Watu 29 wafariki kwenye ajali ya mashua ziwa Victoria Uganda

Watu 26 wafariki kwenye ajali ya mashua ziwa Victoria Uganda
Image caption Watu 29 wafariki kwenye ajali ya mashua ziwa Victoria Uganda

Polisi nchini Uganda wanasema kuwa watu 29 wamefariki kufuatia ajali ya mashua iliyotokea ziwa Victoria.

Shughuli za uokoaji zinaendela lakini naibu Inspekta mkuu wa polisi anayesimamia oparesheni hiyo Asuman Mugenyi anasema kuna uwezekano mdogo wa kupata manusura.

Anasema mashua hiyo ilikuwa inasafirisha zaidi ya watu 90 kwenda kisiwa kimoja katika ziwa Victoria.

Mashua hiyo iliyokuwa na watu waliokuwa wanaelekea sherehe, ilipata ajali katika kaunti ndogo ya Mpatta wilaya ya Mukono.

Prince David Wasajja, ndugu wa mfalme wa Buganda mfalme Kabaka Ronald Mutebi alikuwa pia kwenye mashua hiyo lakini aliokolewa,

Image caption Watu 29 wafariki kwenye ajali ya mashua ziwa Victoria Uganda

Vyombo vya habari nchini Uganda vinasema mwanamuziki Iryn Namubiru naye alinusurika ajali hiyo.

Wasanii kadhaa na watu wengine mashuhuri waliaminika kuwa kwenye mashua hiyo.

Mashua hiyo ilitajwa kukodiwa kwa karamu za wikendi.

Wengi wa wale waliokuwemo hawakuwa wamevaa mavazi ya kuokoa maisha.

Maafisa walisema kwa mashua mbili za uvuvi ambazo ziliwasili kuokoa nazo zilifurika watu na kuzama.

Mada zinazohusiana