India: Simulizi ya mama anayehuzunika na athari za uraibu zilivyompoteza mwanae

Ricky Lahoria
Image caption Mtoto wa Lakshmi Devi alikufa kutokana na uraibu wa dawa za kulevya

Mji wa kaskazini wa India umeshuhudia kuona ongezeko kubwa la vifo vinavyosababishwa na uraibu wa madawa ya kulevya, mwaka huu.

"Alikuwa mtoto wangu pekee lakini nilitamani afe tu… Na sasa ,nnalia usiku wote nikiwa nimeshika picha yake," Lakshmi Devi mwenye umri wa miaka 55 alisema.

Huyu kijana wake Ricky Lahoria, alifariki akiwa na miaka 25.

Mtoto wake ni miongoni mwa watu 60 waliokufa kwa sababu ya uraibu wa madawa ya kulevya katika mji wa Punjab katika mwezi Januari na Juni 2018,

Mamlaka inakadiria kuwa ni watu 30 zaidi wamekufa mwaka huu kutokana na uraibu wa dawa za kulevya ukilinganisha na mwaka 2017.

Maafisa wa polisi wanasema idadi inaweza kuongezeka watakapotoa takwimu zote za mwaka 2018.

Ni mwaka mmoja sasa tangu dawa za kulevya zimepigwa marufuku Punjab.

Awali eneo hilo lilikuwa linatumika kuzipitisha tu kutoka sehemu moja kwenda nyingine lakini sasa ndio wamekuwa wateja wakubwa.

Waziri wa afya wa Punjab, Brahm Mohindra aliiambia BBC kuwa serikali yake imepunguza uingizwaji wa dawa hizo. Lakini anashangaa kwa nini kuna vifo vingi vinavyodaiwa kusababishwa na dawa za kulevya kwa mwaka huu kuliko miaka iliyopita.

"Haijawekwa wazi kuwa ni mchanganyiko wa dawa zipi ndio umesababisha vifo.

Lakini kuna vifo vingi vimetokea. Ni kitu ambacho kinashtua kutokea", waziri alisema.

Utafiti ambao ulifanywa na chuo kikuu cha sayansi mjini Delhi mwaka 2015, ulibainisha kwamba waathirika wa madawa ya kulevya mjini Punjab walikuwa zaidi ya laki mbili.

Haki miliki ya picha Getty Images

Bi. Devi alisema kwamba Ricky alianza kutumia dawa za kulevya wakati ambapo bado yuko shule n ahata alishindwa kumaliza shule.

Siku za mwanzoni, alikuwa na uraibu wa dawa ya kikohozi na akaja kwenye kujidunga sindano lakini badae akaanza kutumia heroin, ambayo kwa kina la huko wanaiita 'chitta'

Anakumbuka kuwa mtoto wake alikuwa anataka kuacha na hata alimuomba amsaidie.

Lakini hakujua ampeleke katika kituo gani cha kutibu uraibu ampeleke.

"Nilimpeleka tu katika hospitali ya kawaida, ambapo alikufa baada ya siku tatu," alisema.

Suluhisho ni nini?

Haki miliki ya picha Getty Images

Maafisa wa afya wamesema kwamba wanataka kufungua vituo zaidi vya kutibu uraibu kwa sababu sasa vipo vichache.

Ikiwa kati ya vituo 90 vya kutibu uraibu, 50 tu vinaendeshwa na serikali.

Serikali imekuwa ikifanya kampeni mbalimbali shuleni na chuoni ili kuwaelimisha watu kuhusu dawa za kulevya.

Lakini familia nyingi vijijini hawavijui vituo hivyo na namna ambavyo vinafanya kazi.

Na unyanyapaa ambao upo kwa waraibu husababisha watu kushindwa kutafuta msaada.

Mada zinazohusiana