Wakulima wanavyogeukia kilimo cha bangi kutokana na faida yake Lesotho

Mampho Thulo in her marijuana field in Lesotho
Image caption Mampho Thulo hufanya kilimo cha bangi bila leseni

Lesotho ina malengo ya kupata fedha kutoka kwa biashara inayokua kwa kasi ya bangi, lakini mwandishi wa BBC Vumani Mkhize anasemna taifa hili ya kusini mwa Afrika tayari linakabiliana na biashara haramu ya bangia kwa matumizi ya kujiburudisha.

Vumbi inaibuka kando mwa Mampho Thulo wakati anatumia mikono yake kukusanya matawi yaliyokauka ya bangi kutoka sakafuni nyumbani mwake kwenda kwa mfuko mkubwa,

Amekuwa akifanya kilimo cha bangi kijijini mwake huko Mapoteng kwa miaka mingi.

Kilomita 70 kaskazini mashariki mwa mji mkuu Maseru, shamba lake liko kwenye bonde linalozungukwa na milima ambayo ni mingi sana nchini humo.

Ni eneo hili lenye mandhari ya kupendeza ndipo watu wamekuwa wakifanya kilimo haramu cha bangi ya kujiburudisha kwa miongo kadhaa.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Bangi

Milima na ardhi yenye rutupa huwawezesha wakulima kuzalisha kiwango cha juu cha bangi kinachotambuliwa kote duniani.

Karibu na mji mkuu, wafanyakazi wako kwenye vituo vilivyo sawa na mazingira na mahabara kuzalisha bangi kwa njia halali kwa matumizi ya kiafya wakati nchi inajaribu kuvuna kutokana na kuongezeka mahitaji ya bangi.

Mwaka uliopita Lesotho ilikuwa nchi za kwanza barani Afrika kuhalalisha kilimo cha bangi kwa matumizi ya afya, hatua iliyoibua sekta mpya kwenye nchi inayokumbwa na changamoto za kubuni ajira.

Lakini pande hizi zina mwanya mkubwa kwa kuwa wakulima wadogo hawakuwa na uwezo kwa miundo msingi na leseni ambazo biashara kama hii inahitaji.

'Mikononi mwa walanguzi'

Kwa Bi Thulo, mama wa watoto watano, bangi ni mmea wa thamani kubwa.

"Hivi ndivyo tunapata kipato kwa kuwa ajira kidogo zilizopo ni za watu wanye elimu. Kwa hivyo tutagemea bangi kwa sababu hatuna kisomo," aliiambia BBC

Image caption Bangi ya matibabu hupandwa kwenye mazingira sawa na mahabara

Licha ya kuondolewa marufuku katika kilimo cha bangi kwa matumizi ya afya, kile Bi Thulo anafanya - kilimo kwa minajili ya kujiburudisha bado ni haramu.

Hatari ya kukamatwa kwa mama huyu miaka 48 huimzuii.

"Ndio ninajua ni haramu kufanya kilimo cha bangi," anasema.

"Watoto wangu wanasoma kwa sababu ya bangi. Nikiuza ninawalipia mimi huwalipia karo."

Amekuja kuzoea uvamizi kutoka kwa polisi ambao wakati mwingine humpokonya mazao yake.

Image caption Lesotho's high altitude and fertile soils are perfect growing conditions for marijuana

Jiografia ya ardhi ya Bi Thulo iliyo kwenye milima yenye miteremko mirefu uhakikisha kuwa bangi yote haichukuliwi.

Wakati wa kuuzwa yeye hujipata mikononi mwa walanguzi ambao amesema hununua kwa pesa kidogo sana ikilinganishwa na thamani yake.

"Wao ndio huamua bei, kwa sababu wanajua tunahitaji pesa sana.

"Mnunuzi atasema nitalipa dola 36 kwa mfuko wa kilo 50. Nina njaa sina chakula, nyumbani hakuna chochote. Huwa ninachukua tu hizo pesa."

Mwanzilishi wa kilimo cha bangi Afrika

Sekta mpya ya kilimo cha bangi matumizi ya afya inatarajiwa kugubika ile haramu ya wakulima wadogo.

Image caption Medigrow tayari inaajiri wafanyakazi 400

Kote duniani kilimo cha bangi ya afya ni biashara kubwa.

Kuingia kwa Lesotho kwenye sekta ya kilimo cha bangi imechochea nchi zingine kuhalalisha sekta hii.

Zimbabwe pia imehalalisha kilimo cha bangi na serikali zingine za Afrika pia nazo zinataka kufuata mkondo kama huo.

Nchini Afrika Kusini mahakama ya katiba ilihalalisha kilimoa cha bangi na matumizi yake kwenye uamuzi mkubwa zaidi mwaka huu.

Serikali ya Lesotho tayari imetoa leseni kwa kampuni kadhaa za kimatiafa kukuuza na kuuza bidhaa za bangi.

Nchi hiyo imefanikiwa kuwavutia wawekezaji kutoka Canada, ambao wamepata mazingira bora na gharama ya chini ya kufanya biashara zao.

Mwaka huu pekee kampuni ya bangi kutoka Toronto iliwekeza dola milioni 10 huko Medigrow Lesotho ikiwa ni asilimia 10 ya hisa kwenye kampuni hiyo.

Image caption Ramani ya Lesotho

Tangu jadi kilimo cha bangi kimekuwa kikifanyika nchini Lesotho.

Mafuta ya CBD ndicho kitu muhimu ambacho wakulima wa bangi wanatafuta.

Mafuta kutoka kwa bangi kisha hutumiwa kama dawa kutibu magonjwa tofauti.

Medigrow ilipata idhini ya Lesotho kuanza kilimo cha bangi mwaka 2016 mwaka mmoja kabla ya serikali kuhalalisha kilimo cha bangi ya minajili ya kiafya kwa kampuni zote.

Kwa kipindi cha miaka 15 kampuni hiyo imepiga hatua kubwa: imejenga barabara, mifumo ya mawasiliano na kwa sasa inakaribia kumaliza kujenga nyumba za kuishi na kiwanda cha mafuta ya CBD.

Kwa sasa Bi Thulo ataendelea kukuza bangi kwa njia haramu na hafahamu chochote kuhusu bangi kwa minajili ya matibabu.

Mada zinazohusiana