John Allen Chau: Je wamishonari wanasaidia au wanaharibu mambo?

Mmishonari wa Australia nchini Papua New Guinea Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ulimwengu unawachukulia vipi wamishonari?

"Nyinyi watu mnafikiria nina wazimu kwa suala hili...Lakini nadhani nivyema kuwahubiria watu hawa injili ya Yesu Kristo."

Haya ni baadhi ya maneno ya mwisho ya John Allen Chau aliyoandika katika barua aliyowaandikia wazazi wake kabla ya kuuawa na watu wa kisiwa cha Sentinel kaskazini wiki iliyopita.

Japo hakuwa mmishonari Chau alisema lengo lake lilikuwa kwapelekea injili wa wa jamii ya Sentinel. Hatua yake hiyo imemwezesha kukutana na maelfu ya waumini wa dini ya Kikristo kutoka kila pembe duniani.

Lakini hawa wamishonari ni kina nani? Lengo lao ni lipi? na je wameleta mabadiliko katika jamii duniani ama uwepo wao haujakaribishwa?

Umishonari ni nini?

Japo dini zingine duniani zimetuma wamishonari wao katika maeneo tofauti duniani, wamishonari hao hawajulikani kuliko wenzao wa dini ya Kikristo

Wamishionari kutoka makanisa mbalimbali ya Kikristo hukariri kifungu cha Biblia, ambacho ni maarufu, na ambacho kinapatikana katika kitabu cha Mathayo, ambapo Yesu Kristo anawasihi wafuasi wake "kwenda ulimwenguni kote kuhubiri injili kwa kila taifa."

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wamishonari wa Kikristo wamefanya kazi kwa karne nyingi duniani

Kwa mujibu wa kituo cha Marekani cha mafunzo ya Kikristo duniani, kuna takribani wamishonari 44,000 wanaofanya kazi ughaibuni kwa mwaka huu wa 2018.

Idadi hii inajumuisha wamishonari wa kanisa katoliki, wakiprotestanti, waothordox na makundi mengine ya kidini kutoka Amerika Kaskazini kama vile Mashahidi wa Yehova na wengineo.

Kanisa la LDS ni moja ya makanisa yanayoendeshwa kupitia mpangilio maalum wa kimishonari.

Inasemekana kanisa hilo pekee chini ya mpango wa wamishonari wa Mormon lina wamishonari 66,000 kote duniani.

Kanisa hilo pia limewatuma zaidi ya wamishonari milioni moja katika maeneo tofauti duniani katika historia yake.

Wamishonari hufanya nini?

John Allen (hana uhusiano wowote na John Allen Chau) yeye na mke wake Lena - ambaye ni mkunga na muuguzi - wanafanya kazi kama wamishonari wa kikristo nchini Papua New Guinea kwa miaka 15.

Wanandoa hao wa Marekani "wanalenga kuendeleza injili ya yesu duniani" bwana Allen aliiambia BBC.

"Sio kwamba tunataka watu waamini kile tunachoamini," aliandika katika barua pepe yake kwa BBC. "Bali inahusu watu kujionea wenyewe kupitia maandiko kwenye bibilia."

John na mke wake walijenga kambi ya matibabu kwa watu wa mkoa wa Kamea ambako pea ni makaazi yao miaka kumi iliyopita.

Raia watano wa Papua New Guinea pamoja na wauguzi watatu wa Marekani wanafanya kazi katika kitua cha afya cha Kunai, na wamekuwa wakitoa huduma mbali mbali kwa wakaazi ikiwa ni pamoja na kuendesha kampeni inayolenga wanawake wajawazito na watoto wachanga.

Bwana anasema yeye na mke wake wanajua kuzungumza lugha ya Tok Pisin, na sasa wanjifunza lugha ya Kamea ili waweze kuwasiliana kwa urahisi.

"Ni vigumu kujifunza kuzungumza na kuandika lugha ya watu lakini tunajitahidi," anasema Allen says.

"Kazi za kimishonari siku hizi zinatofautiana hii ndio sababu tunaendesha shughuli tunayofanya," anaelezea.

Andrew Preston, mhadhiri wa somo la Historia katika chuo kikuu Cambridge, anasema kihistoria, baadhi ya wamishonari walikuwa mstari wa mbele kujifunza lugha za jamii wanazohudumia.

"Lakini siku hizi huo ni uwongo," aliimbia BBC. "Lakini miaka 100 iliyopita wamishonari walisifika kwa uwezo wao wakuzungumza kwa ufasaha lugha za kiafrika, kichina na kijapani."

Watu wanasema nini kuhusu kisa cha John Chau?

"Wakati taarifa kuusu mauaji yake ilipoangaziwa baadhi wa watu walisema kuwa ''tulitaka kufanya kazi hiyo pia," aliongeza John Allen.

Japo yeye binafsi hakuwahi kufikiria kuzuri kisiwa cha Sentinel Kaskazini, amewahi kukutana na watu ambao wamewahi kutangamana na watu wa jamii ya Sentinel.

Haki miliki ya picha Instagram/John Chau
Image caption John Chau akiwa kwenye boti

Je umishonari ni mfu wa utawala wa kiimla?

Siku kadhaa baada ya kifo cha John Chau mmishonari wa zamani Caitlin Lowery aliandika kati aukurasa wake wa Facebook.

"Nilipenda sana umishonari ," ujumbe wake ulisema. "Nilidhani nafanya kazi ya Mungu. Lakini kusema kweli nilijihisi vizuri sana."

"Huu ni uwezo wa mtu mwupe huu niukoloni."

Haki miliki ya picha Amazon Conservation Team
Image caption Mmishonari Mark Plotkin akiwa na watu wa kabila la Amazonia

Ulimwengu umekuwa na maoni tofauti kuhusiana na kazi ya wamishonari.

Kihistoria profesa Preston anasema sio wamishonari wote wanafanya kazi ya kueneza dini.

Wamishonari wa kiprotestanti kutoka Marekani walikuwa wakifanya kazi ya maendeleo kwa "kujenga himaya yao".

"Walijiona kwamba wao pia walikuwa na jukumu la kuendeleza sera ya nchi yao."

Hii ndio sababu baadhi ya wamishonari walitumika kuendeleza ajenda ya utaifa.

Hata hivyo bwana Allen anapinga kauli hiyo.

Anasema "Mimi si mjinga kuamini kwamba siku moja nitageuka kuwa mmoja wa watu wa Kamea,lakini kundi letu linafanya kazi kwa lengo kuvunja kadhia ya ukololoni mambo leo kwa kuwawezesha wale tunaowahudumia ili nao waweze kujitegemea."

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii