Rais wa Korea Kusini amefichua 'zawadi ya amani' iliyotoka kwa Kim Jong Un

Wanambwa waliyozaliwa na mbwa wa amani walitumwa na Kim Jong-un Haki miliki ya picha Blue House
Image caption Wanambwa waliyozaliwa na mbwa wa amani walitumwa na Kim Jong-un

Rais wa Korea Kusini ametoa picha ya kwanza ya watoto wa mbwa waliyozaliwa na mmoja wa mbwa aliyopewa kama zawadi ya amani na kiongozi wa Korea kaskazini.

Mbwa huyo anafahamika kama Gomi.

Kiongozo wa Kaskazini Kim Jong-un, amemtumia mbwa hao mwenzake wa Kusini Moon Jae-in katika juhudi ya kudumisha amani licha ya msuko suko unaoshuhudiwa katika rasi ya Korea.

Gomi, mbwa wa Pungsan anayesifika kwa uwindaji wake hatari alizaa watoto sita, wa kike watatu na wa kiume watatu.

Rais Moon aliweka picha ya mbwa hao katika mtandao rasmi wa Twitter wa Blue House siku ya Jumapili.

"Ikizingatiwa kuwa mbwa hubeba mimba kwa karibu miezi miwili, huenda, tulikabidhiwa Gomi akiwa na mimba," inaripotiwa aliandika hayo mbwa hao walipozaliwa. "Natumai uhusiano wa Korea mbili utakuwa hivi."

Siku kadhaa baada ya mbwa hao kuzaliwa, ndege za kijeshi za Korea Kusini zilitua Pyongyang na shehena ya machenza.

Image caption Rais Kim Jong Un na wa Korea Kusini, Moon Jae-in

Awali Kaskazini ilikuwa imetuma makasha makubwa ya uyoga katika eneo la mpakani wakati wa mkutano kati ya viongozi hao wawili.

Gomi na mbwa wengine, Songgang, walisafirishwa Kusini wakiwa na karibu pauni saba ya chakula na kuungana na mbwa wengine wa rais Moon ikiwa ni pamoja na mbwa anayefahamika kama Tory.

Bwana Moon amekutana na Kim mara tatu mwaka huu na amekuwa kama mpatanishi kati yake na rais wa Marekani Donald Trump.

Mnamo mwezi Septemba , alikuwa kiongozi wa kwanza wa Korea Kusini kuhutubia watu wa Korea Kaskazini wakati wa ziara yake mjini Pyongyang.

Rais wa zamani Robert Mugabe 'hawezi kutembea'

Alizungumza katika michezo ya Arirang- ambayo inatajwa kuwa shughuli kubwa ya propaganda - ambapo aliwahutubia takriban 150,000.

Hivi karibuni rais Moon alisema kuwa anaamini mzozo wa Korea utakomeshwa hivi karibuni.

Mapigano yalikomeshwa mwaka 1953 lakini hakuna mkataba wa amani uliotiwa saini.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii