Sentinel: Huyu ndiye mtu pekee aliyeweza kujenga urafiki na kuishi na kabila linaloogopwa zaidi duniani

Pandit akimkabidhi nazi mwanamume wa Sentinelese mwaka 1991 Haki miliki ya picha TN Pandit
Image caption Picha ya bwana Pandit akimkabidhi nazi mwanamume wa Sentinelese mwaka 1991

Sio watu wengi walio na ufahamu kuhusu jamii ya sentinel kama T N Pandit ambaye ni mtaalamu wa masuala ya jamii za kale nchini India.

Kama mkuu wa kikanda wa wizara ya masuala ya jamii nchini India, Pandit alizuru kisiwa hicho kilichotengwa kwa miongo kadhaa.

Watu wa Jamii ya Sentinel waliyotengwa kwa maelfu ya miaka waligonga vichwa vya habari kwa mara ya kwanza duniani wiki iliyopita.

Hii ni baada ya kudaiwa kuwa walimuua John Allen Chau raia wa Marekani ,2,7 ambaye alikuwa akiendesha shughuli za kimishonari katika kisiwa hicho.

Kundi la kimataifa la kutetea haki la Survival International sasa linahofia shughuli ya kuutafuta mwili wa mmishonari huyo wa Marekani huenda ikawa hatari zaidi.

John Allen Chao anadaiwa kuuawa kwa kufumwa mchale baada ya kutua katika eneo la Sentinel Kaskazini Novemba 17.

Wikendi iliyopita maafisa wa India walijaribu kuchukua mwili wa Chau lakini boti ya polisi iliyokuwa ikiongoza oparesheni hiyo ilikabiliwa vikali na wapiganaji wa kabila la Sentinel.

Maafisa walilazimika kusitisha shughuli hiyo.

Mkurugenzi wa shirika la Survival Internationla Stephen Corry, anasema ''Juhudi kama hizo siku zilizopita ziliishia watu wa jamii hiyo kupigania kisiwa chao.''

''Wachaneni na mwili wa Chau na hali kadhalika watu wa jamii ya Sentinel'' alisemabwana Corry.

Nini kilichofanyika?

Wavuvi waliyomsafirisha Chau kwenda Sentinel Kaskazini wanasema waliwaona watu wa jamii hiyo wakiuburuza mwili wake ufukweni na kuuzika.

Wavuvi hao baadae waliwapeleka polisi kuwaonesha mahali wanapoamini mwili wa marehemu ulipozikwa.

Wavuvi sita pamoja na mtu mwingine mmoja wametiwa mbaroni kuhusiana na kisa hicho

Siku ya Jumamosi polisi walipiga kambi katika ufuo wa kisiwa hicho karibu mita 400 na kwa kutumia darubini waliwaona wapiganaji wa jamii hiyo wakiwa wamejihami vikali kwa nyuta na mishale.

Lakini bwana Pandit, ambaye sasa ana miaka 84, anasema kundi hilo ni la watu "wapenda amani" na anaamini kuwa hali ya kuwaogopa ni ya kuwaonea.

"Wakati nilipotangamana nao walinitishia lakini vitisho hivyo havikufikia kiwango cha kutaka kunijeruhi au kuniua.'' aliiambia BBC.

Kila tulipoona hasira zao zimepanda tulikuwa tunadhibiti shughuli zetu na kurudi nyuma.

"Namsikitikia yule bwana mdogo kutoka Marekani aliyepoteza maisha yake. Lakini alifanya makosa. Alikuwa na muda wa kutosha wa kujiokoa, lakini alilazimisha mambo na hatimaye akalipia kwa maisha yake."

Mara ya kwanza Pandit alipoamua kutembelea kisiwa na Sentinel Kaskazini, mwaka 1967 alizuru eneo hilo kama sehemu ya kundi lililokuwa linafanya safari za kibinafsi ya kujionea mambo mapya.

Awali watu wa kisiwa hicho walikuwa wanajificha misituni wakiona wageni na baadaye kuwashambulia kwa kuwafuma kwa mishale.

Alisema wataalamu wa kijamii walikuwa wakijaribu kuwaletea vitu tofauti kila wanapowatembelea kama njia ya kujenga uhusiano mzuri.

Haki miliki ya picha Survival International
Image caption Kuna picha kidogo sana ya watu wa kabila hilo linaloogopewa

"Tulileta zawadi kama vile vyombo vya kupikia na nazi pamoja na vifaa vya kujengea kama vile mabarti na nyundo. Pia tuliwatumia wenyeji waliyotusaidia kutafsiri lugha na kuelewa tabia na mila zao. Aliandika katika kumbukumbu ya safari zake.

"Lakini wapiganaji wa Sentinel wana nyuso za hasira na huwa wamejihami vikali kwa nyuta na mishale kulinda ardhi yao."

Licha ya juhudi hizo wageni hawakufanikiwa kuingia katika makaazi ya watu hao.

Anasema katika kisa cha kushangaza ni wakati wageni walipo wapaia zawadi ya nguruwe, badala ya kufurahia zawadi waliyopewa waliamua kumuua mnyama huyo na kumzika.

Juhudi za kutangamana nao

Baada ya juhudi kadhaa za kujenga uhusiano na watu wa jamii hiyo hatimaye walifanikiwa kuwafikia mwaka 1991 baada ya watu hao kujitokeza kwa amnai na kukutana nao katika eneo la pwani

"Tulishangazwa sana na hatua hiyo," alisema. "ilikuwa uamuzi wao kukutana na sisi na mkutano huo ulifanyika kwa masharti yao."

"Tuliruka kutoka ndani ya boti na kusimama ndani ya maji yaliyotufikia shingoni na kuanza kuwagawanyia nazi na zawadi nyingine. Lakini hatukuruhusiwa kukanyaga katika ardi ya kisiwa chao."

Haki miliki ya picha TN Pandit
Image caption Bwana Pandit (kulia) alifanyia kazi wizara ya masuala ya kijamii ya India

Bwana Pandit anasema hakuwa na hofu ya kuvamiwa lakini muda wote alikuwa makini akiwa karibu na watu hao.

Anasema watu wa kikundi chake walikuwa wanawasiliana kwa lugha ya ishara na ile ya wasentinel lakini ilikuwa vigumu kwasababu mara nyingi walikuwa wametekwa mawazo na zawadi walizoletewa.

"Wanazungumza wao kwa wao na sisi hatukuelewa lugha yao. japo inakaribiana na lughu inayozungumzwa na makabila menginekatika eneo hilo," anakumbuka bwana Pandit.

'Sikukaribishwa'

Katika moja ya safari zake anasema hatawahi kusahau kisa ambapo mmoja wa watu wa jamii hiyo alimtishia.

"Nilipokuwa nikiwagawanyia nazi na zawadi zingine mtu huyo alinitishia na hpo ndipo nilijitenga na wenzangu na kuanza kurudi taratibu ufuoni," aliiambia BBC.

"Mvulana mmoja wa Kisentinel aligeuza sura na kuchukua kisu akiashiria kuwa atanikata kichwa. Bila kupoteza muda niliitisha boti na kuomba kuondoka eneo hilo haraka iwezekanavyo,"

"Hatua ya kijana huyo ilikuwa nzuri kwa sababu ilinionyesha wazi kuwa uwepo wangu mahala hapo hautakikani."

Serikali ya India ilipiga marufuku ziara ya kuwatunuku watu wa jamii hiyo katika kisiwa cha Sentinel ikiwa ni pamoja na kuzuru ziara zinazohusu kisiwa hicho.

Kuwatenga kabisa watu hao kunamaanisha hawana uhusiano wowowte na watu wa nje hali ambayo inawaeka katika hatari ya kuambukizwa magonjwa kwa sababu hawana kinga dhidi ya magonjwa kama vile ukambi.

Bwana Pandit hata hivyo anasema kundi lake lilikuwa linafanyiwa uchunguzi wa dawa kimatibabu kabla ya kuzuru Sentinel Kaskazini.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii