Ethiopia: Msiba wageuka kuwa sherehe

Mwaume aliyefufuka Ethiopia Haki miliki ya picha SIBU SIRE COMMUNICATION

Wanakijiji wa kijiji kimoja nchini Ethiopia washeherekea kufufuka kwa mwanaume mmoja ambaye alidhaniwa kuwa amekufa.

Hirpha Negero, ambaye ni baba wa watoto watano alitangazwa kuwa amefariki siku ya jumanne ,majira ya saa nne na nusu.

Kulingana tamaduni zao katika vijiji vya pembezoni mwa miji vilivyopo Sibu Sire na mkoa wa Oromia,bunduki ilipigwa mara mbili na hiyo ni ishara kuwa kuna mtu amefariki hivyo watu wanaitwa kuhudhuria katika msiba.

Ndani ya saa moja, mwanakijiji mmoja kwa jina la Etana Kena alimuweka kwenye jeneza tayari kwa mazishi.

Ingawa wakati wa mazishi katika majira ya saa tisa na nusu, walisikia mtu akigonga kutoka katika jeneza.

''Watu walishangaa na huku wengine wakikimbia na hata sikupata mtu wa kunisaidia," bwana Etana alieleza namna alivyohitaji msaada ili aweze kulifungua jeneza.said.

Mtu aliyefufuka aliiambia BBC jinsi alivyojisikia akiwa ndani ya jeneza: "Nilisikia sauti ya mtu akilia. Nlikuwa sina nguvu kabisa n ahata sikuweza kuongea."

Lakini badaye aliweza kuanza kuita.

Baada ya mshtuko ambao uliwapata wengi katika msiba, mazishi yaligeuka kuwa sherehe.

Hirpha alieleza kuwa alishawahi kuzika maiti zaidi ya 50 lakini hakuwahi kukutana na tukio kama hilo.

"Alionekana kuwa amekufa kabisa".

Dr Birra Leggese aliiambia BBC kwamba labda alikuwa amepooza.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii