Nyuki 'Milioni moja wafa Cape Town' Afrika Kusini kutokana na sumu

nyuki Afrika Kusini Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption kampeni ya kunusuru nyuki imeanza

Takriban nyuki milioni moja wanakisiwa kufa kutokana na sumu katika viwanda na maeneo ya utengenezaji wa mvinyo nchini Afrika Kusini.

Brendan Ashley-Cooper ameiambia BBC kwamba dawa ya kuua wadudu inayotumiwa na wakulima wa divai, Fipronil, ndiyo iliyosababisha vifo vya nyuki katika shamba lake.

Mfugaji mwingine wa nyuki katika eneo hilo la Cape Town naye pia ameathirika, ingawa mpaka sasa haijafahamika idadi ya nyuki waliokufa.

Watumiaji wa dawa ya kuua wadudu aina hii ya Fipronil, wameingia lawamani kutokana na vifo vya mamilioni ya nyuki barani Ulaya.

Wanaharakati wa kutetea mazalia ya nyuki wanasema kwamba Fipronil ina kiwango kikubwa cha sumu kwa nyuki wazalishao asali na wadudu wengine, na matumizi yake yalipigwa marufuku barani Ulaya mwaka 2013.

Karibu mizinga 100 ya nyuki, zaidi ya silimia thelathini na tano ambayo anaimiliki katika eneo lililoathirika, imekumbwa na janga hilo, amearifu Ashley-Cooper,ambaye ni makamu mwenyekiti wa wamiliki wenye Viwanda vya wazalishaji asali walioko Magharibi mwa nchi hiyo, na kukadiria kuwa nyuki wake wapatao milioni moja ama milioni moja nukta tano wamekufa.

Haijafahamika wazi kuwa nchini Afrika Kusini kuna nyuki wangapi, ingawa vifo vya nyuki hao hawawezi kuleta tofauti kubwa kwa idadi ya nyuki wao kwa ujumla.

Je kutakuwa na uhabawa asali katika msimu wa sikukuu za mwishoni mwa mwaka kufuatia tukio hilo?

Wadudu hao wa Fipronil walijichanganya pia kwenye suala la mayai barani ulaya mwaka huu pia.

Mamilioni ya mayai yalilazimika kuondolewa katika vichanja vya maduka makubwa ya bidhaa, katika nchi zaidi ya dazeni za Ulaya, ikiwa ni pamoja na Uingereza,baada ya kugunduliwa kwamba baadhi yalikuwa yamenajisiwa na wadudu hao.

Fipronil hutumiwa kuondokana na viroboto,pamba na tiba lakini ni marufuku kwa nchi za Umoja wa Ulaya kutumia sumu hiyo kwa viumbe ambavyo baadaye vitatumika kama wanyama kwa matumizi ya binadamu kama vile kuku.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption kampeni ya kunusuru nyuki imeanza

Uchunguzi zaidi unaendelea kufanyika ili kuthibitisha ikiwa ni Fipronil imehusika, na wamiliki hao wawili wa viwanda vya mvinyo pamoja na serikali kwa pamoja wanashirikiana katika kukabiliana na tatizo hilo.

Mmoja wa wafugaji nyuki bwana Ashley-Cooper, anaarifu kuwa wiki moja iliyopita walianza kupokea simu za wakulima na wafugaji kuwa wanashuhudia nyuki wengi wakiwa wamekufa mbele ya mizinga yao.

Na kwa kiasi kikubwa mizinga mingi imeathirika vibaya na huenda wapenzi wengi wa asali wakajikuta wana sherehekea sikukuu za mwishoni mwa mwaka bila asali.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii