dortmund, Julien Weigl ambae anataka kuondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu (Bild - in German)

Juventus watazui uhamisho wa mabeki Medhi Benatia, 31, na Daniele Rugani, 24, ambao wanahusishwa kujiunga na vilabu vya AC Milan and Chelsea. (Goal)

Klabu ya Galatasaray inavutiwa na kumsajili mshambuliaji wa Liverpool Dominic Solanke, 21, meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amesema watamtoa mchezaji huyo kwa mkopo Japo Solanke amekuwa akihusishwa na kujiunga na Ranger ya Scotland inayonolewa na Steven Gerrard (Fotospor - in Turkish)

Meneja wa Chelsea Maurizio Sarri amekiri, Manchester City wako imara zaidi bila kujali kama klabu ya London itatumia kiasi kikubwa cha pesa katika dirisha la usajili la Januari. (The Guardian)

Haki miliki ya picha Getty Images

Winga Aaron Lennon amesema klabu yake Burnley imemsaidia kupenda tena mpira wa miguu baada kupata matatizo ya afya ya akili (Mail)

Kiungo wa Paris St-Germain, Adrien Rabiot anajianda kukutana na rais wa klabu hiyo Nasser Al Khelaifi kujadili kama naweza kusalia klabuni hapo au aeleke Barcelona .(Sport)

Mchezaji wa zamani wa Barcelona na Real Madrid Bernd Schuster anaamini Nou Camp ni mzigo mzito kwa winga Ousmane Dembele, 21. (Mail)

Sahihiho 27 Novemba, 2018: Taarifa hii awali ilikuwa imeiorodhesha kampuni ya Starbucks kuwa miongoni mwa kampuni ambazo mchezaji N'Golo Kante atakuwa akizizidi kwa ulipaji kodi baada yake kutia saini mkataba mpya. Hilo halikuwa sahihi, na tumeliondoa jina la kampuni hiyo kutoka kwenye tetesi hizo. Tunaomba radhi kwa wasomaji na kwa kampuni ya Starbucks kwa usumbufu uliotokea.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii